Kuwa makini na utapeli huu wa mtandao

Kuwa makini na utapeli huu wa mtandao

Tzhacker 000

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
659
Reaction score
690
b4f275d868e8cfdb1a83e72648991b5b.jpg

Utapeli ni tatizo kubwa sana kwa kila mtu,hasa mtumiaji wa mtandao, huenda wewe ushawahi kukutana na aina fulani ya utapeli.
Kuna aina nyingi sana za utapeli wa kimtandao, leo tutaona baadhi tu na shuhuda mojawapo.

1. KUPIGIWA SIMU NA WATOA HUDUMA WAONGO

Hii imetokea watu wengi sana,unapigiwa simu na mtu anaejitambulisha kuwa anatoka kwenye kampuni za simu kama Tigo, Vodacom au Airtel unaambiwa kuna bonasi umepewa,lakini unatakiwa kutaja jina lako kamili, umri na kiasi cha pesa ulichonacho, basi hapo mtaongea kwa kirefu lakini utaambiwa kabla hujatumiwa pesa tuma kiasi fulani kwanza kwenye namba atakayokupa, lakini pale utakapotuma basi na ndio mwisho wa mawasiliano na hutompata tena.

2.KUPATA RAFIKI MTANDAONI

Wale wapenzi wa Facebook ndio wahanga wengi katika hili,kama ni binti au kijana atakuja rafiki wa jinsia tofauti na wewe.
Cha kwanza kabisa atakuamisha toka Facebook na kutaka muwasiliane kwa barua pepe,huko atakupa historia yake na utajiri aliokua nao baba yake,akijifanya kuwa ni mkimbizi na hana wazazi,anaishi ukimbizini lakini ana akiba ya pesa alizowekewa na baba yake toka mdogo.
Na hapo akukutajia kiasi kikubwa sana,ila anataka ombi moja tu kwako,atoke kambini aje uraiani na kama utafanikisha mtakuja kuwa pamoja au kama umeowa/kuolewa atakulipa kiasi fulani cha pesa,mtatua muda sana kuwasiliana mpaka kuja kuhitaji pesa yako.
ili aendeshe kesi za mirathi na malipo kwa mawakili, kama utakuwa na tamaa ya uhitaji wa hizo pesa mwisho wa siku utapigwa wewe.

3.KUJISHINDIA ZAWADI FULANI TOKA NJE YA NCHI.
Huu ni wizi mpya ambao ndio unaotumika sana, cha kushangaza unaweza kuambiwa umeshinda pesa nyingi sana wakati hajawahi cheza mchezo wowote mtandaoni. Ila sharti lao tuma majina yako kamili,namba yako ya simu, mwaka uliozaliwa kwa kutumia barua pepe. Hapo ukituma hayo maelezo nirahisi mtu kukujua kiundani na unampa njia rahisi ya kukufanyia utapeli.

Habari Leo
 
Aise mimi kuna demu mmoja alinitengeneza vizuri nami nikampa ushirikiano kama miezi 2 hivi akinitumia picha kibao hadi za ndugu zake na familia. Yake na anapoishi ila alikuja kuharibu sehemu ndogo sanaa baada ya kuplan safari ya kujaa huku Tanzania alivyofika Moscow akishiwa nauli hivyo akawa anahitaji dolla900 ili kufika hapa aise Ila mwisho nikamsukia baada ya kumwambia asijali naweza mlipia nauli kwa agent wa huku huku Tanzania akapotea ghafla .alivyorudi tusi langu lilikuwa moja tu fucky you.
 
Tuache kupenda vya bure jamani. Wezi wa mtandao moja ya silaha yao kubwa ni tamaa ya pesa za bure ya victims wao
 
Niliponea chupu chupu na kutapeliwa na binti wa Kikenya, kama kuna mtu alishawahi kutumiwa ile email kuwa ameshinda dola 850 toka kwenye lile shindano la Coca cola womes world cup Canada 2018, moja ya Muhusika ni huyu binti wa Kikenya hapa chini.

Hii ni email niliyomtumia baada ya kuwauliza Coca cola na kunijibu hakuna shindano lolote liloendeshwa
c7e30a18bec6929ca0177be1effb053f.jpg

Kikubwa zaidi ni kuwa sikuwahi kushiriki shindano lolote.
IMG_0801.JPG
 
Niliponea chupu chupu na kutapeliwa na binti wa Kikenya, kama kuna mtu alishawahi kutumiwa ile email kuwa ameshinda dola 850 toka kwenye lile shindano la Coca cola womes world cup Canada 2018, moja ya Muhusika ni huyu binti wa Kikenya hapa chini.

Hii ni email niliyomtumia baada ya kuwauliza Coca cola na kunijibu hakuna shindano lolote liloendeshwa
c7e30a18bec6929ca0177be1effb053f.jpg

Kikubwa zaidi ni kuwa sikuwahi kushiriki shindano lolote.
View attachment 665700
Binti wa Kikenya wa mwaka 1992 alitaka kunitapeli Usd 200 = 380,000Tsh mimi niliekula miaka mama.eee zake, nyoko kabisa huyu, laiti kama angekuwa tz hii ninge.mtia wima
 
Hehehe yan wanahangaika sana, mm nilitumuwa msg ya kawaida nikapewa email.
 
Back
Top Bottom