John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 112
- 217
Kuwa Makini na Maneno Tunayotamka
Mfano wa Yakobo na matamko dhidi ya familia yake
Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu? Yakobo akajibu, akamwambia Labani, kwa sababu naliogopa, nikasema, Usije ukaninyang’anya binti zako kwa nguvu. Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi.
Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli, mke wake, ameiiba (Mwanzo 31:30-32). Yakobo alikuwa na wake wawili, Raheli na Lea, wote watoto wa mama mmoja.
Vinyago vya Labani vilikuwa vinawakilisha urithi wa mali zake, hivyo mtoto wake yeyote ambaye atafanikiwa kuwa navyo, atarithi mali zote za babaye kipindi baba atakapokufa.
Basi jamaa wa karibu watatafuta vinyago vile vipo kwa nani ili kumtambua mrithi na mwendelezaji wa mali za marehemu.
Kwa kulijua hilo, Raheli alikimbilia kuviiba vinyago hivyo ili baadaye anufaike na mali chache zilizosalia za baba yake, Labani. Kwa sababu Raheli na Lea walijua kwamba Yakobo amemfilisi baba yao mali yote, hivyo walijua hawatanufaika chochote kutoka kwa baba yao.
Pamoja na hayo, vinyago vilihusisha masuala ya imani, maana vinyago viliitwa “miungu”. Tafsiri ya neno miungu inatupa kuelewa kwamba kulikuwa na maana ya imani juu ya miungu. Bila shaka walitumia vinyago hivyo kama mungu wa ulinzi.
Labda Raheli alipoviiba vinyago hivyo alitamani aendelee kulindwa na miungu hiyo bila kujua kwamba kuamini miungu ni machukizo mbele za Bwana, kwa maana hakuna ulinzi toshelevu unaopatikana kutoka kwa miungu.
Maneno ya Yakobo ndiyo yalimuua Raheli mke wake na kipenzi chake
Yakobo alitamka kwamba yeyote atakayekutwa na vinyago hivyo, basi afe. Aliyasema hayo bila kujua kwamba, yeye ampendaye, mkewe Raheli ndiye aliyekuwa ameviiba. Laiti kama angelijua mke wake ndiye anavyo vijago hivyo ni dhahiri asingelisema hayo.
Yakobo aliamini kwamba mkewe asingeweza kuiba, kumbe mkewe,Raheli, ndiye mwizi. Wakiwa katika safari, neno lile la “aliyechukua afe” likatimia kwa mkewe Raheli, kwa maana alikufa akiwa njiani wakati alipojifungua mtoto Benyamini (Mwanzo 35:16-18).
Laiti Yakobo kabla ya kutamka “kifo” angelichukua muda kidogo wa kuwauliza au kuwabana wake na watoto wake, labda angeviona vinyago hivyo,au angelijua namna nzuri ya kuyatawala maneno yake. Maneno ya Yakobo yalikuwa na nguvu ya kusababisha uzima au mauti, kwa sababu yeye ni mtumishi wa Mungu. Maneno kama hayo yanaakisi maisha yetu.
Mara nyingi na sisi tumekuwa tukiwaua ndugu zetu kwa kutamka bila kujua kwa kuwa nasi ni watumishi wa Mungu pia. Kwa mfano, unaomba kila mchawi na mshirikina “kufa na afe”, maana mchawi ni mtu mbaya, Sasa kwa sababu unajua mama/baba yako hawezi kuwa mshirikina au mchawi. Lakini laiti ungelijua mama/baba yako naye ni wale wale washirikina tu, basi usingelitamka hayo. Sasa unatamka, tena unamaanisha, Kisha kesho unapigiwa simu unaambiwa mama/baba yako amekufa kijijini kwenu kwa ghafla.
Mfano wa Hamani na Matamko dhidi ya Wayahudi
Unafikiri hata Hamani, mwanamume mwenye kiburi, chini ya mfalme Ahasuero wa Uajemi (Iran ya leo), mtesi wa Wayahudi, alipotangaza kwamba Wayahudi wote waangamizwe (Esta 9:24), bila kujua kwamba Esta, mke wa mfalme, naye ni Myahudi, angelisema hayo maneno? Mfalme alipofahamishwa kuwa Hamani alitoa matangazo hayo, alitoa agizo kuwa, kutokana na Hamani kuamua vibaya juu ya Wayahudi, yeye Hamani na watoto wake watundikwe juu ya mti (Esta 9:25). Matunda ya matamko ya Hamani yalimrudia mwenyewe. Hamani alikuwa amekurupuka na chuki zake akatamka, lakini laiti angelijua anenayo, angelinyamaza au angelitafuta njia nyingine ya kushughulikia yale aliyotaka kuyafanya.
Methali 18:20-21 inasema: 20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. 21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi (mdomo); Na wao waupendao watakula matunda yake. Huo ni msisitizo kuwa mdomo ni lazima utumike kwa makini katika kutoa matamko mbalimbali.
Kuwa Makini na Maneno Unayotamka
Jifunze kuwa makini na maneno yako unayotamka kwa sababu unaweza ukaua au kusababisha hatari kubwa na kujuta sana hapo baadaye. Ni vyema ukafikiri kwanza kabla ya kunena uyatakayo kunena, hasa wakati ule unapochokozwa/una panic. Kama itakuwa shida kunena basi ni afadhali ukae kimya.
Kuna mifano mingi ambapo watu wanatamka maneno hasi. Kwa mfano, mtu anamwambia mtoto wake “wewe utakuwa mwizi”, “hutaoa”, tutaona kama utashinda mtihani”, duka lako haliwezi kupiga hatua”, “mtoto wangu siyo mwizi, akikutwa na vitu vya wizi, po pote pale alipo, akatwe mikono”, kumpa mtoto jina la “shida”. Na mifano mingine mingi aina hiyo.
Fahamu kuwa tamko ni nadhiri, ni kifungo, ni maombi ya kutaka jambo litokee, umeweka saini na mhuri kwa mdomo wako. Hivyo, kwa kutumia mfano mmoja kuhusu matamko ya Yakobo kwa familia yake, tujifunze na kuwa makini katika maneno tunayotamka.
Siyo lazima matamko yako yajibu hapo kwa hapo. Yanaweza kujibu miezi au hata miaka kadhaa baadaye. Ukishatamka, umetamka. Haijalishi hata kama ulikuwa na hasira.
Hivyo, tafakari kwa makini kabla ya kutamka maneno kusudiwa.