Kuwa makini na wanaume walaghai wa midomo

Kuwa makini na wanaume walaghai wa midomo

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Mwadila mabestito

Natumai mko fiti na mnaendelea na majukumu yenu ya kujenga taifa na familia kiujumla.

Leo mwalimu wenu nimekuja na somo jipya ambalo nimeona niwape umakini jinsi ya kuishi vyema na wenzi wenu na kuwa makini nao kwani wengi wao ni vishosho vya midomoni lakini vitendo hawana.

Kwanini leo bestito wenu nimeamua kutoa fundisho hili la jinsi ya kuwatambua na kuwabaini wenzi wenu vishosho (yani waongo wa midomo) na matapeli wa kutunga maneno yakawa mvinyo kama rehani yabisi.

Shostito hata maandiko yanasema kuwa ni vyema ukaishi nao kwa akili na kuwabaini kwani wengi wao ni vishoka tena vile vilivyokubuhi ni afadhali ukawa na wembe ukakakukata kidizzaini kuliko kishoka ambacho ni kikali hata mpini wake hivyohivyo.

Je, utambuaje kuwa huyu ni kishoka wa kuweka lugha laini mdomoni na kuweza kuivuta kila samaki baharini na mwenye kuweza kukulainisha mpaka ukawa gorini mwenyewe bila kupenda
.

Shostito inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, hiyo ni sumu na unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema isije kuwa upo kwenye foleni!

Hakuna kitu kibaya kama kuwa katika foleni ya wapenzi kwa mpenzi mmoja, tena mbaya zaidi awe ni yule ambaye moyo wako umempenda kwa dhati.

Kumbuka, kuwa katika uhusiano na mtu ambaye haeleweki ni sawa na kukaribisha matatizo katika maisha yako, huna sababu ya kuishi kwa wasiwasi ukiwa hujui mpenzi wako anakuchukulia vipi.

Anza kumuwekea mitego mapema. Lakini katika mitego yako achana na simu yake kabisa, huna sababu ya kuchunguza simu yake lakini kama ni msaliti utajua tu, unafikiri atajificha mpaka lini? Atafanya mambo yake gizani mpaka lini?

Kuna siku utagundua na kumuacha aendelee na umalaya wake kama ameona ndiyo maisha. Usikubali kabisa kuwa katika penzi la kitumwa, penzi la kisaliti, kuwa na mtu ambaye anakuchanganya wa kazi gani zaidi ya kukupotezea muda na kukukaribishia machozi Bestito achana naye hukuumbwa kwa ajili ya mmoja? Cha kufanya wewe muache aendelee mbele na we songa mbele na mambo yako.

UTAMJUAJE MPENZI LAGHAI WA MDOMO?
Hapa ndipo kwenye kazi, kwa bahati mbaya sana kama ikitokea ukampenda mtu sana hata kama akifanya mabaya kiasi gani unaweza usiyaone, kama wewe ni wa aina hii unapaswa kubadilika kifikra. Mwone wa kawaida, fanya uchunguzi wako polepole na kama ukiona moja kati ya mambo yafuatayo, ujue kuna kitu.
A) Hataki kukutambulisha kwa marafiki zake:

Hii ni kati ya alama walizonazo matapeli wa mapenzi, ni mtu wa kufanya mambo kwa upekee sana. Kila dakika hakaukiwi na neno nakupenda sana, lakini moyoni mwake hakuna alama hata moja ya mapenzi kwako.

Ni vigumu kumtambua mtu wa aina hii lakini chunguza kuhusu hili, hapendi kabisa kukukutanisha na rafiki zake na hata mkikutana nao kwa bahati mbaya basi hatakutambulisha na kama akikutambulisha hatakutambulisha kama mpenzi wake rasmi. Ataishia kusema ninyi ni marafiki mlioshibana!

Tangu lini mpenzi akatambulishwa kama rafiki? Mtu anapomtambulisha mpenzi wake humtambulisha kwa kujisikia furaha moyoni kwamba anamtambulisha mpenzi wake lakini inakuwaje kwako akutambulishe kama rafiki?

B) Msiri kupitiliza:

Hii ni alama nyingine waliyonayo wanaume wa aina ninayoielezea katika mada hii. Siku zote mambo yake ni kwa siri kubwa, kama mna ahadi ya kukutana, hataki muongozane, atakuambia mkutane moja kwa moja sehemu husika. Hata muda wa kuondoka atafanya kila njia ili kila mmoja aondoke mwenyewe na kama mkiondoka pamoja basi ujue ni usiku na hakuna atakayewaona.

Ikitokea akakubali kuongozana na wewe, hatapenda muongozane pamoja. Atalazimisha utangulie mbele yeye afuate nyuma, kwa nini? Kwa sababu anaogopa kujulikana kuwa yeye ni mpenzi wako na kama anaogopa anakupenda kweli? Mapenzi gani hayo yanafanywa kwa siri? Anakupotezea muda huyo.

(c) Hapendi ndugu wafahamiane

Mpenzi wa aina hii ni mjanja sana, kwanza kabisa atajifanya mtu mwenye ‘ubize' sana, yote hii ni kukwepa kuwajua ndugu zako au wewe kuwajua ndugu zake! Wakati mwingine anakuwa hapendi ndugu zako na wake wakutane wakijua wazi kuwa nyie mna uhusiano, hili ni tatizo.

Bestito na shostito nawasihi kuweni makini na wanaume wa aina hii wengi wao ni matapeli wa mdomoni hawana chochote nia yao kubwa ni kukulaghai na kukuondolea uthamani wa mwili wako uliumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na sio kujirahisi kwao .

Achaneni kama mkiona wako wa dizaini hiyo mimi mama yenu nawasihi sana kwani bila wao msinaendesha tu kwa kwenda mbele kwani jitu likuumize moyo wakati unao uwezo wa kila kitu yaani mtu akufyotoe nawe ulieulie tu eti kisa nini shostito jitunze.

Jiheshimu na jichunge ipo siku Mungu atakupa wa ubavu wako kam mie shostito wenu wa ukweli.

Hili ni somo jema kwenu msijirahisi kiasi hicho kwa watu walio na shosho mbovu,Jipangeni na jiwekeni thabiti kwani mnazo nguvu na uwezo wa kujihudumia.

Ciao mabestito

Wasalaam

Ladyf

cc: Mtambuzi, Mamndenyi, charminglady, Lady doctor, Passion Lady, mwallu, amu, FirstLady1, Preta, mshanajr, KakaKiiza, Asprin, miss chagga, Heaven on Earth, Heaven Sent, Charity, sister, Rich Pol, valentine na marafiki zangu wengine kibao karibuni mlete maoni na dau zenu hapa mabestito

Kwahyo unataka vdumbukie kwenye shimo la taka huku tunajua halifai? Msing mzur ni kuangalia atae kufaa maishan ili usyumbe ovyo. SELECTION must.
Poleni sana mabint kwa kuumizwa mala kwa mala tatizo mnachagua sana.
 
-Siwezi kumtambulisha mtu ambaye hata sifikirii kesho nitakuwa nae
-Siwezi kuwa muwazi kwa mtu ambaye sina future naye
-Siwezi kumpeleka mwanamke ghetto kwangu kama hakidhi vigezo vyangu, atabaki kuwa wa lodge/guest tu

Wanawake mnatakiwa muwe waangalifu sana.
 
Wanaume laghai ni kuwa laghai zaidi yao.

Hakuna mwanaume mzuri au mbaya inategemea umemformat vipi! Anae kukula wewe bure kwa wenzio anatanguliza wallet. Unaemuabudu wewe kwa wengine lafa tu anasujudu kama kawaida. Mi kuna mtu bahili ofisini kashindikana lakini mi kaniwekea bili. Namfuga kama paka, nikiita nyauuu huyu hapa. Watu umemtengenezaa, umemtengeneza kwa hela gani aliyo nayo mpaka ni outsource idara ya miundo mbinu. Siasa tu, nampiga, nisham convice mimi zaidi yake, ili afike level zangu ajikaze mpaka ushuzi umtoke. Hahahaaaaa! MAPENZI SIASA.

It all counts down to wewe unajiwekaje kwake. Ukijiweka level ya dekio atakufanya dekio haswaa, ukijiweka level ya utumbo atakufungia ndani mpaka, ukijiweka level za juu ataku treat hivo hivo.

KAULI MBIU YA LEO MAPENZI SIASA!
 
Poleni sana bhana! ila ndo hivyo tena kama wahenga walivyonena,mchagua nazi mwisho huambulia koroma.lkn c kwenu tu kwan hata upande wa pili tunakutana nayo hayo magumu.
 
ni kweli mwana umeongea hapa haya yote ni pande zote mbili za shilingi hutokeaga
Poleni sana bhana! ila ndo hivyo tena kama wahenga walivyonena,mchagua nazi mwisho huambulia koroma.lkn c kwenu tu kwan hata upande wa pili tunakutana nayo hayo magumu.
 
kweli mapenzi ni SIASA best nimeamini

ila hawa wanaume ni mashombi sana besti ni kuachana nao tu kwani wanazo si lolote si chochote kabisa
Wanaume laghai ni kuwa laghai zaidi yao.

Hakuna mwanaume mzuri au mbaya inategemea umemformat vipi! Anae kukula wewe bure kwa wenzio anatanguliza wallet. Unaemuabudu wewe kwa wengine lafa tu anasujudu kama kawaida. Mi kuna mtu bahili ofisini kashindikana lakini mi kaniwekea bili. Namfuga kama paka, nikiita nyauuu huyu hapa. Watu umemtengenezaa, umemtengeneza kwa hela gani aliyo nayo mpaka ni outsource idara ya miundo mbinu. Siasa tu, nampiga, nisham convice mimi zaidi yake, ili afike level zangu ajikaze mpaka ushuzi umtoke. Hahahaaaaa! MAPENZI SIASA.

It all counts down to wewe unajiwekaje kwake. Ukijiweka level ya dekio atakufanya dekio haswaa, ukijiweka level ya utumbo atakufungia ndani mpaka, ukijiweka level za juu ataku treat hivo hivo.

KAULI MBIU YA LEO MAPENZI SIASA!
 
Na wote tuseme Amen. Cha muhimu tujue tu kusoma Alama za nyakati na majira ya nukta, jua unapopendwa na unapochezewa then fanya maamuzi magumu. Ila wakati mwingine Sijui huwa tunakumbwa na nini. Yani Unaona Kabisa Kuwa hapa sitakiwi au hamna Mwisho mzuri lakini unafumba tu macho. Mungu na atusaidie tuweze kujitambua
 
True that
 
kumbe hamjitambui eeh, is it because kuwa mwalimu wenu ni kipofu? BTW... how are you, long time my dada
 
kweli mapenzi ni SIASA best nimeamini

ila hawa wanaume ni mashombi sana besti ni kuachana nao tu kwani wanazo si lolote si chochote kabisa

na SIASA ni rough game. A likely winner can be a loser at any moment. So play your cards carefully and be risk-conscious!

''Kazi ya moyo ni kusukuma damu, KUPENDA ni kiherehere chako tu'' by Matola
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom