Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Baada ya taarifa ya kuvunjwa kwa CDA na shughuli zake kuhamishiwa Manispaa ya Dodoma,najiuliza majengo ya iliyokuwa CDA sasa kutumika kama mojawapo ya makao makuu ya wizara za serikali au ofisi za serikali zilizohamia Dodoma au majengo hayo sasa yatakuwa chini ya Manispaa ya Dodoma?
Nimewaza sana motive behind kwani nilitaraji labda ingevunjwa na kuundwa upya au kuifanyia mabadiliko makubwa ili iendelee na majukumu yake yaliyokuwa yamekusudiwa hasa kipindi hiki cha serikali kuhamia Dodoma badala ya kurundika kazi zote hizi chini ya Mkurugenzi mmoja /Management moja ambapo kuna hatari ya kuongeza ukiritimba unless CDA iwe ni kitengo maalumu kinachojitegemea ndani ya Manispaa ya Dodoma vinginevyo inaweza kuwa ni afadhali ya jana.
Kwa mfano,kupata hati ya kiwanja hapa CDA ilikuwa ni kero kwasababu ya sheria /utaratibu uliokuwepo ambapo hati zilikuwa zinasainiwa na Mkurugenzi Mkuu tu na hata aliekuwa anakaimu alikuwa harihusiwi kusaini kiasi kwamba akisafiri basi hati hazitoki na ilikuwa ni kila siku unapewa majibu ya njoo baada ya mwezi mmoja au wiki kadhaa Mkurugenzi atakuwa amerudi.
Sasa tujiulize kama sheria/utaratibu huu ndio utandelea huyo Mkurugenzi wa Manispaa mwenye majukumu mengi zaidi atamudu vipi kusaini hizo hati kwa muda mfupi zaidi ili kuondoa kero?
Ni kweli CDA ilukuwa kero na nina hakika wakazi wengi wa Dodoma watashangilia uamuzi huu ila bado inaweza ikawa ni furaha ya muda tu.