kiliochangu
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 1,152
- 886
Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwajulisha kuwa kumezuka tabia ya watu kuiba namba za simu za watu wengine na kuanza kuzitumia kutuma taarifa za uongo. Hii imenitokea jana jioni. Bahati nzuri niligundua baada ya muda wa robo saa wakati mwenzangu aliponiuliza mbona namba yako ya whatsap umetuma taarifa kwa lugha ya Kiswahili na picha za magari hatuelewi? Nilimjibu kuwa labda imetokea kimakosa. Kurudi gafla kuangalia whatsap yangu nifungue haikufunguka tena bali nilitakiwa ni verify number yangu. Kwa kuwa sipo Tanzania sikuweza ikabidi nisajili whatsap kwa namba nyingine na kuanza kutuma taarifa kwa watu wote niliokuwa nawasiliana nao kwa kutumia whatsap.
Jambo nisiloelewa wamewezaje kufanya hivyo wakati simu hawajaiba ninayo hapa na card number ya simu ninayo hapa. Unaposajili namba ya whatsap huwa inakupa sms na unasoma kwenye simu yako kuverify, bado nafuatilia kujua how they have managed to do so
kwa muda mfupi kwa kuwa walijifanya kuna mtu wanamfahamu anauza gari Mil 6 kwa kuwa ana shida, walishafanikiwa kuwa attract watu maana watu walifikiri ni kweli taarifa nimewatumia mimi. Bahati nzuri wepesi wakutuma taarifa kwa kuwa WIFi ni free nilipo nilituma kila mahali na group zote wakaji disconnect na hao watu. Kuna mtu mmoja aliwasiliana nao mpaka kumwambia aende Goba akaangalie hilo gari. Hivyo hilo suala na muhisika yupo Tanzania.
Nawapa taarifa hii muwe makini nakufanya mawasiliano ya biashara yoyote kupitia Whatsap au msg. Ukiona unahitaji kitu piga simu kwa muhusika kujiridhisha kama ndiye kweli au la.