Wewe kama unaishi DSM unatakiwa kuwa macho kuliko swala wa serengeti ambaye hofu yake siyo simba tuu, kuna threats nyingi sana mafisi, mwewe ,tai , mbwa mwitu, wawindaji haramu na kadhalika. DAR nako kuna utapeli wa kila namna kuanzia huo wa madawa ya mifugo, wauzaji wa bidhaa fake, wezi wa mfukoni,vibaka, majambazi, wauzaji wa viwanja fake, watoza ushuru(TRA) fake, mapolisi fake, michango ya harusi fake, michango ya ujenzi wa makanisa ambayo haifiki kanisani, tegemeza jimbo, changia jumuia ndogo ndogo,wezi wa majumbani wanaoingia kama wasoma mita wa tanesco, changia ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari za kata, michango ya kila siku isiyoisha kwa ajili ya watoto wetu wanaosoma shule zetu za msingi za kayumba, nk,nk,..orodha ni ndefu cha msingi ukitaka kuishi DAR kwa raha usimwamini mtu yoyote sii padri, shehe, mwenyekiti wa mtaa, katibu kata, katibu tarafa wala mzee wa upako ....Napendekeza ianzishwe thread kila mtu aweke kila aina ya utapeli anaoufahamu upo DAR ili tuwanusuru members wenzetu.