Kuwalaghai Wanawake Sio Kosa ...

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20

3647778.jpg


Mahakama nchini Korea Kusini imefuta sheria ambayo wanaume walikuwa wakitupwa jela miaka miwili kwa kuwapa ahadi za uongo za kuwaoa wanawake ili wafanye nao mapenzi na kisha kuwatelekeza.Wanaume nchini Korea Kusini ambao huwaahidi wanawake kuwaoa ili wafanye nao mapenzi na kisha kuwakimbia, hawatapandishwa tena kizimbani baada ya sheria iliyokuwa ikiwabana kufutwa.

Kitengo cha sheria namba 304 cha katiba ya Korea Kusini kilikuwa kikiamuru adhabu ya kutupwa jela miaka miwili wanaume wote wanaowahadai wanawake kwa kuwaahidi kuwaoa ili wafanye nao mapenzi.

Sheria hiyo imefutwa baada ya kuonekana inawanyima wanawake haki zao za kuamua wanaume wanaowapenda.

Sheria hiyo pia ilikuwa ikitumiwa vibaya na wanawake ambao waliwalaghai wanaume kufanya nao mapenzi na kisha kuwadai kiasi kikubwa cha pesa wakiwatishia kuwafikisha mahakamani kwa kudai kuwa walifanya nao mapenzi baada ya kuahidiwa kuolewa.

Kutokana na sababu hizo, mahakama kuu ya Korea Kusini imeamua kuitupilia mbali sheria hiyo.

Source: AFP
 
Back
Top Bottom