Kuwa makini, hii namba inatumika kwa utapeli

sir j

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
317
212
0746026829
Huyu mwenye namba hiyo kanipigia asubuhi ya leo, akidai yeye ni mtoa huduma kwa wateja- VODACOM

Akanambia kuwa nimejishindia kiasi cha Tshs 200,000/= kwenye kampeni ya nogesha upendo na vodacom na muda sio mrefu wangenitumia msg kuthibitisha muamala huo na akanambia baada tu ya msg hiyo kuingia niende vodashop nikaoneshe hiyo msg then nitajipatia simu kali ya smart aina ya tecno C8.

Lakini kimbembe kikaanzia hapa akaniuliza.nimefanya muamala wa mwisho lini....na nina salio kiasi gani kwenye akaunti yangu ya M-pesa mie nkamuuliz wewe umesema ni mtoa huduma kwa wateja Vodacom sasa inakuwaje usijue taarifa zangu akanijibu. ..'.ooohh tunataka kujiridhisha kama wewe ndiye mmliki wa simu hii nikamwambia mie nina mambo mengi sikumbuki na badala yake, yeye ndiye anikumbushe mara ya mwisho nimefanya muamala lini jamaa kuona hivyo akakata simu.

Ndipo nikawapigia Vodacom wakanambia hao watu ni matapeli ukiwasikiliza, mwishowe watakutumia msg yao ya m-pesa na kukutaka ufuate maelekezo yao mwisho wa siku wanakuibia pesa zako kwenye akaunti yako.

Kwa hiyo kuwa makini na simu za namna hiyo usije kutapeliwa kwa hivyo imenitokea leo nkaona niwashirikishe na ninyi.
 
Inaonekana hakuna ushirikiano kati ya vodacom, Police na TCRA, hawa watu hawajaanza huu mchezo leo tulitarajia wangekuwa wamekamatwa wakatangazwa hadharani na kufungwa wasahaulikie huko
 
Matapeli wapo wengi wengine wameweka matangazo ya kazi kwenye vituo vya daladala eti kazi airport ila utoe 50,000 kwanza.

Ngastuka
 
Inaonekana hakuna ushirikiano kati ya vodacom, Police na TCRA, hawa watu hawajaanza huu mchezo leo tulitarajia wangekuwa wamekamatwa wakatangazwa hadharani na kufungwa wasahaulikie huko

Ajabu ni kwamba, Vodacom wenyewe ndio wakaniambia kuwa, akiendelea kunisumbua nikaripoti kituo cha Polisi.
Je, wao hawahusiki kwa lolote walau kufanya mawasiliano na tcra...??? Kwani mtandao wao ndio unatumiwa na matapeli hawa.....ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya matapeli hawa....???????
 
Vodacom na huyo mtu ni waarabu wa pemba, biashara imekuwa mbaya wao wanajuana kwa vilemba vyao
 
polee aisee
9f7f897d084da8e0cb927749a832dab9.jpg
 
kumbe juzi juzi tu hapa pole sana kiongozi

Mwezi uliita tu halaf kibaya zaidi ukienda polisi wanakukatisha tamaa na ufuatiliaji wao mm nmeibiwa bado na hela nitoe sijui faili liende kwa mpelelezi nkaona bora nisamehe tu
 
Kipindi hiki ukitapeliwa basi utakuwa na matatizo! Pole mkuu! Zaman tuliishia kusema sadaka!
 
Lengo kuu la sheria za uhalifu wa mitandaoni ni kushughulikia wasumbufu wa kisiasa, matapeli ni kama wameruhusiwa hivi.
 
Back
Top Bottom