Kuzomewa Waziri Pinda UVCCM yamvaa mbunge;kinaonekana kuanza kuwachang'anya viongozi wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuzomewa Waziri Pinda UVCCM yamvaa mbunge;kinaonekana kuanza kuwachang'anya viongozi wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  20 SEPTEMBER 2012


  Daud Magesa,Mwanza na Zourha Malisa, Dar

  KITENDO cha wananchi kumzomea Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, kinaonekana kuanza kuwachang'anya viongozi wa CCM, ambapo Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), umetoa tamko likimhusisha mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Ezekiel Wenja, kuwa aliandaa mpango huo.


  Kauli hiyo ilitolewa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Bw.Elias
  Mpanda, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa tamko la kulaani kitendo hicho.

  Alidai mbunge wa Jimbo la Nyamagana anahusika kuwanununlia viroba vya pombe vijana ili wamzomee Waziri Mkuu, Bw.Pinda kwenye
  mkutano huo.

  "Bw.Wenje tunaheshimu ni mbunge wetu, salamu alizokataa kuzitoa Buhongwa alipoombwa na Waziri Mkuu, aliahidi kuzitoa Sahara na kilichotokea ni kwa Waziri Pinda kuzomewa, hivyo aliwandaa vijana kwa kazi hiyo,"alisisitiza, Bw. Mpanda na kuongeza;

  "Nashangaa wanasiasa kuwatumia vijana vibaya na hili ni hatari kwa maisha yetu. Waziri Mkuu anatokana na CCM, sisi UVCCM tunachukia kuona anazomewa, wakati anazumgumzia maendeleo ya nchi na mkoa wetu. Tunalaani wanasiasa waache kuwatumia vibaya vijana kujinufaisha kisiasa."

  "Anayezomea ni mlevi au kichaa siku mambo yakiharibika, waathirika wa kwanza ni kundi kubwa ni vijana kama ilivyotokea Kenya. Huwezi kusema CCM haina vijana wanachama na washabiki, inao wengi. kilichotokea uwanja wa Sahara tunakifahamu kuwa vijana wale walinunuliwa pombe na Mbunge, " alisema

  Alisema Watanzania wote ni ndugu isipokuwa wanatofauti kiitikadi. "Vijana tusifike mahali tuache kugombanishwa na wanasiasa. Ni kitendo cha aibu kiongozi kuwanunulia vijana vileo,"alisema, Bw. Mpanda.

  Bw. Mpanda alisema,kujadili siasa ni kujadili maisha ya watu kwamba siasa inapoharibika shughuli za kiuchumi na maendeleo pia huharibika na kuonya vijana kuacha kuchonganishwa na wanasiasa kwa kuwa wote ni ndugu.

  Alisema baadhi ya wanasiasa wanawatumia vibaya vijana ili kujinufaisha kisiasa. "Ni aibu kiongozi anayeheshimika kuwanunulia pombe vijana wafanye vurugu na kuzomea,"alisema.

  Alisema kwa hali inavyojionesha hivi sasa Watanzania wanaelekea kufanana Kenya, ambao malumbano ya mshindi wa kiti cha Urais Kati ya Rais Bw.Mwai Kibaki na Waziri Mkuu, Bw. Raila Odinga, yaliyosababisha maafa kwa watu kupoteza maisha.

  Kutokana na kauli hiyo mmoja wa waandishi akata kupata uhakika wa ushahidi dhidi ya Bw. Wenje kuhusika na tukio la kuzomewa kwa Bw.Pinda, ambapo baadhi ya waandishi waliingilia kati na kuzua malumbano. AKizungumzia madai hayo, Bw. Wenje alisema ni ya kutapatapa na wanachofanya wanatafuta sehemu ya kutokea.

  Alisema wakiwa Buhongwa watu wa CCM walinyimwa nafasi ya kusalimia wananchi na Waziri Mkuu, Bw. Pinda alipoona hali hiyo alimpa nafasi. "Nilisimama nikasema hii ndiyo Mwanza na salamu zaidi utazipata Sahara," alisema.

  Alisema madai kuwa aliwanunulia viroba wananchi hao si ya kweli. "Watu waliojaa uwanja mzima niwanunulie viroba hizo hela nimezipata wapi...Kweli inawezeka maana uwanja mzima ulizomea," alisema Bw. Wenje na kuongeza;

  "Nilikuwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu tangu asubuhi hadi jioni, sasa huo muda wa kuwanunulia viroba niliupata wapi?" Alisema mkuu wa wilaya alienda mbali na kusema niliwapa bangi vijana hao. "Kama wana ushahidi si wanikamate na kunipeleka mahakamani," alisema na kuongeza; "Waziri Mkuu alikiri mwenyewe kuwa ameona watu wa Mwanza."

  Wakati huo huo, Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kitendo cha kuzomewa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ni dalili za wananchi kuchoshwa na viongozi waliopo madarakani kushindwa kutimiza ndoto zao.

  Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julias Mtatiro, alipokuwa anatoa maoni yake kuhusu tukio la wananchi mkoani Mwanza kumzomea waziri Pinda.

  Alisema kuwa wananchi wamechoshwa na CCM pamoja na viongozi waliopo madarakani, kwani wameshindwa kutimiza wajibu wao tangu walipoingia madarakani.

  "Wananchi wameoneshwa kuchoshwa na chama kilichopo madarakani tangu miaka 50 ya Uhuru hadi sasa ndoto zao hazijakamilishwa ugumu wa maisha upo palepale," alisema, Bw. Mtatiro.

  Mbali na hilo, Mtatiro aliongezea kuwa kuzomewa pia kunasababishwa na kiongozi mwenye amepeleka ujumbe gani kwa wananchi wake.

  "Wananchi wamefikia hatua ya kumzomea waziri mkuu kwa tabia yake ya kutotoa majibu kwa wananchi na kusababisha wananchi kukosa amani naye kama kiongozi wa ngazi ya juu" alisema.

  Aliongezea kuwa kiongozi huyo amekuwa akitumiwa kwenye mfumo mzima wa utawala, hivyo hali hiyo inasababisha wananchi kuchoshwa na kiongozi huyo.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Ndio Fisadi Lau Masha anasema ataweza kuwa MBUNGE tena NYAMAGANA ? Labda wamkatie JIMBO LINGINE kama

  walivyofanya kugawa ILEMELA na NYAMAGANA... Watengeneza Jimbo la zamani la BABA yake UZINZA...
   
 3. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCM msiangaike kutafuta mchawi...ni nyinyi wenyewe....wale vijana waliomwitaga Mkapa fisadi walitumwa na CDM? wale waliompopoa mawe JK kule mbeya nao Walitumwa na Sugu?
   
 4. T

  TATOO Senior Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mizengo pinda akafanye kazi ya kuwafurahisha wananchi hawatazomea,,mana binadam anakuwa na hulika mbili ukimfurahisha atacheka kwa furaha na kukupigia makofi na ukimuudhi atakuzomea,,,so afanye yaliyo majukum yake kiukweli
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wenje ndiye kasababisha vijana wakakosa ajira, Wenje ndiye amesabisha maji kukosekana, Wenje ndiye amesababisha huduma za afya kudorora!

  UVCCM should thank thier lucky stars waziri mkuu hakurushiwa mayai viza. Sijui kama viongozi wa nchi wanaelewa ni jinsi gani wananchi wamechoshwa na ubabaishaji?
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  hivi UVCCM hawana kazi zaidi ya kuvaana tu??

  mara wamvaa wenje, mara wamvaa slaa, mara wanavaana wenyewe

  poooooooooooooooooofff
   
 7. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  wacha waendelee kudanganyana
   
 8. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...kwa sisi wenye hekima zetu tunajua ya kwamba waziri mkuu alizomewa sikunyiiiiingi kabla ya hata ajafika Mwanza!?...waziri mkuu alizomewa na wakazi wa MWANZA tangu mwaka 2010 kwenye box la kura,lakini kwakuwa uwezo wake wa kuona unaishia kwenye pua yake alishindwa kuliona hilo...huku Mwanza CCM imebakiza bendera,tume ya uchaguzi,polisi na vikaragosi vichache vinavyo vaa tisheti na kofia za kijani na njano..."LIWALO NA LIWE"...
   
 9. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwani hapakuwa na a ccm wakashangilia......tatizo ukizoea kushangiliwa ndio hivyo liwalo na liwe
   
 10. neva cin neva bin

  neva cin neva bin Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona CCM huwa mnawapa vijana ubwabwa kwenye mikutano wanaishia kusinzia na kuchafua hewa, bora viroba vinaamsha hasira za umasikin wetu
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hawa wana lalamika kuzomewa, je aliye rushiwa mawe asemeje?

  Liwalo na liwe
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  aisee hakuna kitu naichukia km uvccm, yaani km uniwekee kinyesi cha mlevi wa tembo.
   
 13. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  UVCCM imebakia kuwa kijiwe cha kutoa matamko badala ya kuangalia mustakabari wa taifa letu wanatia aibu sana hawa vijana.
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo na JK alivopigwa mawe mbeya n ayo ni chadema ..CCM muwe mnatumia akili kufikiri sio mnakuwa kama walevi
   
 15. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hao ni wehu wenje hataamasisha mji mzima watafute suluhu kwa vituko vyao vya ufisdi na kuchomeka majaji feki hilo ndio mchawi wao wasitafute visingizio
   
 16. n

  nyanyonyi Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado watazomewa sana mwanzoni tulimwamini sana pinda tukiamini kweli ni mtoto wa mkulima kumbe alikuwa anatuzuga.uliona wapi waziri mkuu anashindwa kuwa na maamuzi yake binafsi badala yake kila kitu lazima akamuulize baba tabasamu.
   
 17. n

  nakuru Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawaonea sana huruma ma-ccm kwani Mungu alishawapiga upofu, kila kinachotokea kwa wao kutokubalika wanasema yametengezwa na CDM huu ni upofu toka kwa Mungu, wataendelea kusema hivyo hadi watakapomuona Dr. Slaa anafunguliwa mlango wa kuingia Ikulu hapo ndipo watanyamaza!
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,815
  Likes Received: 36,910
  Trophy Points: 280
  Kama pinda alizomewa kwa sababu wananchi walinunuliwa pombe basi tumekuwa tukinyweshwa pombe na ccm kwa miaka 50.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60


  huyo katibu wa uvccm aache kutukana wana mwanza, waliomzomea si vijana wanywa viroba, bali ni wana mwanza waliochoshwa na ghiriba , hila na ulaghai wa ccm.Nikumbushe wakati wamdororo wa uchumi serikali ilisaidia wafanya biashra wa pamba waweze kusaidia wakulima wasikose soko la pamba.Lakini mpaka sasa mkaguzi mkuu wa serikali alibainisha mapungufu mengi na hada ufunjaji wa fedha hizo.Leo kuna tatizo la soko la pamba waziri mkuu na raisi wake waliishia kusema mabadiliko ya soko duniani, bila kujali athari nmna gani wakulima hao watateseka.Pia soko la minofu ya samaki bei yake imeteremka kwa 50%, serikali ikatoa ripoti ya upotoshwaji na kuwaacha wavuvi bila msaada.Leo wanatafuta mchawi, kwa uzembe na kutojali wanyonge.Wenje hana ubavu wa kulazimisha wanamwanza wawe walevi au wazomee kama kuna mazuri, hiyo ni dalili tosha kuwa watu wamechoka maisha mabovu.
   
 20. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwani mbunge alimzomea?
   
Loading...