Kuwa makini na wanaume walaghai wa midomo

Kuwa makini na wanaume walaghai wa midomo

KWA SASA TUNAWAZA KUIONDOA CCM TU, HAYO MAMBO MENGINE BAADAYE


TUFIKIRI PAMOJA, TUSEME PAMOJA NA TUTENDE PAMOJA


SEMA:-
NIMECHOKA KUUAWA, NIMECHOKA KUIBIWA, NIMECHOKA KUTESWA NA KUNYANYASWA NDANI YA
NCHI YANGU, NIMECHOKA KUITWA MPINZANI NIMECHOKA KUDHARAULIWA.

SITAKI TENA UTUMWA NDANI YA NCHI YANGU, SASA NI MIMI NA TANZANIA HAPANA CCM OCTOBA 2015.

msema yote


 
Some people they can not cry until they see a coffin. (In Naija voicoo)
 
kumbe hamjitambui eeh, is it because kuwa mwalimu wenu ni kipofu? BTW... how are you, long time my dada
I'm doing ok brod, sijui wewe. Sio kwamba hatujitambui sema kuna time tunakuwa blinded na mapenzi hadi tunajisahau nini tunataka. Ila ndo tushaanza mapinduzi Kama hivi teh
 
hata waganga wakienyeji wana dawa za mapenzi lakini wanateswa na mapenzi
 
mwadila mabestito

natumai mko fiti na mnaendelea na majukumu yenu ya kujenga taifa na familia kiujumla.

Leo mwalimu wenu nimekuja na somo jipya ambalo nimeona niwape umakini jinsi ya kuishi vyema na wenzi wenu na kuwa makini nao kwani wengi wao ni vishosho vya midomoni lakini vitendo hawana.

Kwanini leo bestito wenu nimeamua kutoa fundisho hili la jinsi ya kuwatambua na kuwabaini wenzi wenu vishosho (yani waongo wa midomo) na matapeli wa kutunga maneno yakawa mvinyo kama rehani yabisi.

Shostito hata maandiko yanasema kuwa ni vyema ukaishi nao kwa akili na kuwabaini kwani wengi wao ni vishoka tena vile vilivyokubuhi ni afadhali ukawa na wembe ukakakukata kidizzaini kuliko kishoka ambacho ni kikali hata mpini wake hivyohivyo.

Je, utambuaje kuwa huyu ni kishoka wa kuweka lugha laini mdomoni na kuweza kuivuta kila samaki baharini na mwenye kuweza kukulainisha mpaka ukawa gorini mwenyewe bila kupenda
.

Shostito inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, hiyo ni sumu na unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema isije kuwa upo kwenye foleni!

hakuna kitu kibaya kama kuwa katika foleni ya wapenzi kwa mpenzi mmoja, tena mbaya zaidi awe ni yule ambaye moyo wako umempenda kwa dhati.


kumbuka, kuwa katika uhusiano na mtu ambaye haeleweki ni sawa na kukaribisha matatizo katika maisha yako, huna sababu ya kuishi kwa wasiwasi ukiwa hujui mpenzi wako anakuchukulia vipi.

anza kumuwekea mitego mapema. Lakini katika mitego yako achana na simu yake kabisa, huna sababu ya kuchunguza simu yake lakini kama ni msaliti utajua tu, unafikiri atajificha mpaka lini? atafanya mambo yake gizani mpaka lini?

Kuna siku utagundua na kumuacha aendelee na umalaya wake kama ameona ndiyo maisha. Usikubali kabisa kuwa katika penzi la kitumwa, penzi la kisaliti, kuwa na mtu ambaye anakuchanganya wa kazi gani zaidi ya kukupotezea muda na kukukaribishia machozi bestito achana naye hukuumbwa kwa ajili ya mmoja? Cha kufanya wewe muache aendelee mbele na we songa mbele na mambo yako.

utamjuaje mpenzi laghai wa mdomo?
hapa ndipo kwenye kazi, kwa bahati mbaya sana kama ikitokea ukampenda mtu sana hata kama akifanya mabaya kiasi gani unaweza usiyaone, kama wewe ni wa aina hii unapaswa kubadilika kifikra. Mwone wa kawaida, fanya uchunguzi wako polepole na kama ukiona moja kati ya mambo yafuatayo, ujue kuna kitu.
a) hataki kukutambulisha kwa marafiki zake:

hii ni kati ya alama walizonazo matapeli wa mapenzi, ni mtu wa kufanya mambo kwa upekee sana. Kila dakika hakaukiwi na neno nakupenda sana, lakini moyoni mwake hakuna alama hata moja ya mapenzi kwako.


ni vigumu kumtambua mtu wa aina hii lakini chunguza kuhusu hili, hapendi kabisa kukukutanisha na rafiki zake na hata mkikutana nao kwa bahati mbaya basi hatakutambulisha na kama akikutambulisha hatakutambulisha kama mpenzi wake rasmi. Ataishia kusema ninyi ni marafiki mlioshibana!

tangu lini mpenzi akatambulishwa kama rafiki? Mtu anapomtambulisha mpenzi wake humtambulisha kwa kujisikia furaha moyoni kwamba anamtambulisha mpenzi wake lakini inakuwaje kwako akutambulishe kama rafiki?

b) msiri kupitiliza:

hii ni alama nyingine waliyonayo wanaume wa aina ninayoielezea katika mada hii. Siku zote mambo yake ni kwa siri kubwa, kama mna ahadi ya kukutana, hataki muongozane, atakuambia mkutane moja kwa moja sehemu husika. Hata muda wa kuondoka atafanya kila njia ili kila mmoja aondoke mwenyewe na kama mkiondoka pamoja basi ujue ni usiku na hakuna atakayewaona.

ikitokea akakubali kuongozana na wewe, hatapenda muongozane pamoja. Atalazimisha utangulie mbele yeye afuate nyuma, kwa nini? Kwa sababu anaogopa kujulikana kuwa yeye ni mpenzi wako na kama anaogopa anakupenda kweli? Mapenzi gani hayo yanafanywa kwa siri? Anakupotezea muda huyo.

(c) hapendi ndugu wafahamiane

mpenzi wa aina hii ni mjanja sana, kwanza kabisa atajifanya mtu mwenye ‘ubize’ sana, yote hii ni kukwepa kuwajua ndugu zako au wewe kuwajua ndugu zake! Wakati mwingine anakuwa hapendi ndugu zako na wake wakutane wakijua wazi kuwa nyie mna uhusiano, hili ni tatizo.

Bestito na shostito nawasihi kuweni makini na wanaume wa aina hii wengi wao ni matapeli wa mdomoni hawana chochote nia yao kubwa ni kukulaghai na kukuondolea uthamani wa mwili wako uliumbwa kwa ajili ya utukufu wa mungu na sio kujirahisi kwao .

Achaneni kama mkiona wako wa dizaini hiyo mimi mama yenu nawasihi sana kwani bila wao msinaendesha tu kwa kwenda mbele kwani jitu likuumize moyo wakati unao uwezo wa kila kitu yaani mtu akufyotoe nawe ulieulie tu eti kisa nini shostito jitunze.

Jiheshimu na jichunge ipo siku mungu atakupa wa ubavu wako kam mie shostito wenu wa ukweli.

Hili ni somo jema kwenu msijirahisi kiasi hicho kwa watu walio na shosho mbovu,jipangeni na jiwekeni thabiti kwani mnazo nguvu na uwezo wa kujihudumia.

Ciao mabestito

wasalaam

ladyf

cc: mtambuzi, mamndenyi, charminglady, lady doctor, passion lady, mwallu, amu, firstlady1, preta, mshanajr, kakakiiza, asprin, miss chagga, heaven on earth, heaven sent, charity, sister, rich pol, valentine na marafiki zangu wengine kibao karibuni mlete maoni na dau zenu hapa mabestito


wanawake bwana mmeumbwa kipekee uzoefu unaonesha mtu akishatendwa ikisha mara kwa mara ndio anakua mwalimu huna ualimu wowote usipende kukurupuka katika mapenzi utalia kila siku pole we
 
Wanawake wanaokurupuka ndio huwa inakula kwao ndilo lililokutokea wewe mtoa post hadi umekua mwalimu mzuri hongera teacher
 
-Siwezi kumtambulisha mtu ambaye hata sifikirii kesho nitakuwa nae
-Siwezi kuwa muwazi kwa mtu ambaye sina future naye
-Siwezi kumpeleka mwanamke ghetto kwangu kama hakidhi vigezo vyangu, atabaki kuwa wa lodge/guest tu

Wanawake mnatakiwa muwe waangalifu sana.

sasa kama hauna future nae si mwambie tu right from the start kuliko unakuwa nae afu badae unamlostisha kwa

kumwambia hana vigezo dah yani , ume m utilize weee huko guest sijui lodge afu unamtosa kama huna future nae kuliko kumfanyia hayo bora mwambie tu kiungwana.
 
Hivyo vigezo ni dynamics.... in a matter of speaking Kuna wanaume wanatabia hizo Na hawana hata mchepuko mmoja Na maisha yako Saaaafi na wenzi wao... kutambulisha tambulisha ni ushamba flan hiv wakat mwingine... ...MPENZI NI YA WAWIL ...mengine yooote yanayoitwa sijui sifa za mpenzi.. sijui utajuaje mpenzio anakupnda... sijui ivi sijui Dalili za kuchokwa sijui nn.....zooote ni utopian .... sio kila ukipatwa homa ni Dalili za malaria...
 
sasa kama hauna future nae si mwambie tu right from the start kuliko unakuwa nae afu badae unamlostisha kwa

kumwambia hana vigezo dah yani , ume m utilize weee huko guest sijui lodge afu unamtosa kama huna future nae kuliko kumfanyia hayo bora mwambie tu kiungwana.
Hapa najaribu kuwaonyesha wanawake wajue jinsi ya kunasua mitego ya kutumika bila shukrani..
 
hhahhahh uzuri wa hili gem halijawahi pata shujaa / mshindi hata alama uzisome vipi anything can happen at anytime chezea penats wewe - love si mchezo wa kawaida - ni kuomba mungu tu :sleepy:
 
Duuh Nipe Macho ya Roho nione kama uonavyo wewe Baba.... Asante Mama kwa message ... Thanks ..
 
kujinasua ni kuepuka kwenda guest na lodge tu, manake huko ni uasherati tu, yani you men ?


Imagine mdada tangu amfahamu bf wake, hajui hata anaishi wapi, anaishi na nani! Huenda huyo bf ana mke wake walioana miaka mitano ilopita. Sasa unajiuliza, inakuwaje mdada anakubali kwenda lodge tu, hataki kufahamu bf wake anaishi wapi?
Mtu hata hajui ndugu yoyote, je akipata matatizo wakati mpo pamoja utamwambia nani, unakuta mwaka unapita hata ndugu mmoja humfahamu..wewe hushtuki tu?
Muwe mnaangalia, sio kwa vile unapewa visenti na kuridhishwa kinako basi unajisahau.
 
Imagine mdada tangu amfahamu bf wake, hajui hata anaishi wapi, anaishi na nani! Huenda huyo bf ana mke wake walioana miaka mitano ilopita. Sasa unajiuliza, inakuwaje mdada anakubali kwenda lodge tu, hataki kufahamu bf wake anaishi wapi?
Mtu hata hajui ndugu yoyote, je akipata matatizo wakati mpo pamoja utamwambia nani, unakuta mwaka unapita hata ndugu mmoja humfahamu..wewe hushtuki tu?
Muwe mnaangalia, sio kwa vile unapewa visenti na kuridhishwa kinako basi unajisahau.


mmh yani
 
nashukuru hata kwa wewe best uliyesoma hapa naomba uwe chachu kwa wenigine wajitambue na wajinasua toka kwenye meno ya hao mababazazi
Duuh Nipe Macho ya Roho nione kama uonavyo wewe Baba.... Asante Mama kwa message ... Thanks ..
 
hahahahahhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa yaani umenifurahishha besti
na umenifanya niongeze siku ya leo asante kwa ujumbe huu murua umewafikia walengwa thanks bestito
Imagine mdada tangu amfahamu bf wake, hajui hata anaishi wapi, anaishi na nani! Huenda huyo bf ana mke wake walioana miaka mitano ilopita. Sasa unajiuliza, inakuwaje mdada anakubali kwenda lodge tu, hataki kufahamu bf wake anaishi wapi?
Mtu hata hajui ndugu yoyote, je akipata matatizo wakati mpo pamoja utamwambia nani, unakuta mwaka unapita hata ndugu mmoja humfahamu..wewe hushtuki tu?
Muwe mnaangalia, sio kwa vile unapewa visenti na kuridhishwa kinako basi unajisahau.
 
Back
Top Bottom