No! Unajua ujasiri wa mke kumruhusu mume aoe mke wa pili kwa 80% mume hawezi kuleta ujinga wa kuenda nje tena. Na mwanamke anatakiwa awe na Amani kuwa leo yupo kwa mwezangu.
Faida: mahitaji wote watapata
Ujasili wa kujua yupo kwa mwenzio, inafaida gani kwa mke? sawa yupo kwa mwenzio, mtoto kaugua usiku upigie simu aje akusindikize hospitali au uite majirani au uende mwenyewe?si bora ujue upo peke yako kuliko kujidai unamume wa mitala kila leo unaupweke,unahabari ya kumshirikisha umsubiri itakapofika zamu yako aje kwako, unahamu nae ni zamu ya mwenzio,ikifika zamu yako upo MP, ni ngumu sana hakuna mwanamke anependa mitala,hata akijishaua vipi ndani ya moyo anaumia mume anapokuwa kwa mwanamke mwingine awe mke mweza au kimada inauma, Raha ya mume ulale nae uamke nae,ukikohoa usiku ajue,ukiwa na hamu nae umpate sio kukosa usingizi yeye yupo kwa mwenzio.
Pia ukitafakari sana mitala ni uchafu, wanaume wengi wanawake wengi ni uchafu,na mapenzi ya siku hizi wanaume wanacopy kila kitu kwenye mitandao ni tabu, pata picha ananyonya mate ya mwenzio,matiti ya mwenzio kesho anakuja kwako.wengine wananyonya mpaka papuchi ya mwenzako alafu jioni anataka denda kwako, uwii nishee bila kujua kwa kujua na kuhalalisha sitaki bora niwe peke yangu. Hivi mpaka mwanume anakuletea mke mwenza bado unajidanganya kuna upendo?au ndo uoga wa kuwa peke yako?
Na watoto tutawafunzaje?ruksa kuoa wake wengi na kwamba binti yangu ruksa kujenga mahusiano na mume wa mtu ili aolewe mitala? "Na utafiti mwingi unaonyesha wanaume wengi wanashindwa kuwaridhisha wake zao". lakini wanajidai kutaka mitala.
Any way maisha kuchagua, unajisikia kuwa na wengi kuwa nao ni maisha binafsi. ila usilazimishe wanawake wote wakubali mitala kwa wengine hawawezi ndo maana mwingine akijua unakimada ndoa inakufa, ukioa mke wa pili yeye anakupisha usimshangae ndo asili yake hawezi uke wenza, wengine wanavumilia mitala na mateso juu tunatofautiana, ukipenda mitala chagua walio tayari kwa mitala wapo wengi tuu wanaonekana kwa macho ya kawaida kabisa mataani, maofisini wamejaa.
Pia ni dhambi kubwa wakati unamsaka unamuaminisha ni yeye tu, ukioa unaanza kusaka mwingine, wengi mmeapa mpaka mbele za watu na Mungu kwa shida na raha mpaka kifo kiwatenganishe, kesho unamtwisha mizigo mwenzio kwa vimada na kuongeza wanawake.
Ndo maana wanaume wengi wanakufa mapema wanajitwika majukumu mengi wasiyoyaweza, wengi uchungu wa kutelekeza familia na kushindwa kuziangalia vizuri sababu ya mitala unawaandama sana, na majuto ya kuwa na mitala, na usaliti waliofanya kwa wake zao unawaandama sana, na mara nyingi amani kati ya mke na mke na watoto inakuwa ndogo.mwisho unakufa kwa stress na maradhi ya zinaa, wanaume wanajiroga wenyewe.