Kuwe na utaratibu wa madokta na wauguzi kupimwa afya zao pindi waanzapo kazi rasmi na kila baada ya miezi 3

iamriq_arthur

JF-Expert Member
May 1, 2021
377
884
Habari wana JF !

Nina pendekezo kuhusu watoa huduma za mahospital na sehemu zote za huduma ya afya, kuwe na utaratibu wa kupimwa afya zao ili wagongwa wanapokuwa mahospital wawe na amani na huduma wapatazo kwenye vituo hivyo.

Kuna baadhi ya hospital asilimia kuwa ya wauguzi wa hospital hizo wameugua (wagonjwa wa ukimwi) na inafahamika kabisa, lakini kutwa kuwachoma sindano tu wagonjwa.

Wengine wapo sekta ya kuwazalisha kuna mama, sasa dokta mgonjwa wa ukimwi anakuwa kitengo cha kuwazalisha kina mama na kuwachoma masindano au kuwasafisha vidonga na ameugua, akiwa na roho mbaya ataweza kuwa anawaambukiza wagongwa wengine waliokuja hospital kwaajiri ya kutibiwa ugonjwa tofauti, wakitoka hospital wanatoka na ugonjwa ambao hawakua nao.

Dokta mwenye Uukimwi anajitolea damu anachangaya kwenye dawa nyingne na anamchoma nayo mgonjwa aliekuja kutibiwa kwa ugonjwa mwingne.

Naomba vituo vyote vya afya waiguzi wawe wanapimwa afya zako kila baada ya miezi mitatu, watakaogundulika wameathirika ukimwi wawe wanafukuzwa kazi.
 
Wew unashida kubwa Sana kichwani mwako kwanza ilibidi upewe elimu ya HIV and AIDS kiujumla Maana inaonekana unaunyapapa Sana Na Nani alikwambia waathirika hawatakiwi kuwa wauguzi au wafanyakazi kwa maana hiyo wew ukiathirika ukiende Hospital daktari asikufanyie sugery kisa wew ni mgonjwa yey ni mzima sababu akikufanyia sugery utamuambukiza kitu unachotakiwa kuelewa ni kwamba wale ni qualified hawakuamka tu nakuanza kuchoma Sindano watu ovyo ovyo wanajua tahadhari zote.
 
Kwanza kitaaluma kitu kama hicho kwamba mtumishi wa afya akuambukize ugonjwa kimaksudi hakiruhusiwi.

Ni vyema ukaongea kwa kuleta ushahidi kabisa kuliko kusonta vidole tu.

Daktari au Nesi kuwa na ugonjwa huo haimaanishi hawezi kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa. Wewe kwa sababu tayari neno Ukimwi unaliogopa, hali hiyo imepelekea kuwa na uoga wa kuhudumiwa na hao kwamba utaambukizwa.

Haya tuseme wamepimwa, wakishapimwa wakakutwa nao, kwamba wafukuzwe kazi au? Sababu ya kupima ni hipi, na ugundue nini, na ukishagundua kitokee nini? Hayo ndio maswali ulitakiwa kujiuliza kabla ya kuleta mada.

Ukitoka kwa madaktari na manesi utataka na waalimu nao wapimwe, utataka na wauza chakula wapimwe.

As long as tayari huo ugonjwa unauogopa utataka ata jirani yako apimwe.
 
Kwanza unatakiwa kujua hao waliopata huo ugonjwa hakuna aliyepata kwa kutarajia.

Madaktari na manesi wengi wanapata magonjwa kwa sababu ya hao hao wagonjwa. Kuna Daktari mmoja wa Bugando alifariki kwa Corona kwa sababu ya wagonjwa aliokuwa anaenda kuwatibu. Anakuja mgonjwa anamatatizo ya upumuaji, daktari hajui chochote wakati wa mahojiano nae anaambukizwa hayo magonjwa ya upumuaji kama Ebola.

Au anakuja Mama Mjamzito hospitalini hasa hizi za serekali, ameanza kusukuma, gloves na vifaa vya kuzalishia zimeisha hili kuokoa maisha ya mtoto na mama analazimika kutumia njia mbadala kumsaidia ikiwemo kutumia mikono bila gloves. Kumbe mama alikuwa tayari ana maambukizi, nesi wa watu nae anaambukizwa.

Heshimu sana kada za afya kwa sababu maisha yao yako mikononi muda wowote. Wagonjwa mnaowakataa mtaani ndio wanaenda kukutana na hao madaktari. Imagine mgonjwa wa Ebola, anaingia anamkuta daktari, daktari nae kama hakujikinga vizuri tayari nae anaambukizwa.
 
Acha unyanyapaa...hata wakipimwa kama kuupata unaweza ukaupatia hapo nyumbani kwako umekaa ndani ....

Mmh we nae umejifunzia uongo wa namna hyo tena, yan ukimwi uupate ukiwa umekaa nyumbani.?.
Hebu nambie unaanzaje kuupata
 
Nadhani kama uko matured enough umenielewa sio mpk utafuniwe...ww kama ni ke au me...unaweza ukajilinda na hao madaktari huko hospitalini ila ukaletewa ugonjwa na partner wako hapo nyumbani...kama uko vzr upstairs sikutegemea hili swali...
 
Huyo bado mtoto, akili bado
 
Nadhani kama uko matured enough umenielewa sio mpk utafuniwe...ww kama ni ke au me...unaweza ukajilinda na hao madaktari huko hospitalini ila ukaletewa ugonjwa na partner wako hapo nyumbani...kama uko vzr upstairs sikutegemea hili swali...

Sawa mke wangu
 
Hoja yako ina mashiko japo wasiotaka kusikia mawazo mbadala watakutukana. Zamani madaktari na wakunga wakitoka kuzalisha walikuwa hawanawi mikono wala kutumia gloves, kisha wanaenda kuzalisha mwingine. Wanawake walikufa sana wakati wa kuzaa. Wakati huo watu hawafahamu kuwa kuna vimelea vya magonjwa. Daktari mmoja akapendekeza kuwa kutonawa ndiko kunasababisha magonjwa hayo, hivyo kwenye wodi yake akasema iwe lazima kunawa baada ya kumhudumia mgonjwa. Watu walipinga sana, walisema mkoloni na anakichaa na maneno mengine.

Alikomaa na msimamo wake na wakashangaa wodi yake vifo vinapungua kwa kasi sana. Ndiyo hospitali nzima na sekta nzima ya afya kuanza utaratibu wa kusanitize na kuvaa vifaa vya kujikinga. Kama wapishi na mama ntilie wanatakiwa kupima afya vipi kwa madaktari na manesi?
 
Habari wana JF !

Nina pendekezo kuhusu watoa huduma za mahospital na sehemu zote za huduma ya afya, kuwe na utaratibu wa kupimwa afya zao ili wagongwa wanapokuwa mahospital wawe na amani na huduma wapatazo kwenye vituo hivyo.

Kuna baadhi ya hospital asilimia kuwa ya wauguzi wa hospital hizo wameugua (wagonjwa wa ukimwi) na inafahamika kabisa, lakini kutwa kuwachoma sindano tu wagonjwa.

Wengine wapo sekta ya kuwazalisha kuna mama, sasa dokta mgonjwa wa ukimwi anakuwa kitengo cha kuwazalisha kina mama na kuwachoma masindano au kuwasafisha vidonga na ameugua, akiwa na roho mbaya ataweza kuwa anawaambukiza wagongwa wengine waliokuja hospital kwaajiri ya kutibiwa ugonjwa tofauti, wakitoka hospital wanatoka na ugonjwa ambao hawakua nao.

Dokta mwenye Uukimwi anajitolea damu anachangaya kwenye dawa nyingne na anamchoma nayo mgonjwa aliekuja kutibiwa kwa ugonjwa mwingne.

Naomba vituo vyote vya afya waiguzi wawe wanapimwa afya zako kila baada ya miezi mitatu, watakaogundulika wameathirika ukimwi wawe wanafukuzwa kazi.
Duuh hio ni kiboko ya wenyewe
 
Hivi hamjui na nyie huwa mnatuambukiza magonjwa yenu ya ajabu ajabu ?
 
Mleta mada ana hoja muhimu sana na asipuuzwe hata kidogo.
Watu wengi hawana ufahamu na kitu/mada hii.

1. Kwa madaktari na manesi kuna kitu kinaitwa “Exposure Prone Procedures (EPPs)” hasa upande wa operation au surgery. Hali za afya za watumishi wanaojihusisha na EPPs ni muhimu zifahamike na wapewe kinga (chanjo) inapowezekana. Iwapo daktari au nesi ana ugonjwa mfano hiv, inabidi asifanye kazi zinazohusu EPPs. Afanye kazi ambazo si za EPPs.

EPPs = Viganja au vidole vya daktari au nesi vinapoingia chini ya ngozi ya mgonjwa, kwa maana nyingine ndani ya jeraha au kidonda wakati wa kufanya operation.

2. Vile vile madaktari na manesi wanashauriwa wachukue tahadhari wafanyapo kazi zao “Universal Precautions”
Yaani kutumia vifaa vya kinga kazini.

3. Kuosha mikono (Hand washing) kabla na baada ya kumhudumia mgonjwa inasaidia mno mno kupunguza ueneaji wa magojwa (Infections) hospitalini na husaidia kupunguza Vifo.

4. Kwa ujumla ajali hatarishi kazini wakati mwingine haziepukiki.

Hili ni somo refu ila hapo ni kwa ufupi tu.
 
Habari wana JF !

Nina pendekezo kuhusu watoa huduma za mahospital na sehemu zote za huduma ya afya, kuwe na utaratibu wa kupimwa afya zao ili wagongwa wanapokuwa mahospital wawe na amani na huduma wapatazo kwenye vituo hivyo.

Kuna baadhi ya hospital asilimia kuwa ya wauguzi wa hospital hizo wameugua (wagonjwa wa ukimwi) na inafahamika kabisa, lakini kutwa kuwachoma sindano tu wagonjwa.

Wengine wapo sekta ya kuwazalisha kuna mama, sasa dokta mgonjwa wa ukimwi anakuwa kitengo cha kuwazalisha kina mama na kuwachoma masindano au kuwasafisha vidonga na ameugua, akiwa na roho mbaya ataweza kuwa anawaambukiza wagongwa wengine waliokuja hospital kwaajiri ya kutibiwa ugonjwa tofauti, wakitoka hospital wanatoka na ugonjwa ambao hawakua nao.

Dokta mwenye Uukimwi anajitolea damu anachangaya kwenye dawa nyingne na anamchoma nayo mgonjwa aliekuja kutibiwa kwa ugonjwa mwingne.

Naomba vituo vyote vya afya waiguzi wawe wanapimwa afya zako kila baada ya miezi mitatu, watakaogundulika wameathirika ukimwi wawe wanafukuzwa kazi.
Kwanza kabisa Punguza uoga hakuna mtu mwenye Roho hiyo unayofikiria Maana umefikiria vitu vikubwa sana ambavyo kiuhalisia ni Impossible Hasa kwa kada ya afya uliyotaja..Watu walio na weredi na waliosoma Ethics kwa muda mrefu..
Na ukikuta Wasio na weredi ni 2 kati ya 100..

Na hata hao hawafikii Level ya kusababisha Matatizo makubwa kwa wagonjwa...kwa hiyo hicho ulicho waza ni impossible..

Yaani kifupi vyote haviwezekani..

Umepropose kuhusu Watoa huduma kufanyiwa checkup hiyo ni sheria ya kikanuni kwamba kabla hajaanza kazi lazima afanyiwe check up na Daktari wa Serikali ili kuthibitisha...

Na ipo Chini ya Standing order of the public services ya mwaka 2009 (KANUNI ZA KUDUMU ZA UTUMISHI WA UMMA 2009) Kipengele au Kanuni D.16
Screenshot_20231031-082108.png

Ila kuendelea kumpima Kwa kigezo cha kupreviw au kut9a majibu ya Afya yake hairuhusiwi kisheria na Ni kinyume kutunga sheria yoyote au Kanuni au Sera Ambayo itabdilisha au kuexpose Privacy and confidentiality yake...
Hii ni kwa mujibu wa HIV and AIDS (Prevention and Control) ya Mwaka 2008 kifungu cha 28 cha sheria
Screenshot_20231031-083449.png

Lakini kingine Jua kabisa kwamba Hakuna mtu stakaye lazimishwa kisheria kupima HIV kwa sababu ni kinyume cha sheria Hiyo hiyo..
HIV and AIDS (Prevention and Control) ya Mwaka 2008 kifungu cha 15 cha sheria hiyo

Screenshot_20231031-083158.png

Tuseme bhasi amelazimisha na ameruhusiwa na sheria kukupima na amekukuta na HIV pia hairuhusiwi kuachishwa kazi kwa Ajili ya HIV/AIDS

Kwa mujibu wa Kanuni Za Ajira Na mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora) Za mwaka 2007 ambazo zimeandaliwa chini ya sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na zipo kwenye Tangazo la Serikali no 42 la Tarehe 16/02/2007 Kanuni Namba 20

Screenshot_20231031-081650.png

Ila endapo kama atapatwa HIV na akashindwa kuhimili kazi kama kanuni hiyo hiyo kanuni namba 19 inavyosema...
Screenshot_20231031-081632.png

Vinginevyo haiwezekani kwa hicho kitu....

Naomba nikutoe hofu kwamba Hospitali zote kwa ngazi zote..zinatoa huduma Stahiki na kwa Mujibu wa sheria na taratibu huku ikizingatia Sheria na Miongozo iliyowekwa na hakuna atakayeweza kusababisha Matatizo kwa Wagonjwa Hata kama akitaka....
 
Back
Top Bottom