Kuweni makini na baadhi ya pharmacies! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuweni makini na baadhi ya pharmacies!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by patience96, Nov 17, 2011.

 1. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Nimegundua kuwa baadhi ya wafanyakazi (Pharmacists?) ktk Pharmacies za madawa ya binadamu(private Pharmacies), hawana taaluma yoyote ya madawa ya binadamu! Baadhi yao wamekaririshwa tu na wakati mwingine mambo yakiwa magumu si ajabu ukakuta wanapekua vitu fulani fulani ktk counterbook zao au kupiga simu kwa maboss wao ili kuhitaji msaada.
  Hivi majuzi nilikwenda kununua dawa ya kutibu malaria ktk Pharmacy fulani, kabla ya kwenda pale, nilishaandikiwa na Daktari dawa ya "Artesunate/Thaitanzunate" dawa ninayotumia mara kwa mara. Bahati mbaya sikupata pale Pharmacy; mama mmoja mfanyakazi wa pale alinishauri nitumie "Duo-Cotecxin[SUP]R [/SUP]" kwamba ni nzuri tu aidha haina side effects, sikuwa na option kwani sehemu hile Pharmacy ni moja tu!
  Yule mama alinipatia prescription kuwa dose ya dawa husika ni: 3/3/2 kwa maana ya siku ya kwanza vidonge 3, siku ya pili 3 na siku ya tatu 2.
  Kwa vile sikuwa na imani na mama yule kutokana na mazingira niliyoyaona pale, niliangalia leaflet ya dawa ile na ilisomeka hivi:

  Weight Age Day 1 Day 2 Day 3
  >40kg >14yrs 3 3 3 e.t.c.

  Nilipomwonyesha yule mama sehemu hii, alipata kigugumizi kisha akaniambia nifanye alivyonielekeza yeye, baada ya kumbana kidogo aliangalia ktk kiji-counter book kisha aliomba muda kidogo ili awasiliane na boss wake. Bahati nzuri sauti ya boss wake nilikuwa naisikia akamwambia yule mama kuwa bei ya dawa ni tshs. 8,000/= (wakati nilishalipa 10,000/=), na dosage ni 3/3/2. Nilichukua namba ya simu ya yule boss na kumpigia, baada ya kumweleza wasiwasi wangu alikiri kuwa yeye ni Nurse nimpe dk 3 ajaribu kuulizia kwa Daktari pale anapofanya kazi (Hospilati teule ya Wilaya)! Majibu ya Daktari yalikuwa 3/3/3! Nilijaribu kumpigia rafiki yangu pale Sekou Toure Mwanza (Daktari wa binadamu), aliniambia dose ya dawa ile ni 3/3/2! Nilishindwa kushangaa nini kinaendelea!

  Wataalamu wanaofahamu mambo haya, What is the usual mean dose of Duo-Cotecxin[SUP]R[/SUP] for an adult person above 35yrs and above 75 kg of weight?
   
 2. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,419
  Likes Received: 1,727
  Trophy Points: 280
  pole sana mkuu! Usipokuwa makini hawa wauza dawa watakuua hawajuhi kitu, wengi ni ndugu wa wenye maduka,hata hivyo nakupongeza kwa kuwa na tabia ya kusoma leaflets(maelekezo ya dawa husika)

  Kuhusu Duo-Coatexin dozi yake kwa uzito ulioutaja ni vidonge 3 kila siku kwa siku tatu ambayo wenyewe uandika 3, 3, 3. Huyo mhudumu na nesi walisahau jambo moja:awali dawa ile ilikuwa ikitolewa 3, 3, 2 watengenezaji (kampuni moja huko China )walibadilisha dose nadhani baada ya majaribio ya awali kuonyesha dosari kidogo. Hata ufungashaji wa awali ni tofauti na huo wa dawa uliyoinunua.
   
 3. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,279
  Likes Received: 907
  Trophy Points: 280
  Pole ndg pia hongera kwa kutomuamini huyo muuza dawa.Yamenitokea leo ktk pharmacy moja mtoto wa miezi 9 anapewa ALBENDAZOLE gm 500, 12 AMEZESHWE 2*3.jamani TFDA mnafanyakazi gani hawa wauza madawa hawana taaluma hiyo.Eti wengine wamepata kozi ya HUDUMA YA 1 tu kesho ni Muuguzi. Mtatuuwa!
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa wameclem mimi huwa natumia iyo dawa kwa kusoma leaflet na huwa inanitibu vyema tuu.
  Afterall dawa hawajatengeneza wao na competence yao wengi ni questionable
   
Loading...