Kuwa na imani ya dini au Mungu katika bara la Afrika ni mtaji wa maisha tulivu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,597
46,221
Africa ni bara ambalo karibia asilimia 99 ya watu wake wanaamini katika dini. Ukitaka Kuishi bila dini ukiwa barani Afrika ujipange sawa sawa.

Hizi ndizo adha utakazozipata ukiwa huna dini au haumuamini Mungu na unaishi Africa.

1. Utakuwa mtu wa kushangawa kila mahali kwa sababu asilimia 99 ya watu hawajawahi kukutuna na mtu asiye na dini au haamini Mungu. Wengi watafikiri unafanya mzahaa au umechanganyikiwa. Tegemea wewe kuwa ndiye mtu wa kwanza kukutana nao ukiwa huna dini. Mimi sijawahi kukutana na mtu ambaye hana dini au haamini Mungu, huwa nawasoma tu mtandaoni.

2. Utawekwa mbali na ndugu zako, mara nyingi wataona kama unawaletea balaa au mikosi katika shughuli zao.

3. Kama ni mwanaume na huna pesa Itakuwa vigumu kwako kupata mwanamke mzuri wa kuoa. Wanawake barani Afrika ni watu wa kidini sana na karibu kila kitu wanakiunganisha na mambo ya kidini.

4. Kama ni mwanamke haitakuwa rahisi kupata mtu wa kukuoa hususani kama umefanikiwa sana. Wanaume wengi barani hapa wanaamini mwanamke aliyejikita katika dini ni msaada kwao kuiombea familia, kuwakumbusha wajibu wao kiimani na kuwasimimia watoto kiimani.

5. Shuguli karibia zote za Serikali, michezo na hata binafsi huwa lazima zihusishe aina fulani ya imani za kidini mfano Maombi, sadaka, mahubiri n.k hivyo itakubidi uwe mvumulivu wa hayo yote.

6. Watoto wako itakuwa vigumu kuwalea nje ya mfumo dini. Watakuwa kituko katika jamii kama hawatashiriki mambo ya kidini na itawaathiri sana kisaikolojia.

7. Mwisho, ukifa utazikiwa kidini tu na kama una ndugu wa dini fulani utawapa tabu sana kupata watu wa kuendesha maziko yako.

Wale wote mnaofikiria kutokuwa na dini katika kipindi hiki na Barani hapa yawekeni haya pia akilini mwenu.

It won't be walking in the park.
 
Au sio
 
Back
Top Bottom