barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
KUWA MTOTO, NDUGU AU RAFIKI WA RAIS SI DHAMBI.
Uteuzi wa Happy Senenda Willium, umeleta maneno mengi. Kuna wanaosema huyu ni mototo wa kuzaa wa Rais Magufuli na wengine wanasema ni mtoto wa kumlea. Vyovyote vile, ni kwamba huyu ni jamaa wa karibu wa Rais Magufuli. Hoja hapa ni kwamba si dhambi kuwa mtoto wa Rais.!
Kwenye mitandao ya kijamii, inajadiliwa kwamba Rais, kakosea kumchangua mtu aliye karibu naye kuwa mkuu wa wilaya. Wanafikiri hapa kutakuwa na mgongano wa maslahi. Kelele nyingi zinapigwa na vijana wa CCM, ambao walipambana kufa na kupona kuhakikisha Rais Magufuli, ana shinda na kuwa Rais wa tano wa Tanzania. Kusema ukweli wenyewe walifanya kazi kubwa, haikuwa kazi nyepesi kupata ushindi. Sote tulishuhudia upinzani mkubwa. Sasa uteuzi umekwisha, na milango imefungwa, vijana hawa wameachwa nje. Roho inauma na hasa baada ya kuona Rais, amemteua mtoto wake.
Hapa kuna hoja mbili za msingi: Kwanza kuwa mtoto wa Rais, si kigezo cha kutochaguliwa nafasi yoyote ile katika utumishi wa umma. Mtoto wa Rais naye ni mtanzania kama walivyo wengine. Pia, vigezo muhimu ni uwezo, elimu na uzalendo. Kama Happy, ana uwezo, amesoma na ni mzalendo, kwa nini asiwe Mkuu wa wilaya, hata kama ni mtoto wa Rais? Yeye hakuchaguwa kuwa mtoto wa Rais, amejikuta ni mtoto wa Rais. Haiwezekani akaachwa, asipewe nafasi ya kulitumikia taifa lake, eti kwa vile yeye ni mtoto wa rais.
Hoja ya pili ni ile ya vijana wa CCM, ambao wameanza kupiga kelele kwamba Rais, kawasahau. Hawa, hawana uzalendo! Ni kweli, wengi tulijitolea kumsaidia Rais Magufuli, kwa lengo la kumsaidia yeye na chama chetu. Sote tulilenga chama kutwaa madaraka na kuwahudumia watanzania. Tuliamini chama chetu ndo kina sera nzuri na kimebobea kwenye utawala na uongozi. Hivyo tulijitoa kwa moyo wote si kwa lengo la baadaye kupata vyeo, bali kwa roho ya uzalendo. Hivyo kulalamika kwa vijana hawa, kunaonyesha wazi kwamba walifanya kazi ya uchaguzi mkuu si kwa roho ya uzalendo, bali kwa kulenga kupata vyeo. Vijana hawa hawatufai kabisa.
Tumwache Rais, afanye kazi zake. Tusianze kuleta uchonganishi na maneno ya kumtenga na jamii. Yeye ni mchapa kazi, hapendi watu wavivu. Tumeshuhudia kilichotokea kwa rafiki yake wa karibu Bwana Kitwanga. Hakuangalia urafiki, bali alimwajibisha mara moja. Kama Happy,ni mtoto wake ni wazi atakuwa anamfahamu vizuri kwa tabia. Tunavyomfahamu Rais Magufuli, hawezi kuteuwa mzembe kwenye nafasi hiyo. Kama amemteuwa, ni wazi huyu atakuwa mzalendo na mchapa kazi. Akifanya kinyume, ni wazi tutamshuhudia Rais, akitumbua jipu la mtoto wake mwenyewe. Hivyo tumpe nafasi Happy Senenda Willium, tuone mchango wake katika taifa letu
Kwa hisani ya
Kilian Myenzi
0714028734(Kada mtiifu wa CCM-Iringa)