Kuwa msema kweli kwa wanawake

Kuwa msema kweli kwa wanawake

fenisher

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
339
Reaction score
726
Habari wakuu,

Hiki ni kisa kilichomtokea rafiki yangu na nilijifunza mengi kutokana na kisa chake cha mahusiano na naona ni vyema tuka share wengine pia wajifunze.

Ilikua ni siku yenye kunyesha mvua na David alikua anatoka kwa bibi yake na wakati huo alikua anarudi nyumbani kwao, baada ya kushuka kwenye daladala alianza kukimbia kutafuta sehemu ya kujihifadhi na mvua na kwa bahati mbaya akagongana na mdada aliyekua ameshika mwamvuli kwa kua alikua akitazama chini, anamuomba msamaha yule dada huku akijifuta maji yaliyokua yakichirizika usoni mwake lakini moyo ukaanza kudunda kwa haraka alipomuangalia huyo mwanamke aliyegongana nae, "alijibu yule dada" usijali ila uwe unaangalia mbele unapokimbia.

David aliendelea kumshangaa yule dada mpaka yule mwanamke alipoanza kuondoka na kuelekea kupanda daladala, David anamuangalia hadi yule mwanamke anapanda daladala hadi gari inaondoka na hapo anasikitika na kuanza kuondoka lakin safar alikua akitembea taratibu na ghafla akisikia akiitwa kwa sauti "wewe kijana umedondosha simu yako hii" anapokea simu ndogo ya nokia kutoka kwa mzee wa makamo akiambiwa aingalie kama haijaingia maji. Hadi anapokea simu anafahamu si simu yake lakini anaipokea na kuweka mfukoni na kuelekea nyumbani.

Njiani simu ilianza kuita na akafahamu hiyo si simu yake ni ile simu nyingine na anapokea kwakua simu haikua na nywila yoyote na kuanza kusikiliza masikioni, " Samahani nakuomba unisikilize kwa dakika chache" ilisikika sauti ya kike, David alijibu sawa dada angu nakusikiliza "

Naomba unirudishie hiyo simu kaka yangu kuna namba muhimu au hata laini peke nikiipata kwa kua kuna jambo muhimu na mtu nitahitaji kuwasiliana nae kupitia namba hii.." simu inakata na David anapoingalia anaona simu imezima na anapojaribu kuiwasha inaonyesha haina chaji na kujizima tena, anairudisha mfukoni na kuelekea nyumbani na anafika nyumbani na kubadilisha nguo na kukaa kitandani na kuanza kuitazama simu ile ambayo si yake na anatoa laini na...
 
INAENDELEA

Na... Kuiweka katika simu yake kwa kua simu yake ilikua na uwezo wa laini mbili na anakwenda kwa jirani na kuazima chaji na kuiweka chaji ile simu, anatoka nje na kukaa barazani kwao akiwaza na mara simu yake inaingia meseji na anapoangalia ni upande wa laini ya ile laini ambayo si yake " Tafadhali naomba unitumie namba yenye jina la MUHIMU, nakuomba kaka yangu unitumie ni namba muhimu" akiwa bado anaitazama meseji simu ikawa inaita kupitia laini ile ile namba iliotuma meseji na anapokea na sauti ya kike ilisikikka " Nitakupatia kiasi cha shilingi 50,000 kam utaniletea hiyo simu na laini ake kwa mda huu na nitalipia gharama za usafiri hadi nilipo" David anamjibu "sawa dada yangu nitakuletea pasipo kuhitaji malipo ila kwa sasa kuna mvua kubwa na simu imezima chaji na hii laini nimeweka katika simu yangu"... Unaweza kuchukua hata tax au bajaji na unifuate nilipia gharama zote ila naomba uje kwa muda huu " alisema yule dada" ....David anamjibu sawa nitafanya hivo na anapewa maelekezo ya mahala pa kwenda na anakwenda kuitoa simu chaji na kuirudisha ile laini kwenye simu yake na kuiwasha na wakati mvua ilikua inaanza kupungua na anafikiria usafiri wa kufika huko na anaona ni bora atumie usafiri wa pikipiki na anaamua kumpigia rafiki ake ambaye ni dereva wa bodaboda na mojamoja wanaanza safari na kufika huko lakini hakumwambia rafiki kama anapeleka simu aliyoiokota na wanafika hadi katika duka la nguo za wanawake na anashuka na kuingia hadi ndani ya duka na anakutana na dada na mvulana wakiwa wanapigana mabusu kwa kutumia ndimi zao na David anaguna na kuwastua watu wale na wanastuka na kuacha walichokua wakifanya na anapata nafasi ya kuona tena sura ambayo aliyokua ameiona kwenye kituo cha mabasi na akakumbana nae na kitendo cha kuwaona wakiwa katika hali ile na yule mwanaume kilimfanya uso wake uonekane wenye kukosa amani na anaingia mfukoni na kumkabidhi simu yule dada na kumwambia huo mzigo wako na naomba unipatie ulichoniahidi huku sura yake ikionyesha mwenye kua na hasira usoni, Yule dada anapokea na kuuliza gharama za usafiri ya pikipiki na David anamwambia ni shilingi 10,000 na yule dada anaingia kweny droo na kumkabidhi David kiasi cha 60,000 na kumshukuru sana kwa uaminifu wake na kumwambia hata hiko kiasi cha pesa alichompatia anahisi hakitoshi na anampa mkono na kumwambia asante sana kaka yangu wewe ni kama mdogo angu na nashukur kwa ukarimu wako na David anapokea pesa na kuaga na anafungua mlango na kumfuata rafiki ake na kupanda pikipiki na kuondoka......itaendelea
 
Back
Top Bottom