Larusai Mux
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 979
- 277
Heshima kwenu wakuu!
Uwajibikaji wa viongozi wa umma na kiserikali si jambo jipya bali ni kitendo cha kuonesha kwa vitendo kuachia ngazi kwa kuto kutekeleza wajibu na majukumu waliyopewa na umma au na viongozi walio juu yao au kwa kutokutimiza matarajio ya majukumu yao.
Rais mstaafu mh Ali Hassan Mwinyi aliwahi kuwajibika kwa kujiuzulu alipokuwa waziri wa mambo ya ndani,Mh Edward Lowasa mwaka 2008 aliwahi kuwajibika kwa kujiuzulu alipokuwa waziri mkuu kwa kashfa ya Richmond, mawaziri kadhaa waliwahi kuwajibishwa kwa tuhuma mbalimbali wakiwamo mawaziri kadhaa wa nishati na madini prof Sospeter Muhongo, Mh Kagasheki,pamoja na waziri wa mambo ya ndani mh Lawrence Masha,na wengine kadhaa kwa kashfa au kwa kutotimiza majukumu fulani na kusababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia au kuliingizia taifa hasara!
Turudi kwenye kuwajibika na kuwajibishwa kwa viongozi wa umma na kiserikali,kwa siku za karibuni na hata Jana tumepata taarifa za matukio ya mauaji zaidi ya 10 huko Kibiti Pwani na raia wasiokuwa na hatia pamoja na asikari wetu jumla ikiwa ni zaidi 20 wakipoteza maisha kwa mashambulizi ya aina mbalimbali ya kutumia silaha za moto nyie ni mashahidi! ,lakini cha kushangaza hatujasikia kuwajibika kwa wizara husika au viongozi wahusika wa usalama wa raia na Mali zao.
Ni jambo la kusikitisha kuona ni zaidi ya miezi 6 sasa matukio yakiendelea na ndugu zetu wasiokuwa na hatia kuendelea kupoteza maisha bila viongozi husika kuwajibika au kuwajibishwa, je ni mpaka wafe wangapi ndio tuone Uwajibikaji? Je raia wachukuwe jukumu la kujilinda?
Niitake wizara husika na viongozi husika kuwajibika sasa ikiwa ni muda u naenda huwa watu wakipoteza maisha!
Pia jf iwe ni sehemu ya kuhamasisha Uwajibikaji wa viongozi Hao Kwani ni janga kwa taifa na haitakiwi kukaa kimyaaa.
Naomba kuwasilisha