Kwa kuweka sawa mambo ni kuwa hizo nchi ulizotaja hazikuwa sehemu ya utawala wa USSR Bali walikuwa washirika wake Mwenye mambo ya ulinzi ikijulikana kama WARSAW PACT napia zilikuwa na Sera ya kijamaa kama USSR. Na umoja huo ulikuwa ni kukabiliana na NATO ya Marekani na nchi za kibepari za magharibi kama zinavojulikana leo. Baadhi ya nchi zilizounda USSR ni Uzbekistan ,Kazakhstan, Byelorus , Ukraine, Georgia na zingine kaama name zote zinamzunguka Russia ya Leo .Gorbachev hakupandikizwa yeye alianzisha ya Uhuru na Uwazi akiita Perestroika na Glasnost. Wahafidhina wa chama chake wakachukia wakampindua wakati yuko Mwenye mapumziko Mwenye pwani moja nchi ni kwake .Walipompindua hao wahafidhina ilikuta wananchi wameonja kautamu ka Uhuru waliokosa muda mrefu. Ndipo aliyekuwa meya wa Moscow Yeltsin akakataa kuyatambua Mapinduzi ya Wahafidhina akasema yeye anaunda taiga la Russia ambayo Ndiyo ya Leo .Wanajeshi wakamuunga mkono tens alipanda juu ya kifaru cha jeshi kupinga mapinduzi ya kumng'oa Gorbachev na Mapombe akiwa amelewa chakari. Ilipotokea hivo na vile vinchi jumuishi vikaona navyo vijitenge na ukawa mwisho wa USSR kamailivojulikana maana Russia ya Leo Ndiyo sehemu kubwa ya iliyokuwa USSR. Wakagawna Mbao kila nchi ikajitangazia Uhuru.Lakini Gorbachev alikuwa na nia njema ya kukomboa Uhuru wa RAIA ila sasa matokeo take ndio hayo badala ya kukomboa ikawa ni kuvunja nchi. Nakumbuka wakati wabunge wa G 55 wanataka serikali 3 za jamhuri ya Tanzania MWL Nyerere aliwauliza kuwa mumeishaandaa Yeltsin wenu maana hakukuwa na uwezekano wa serikali tatu halafu Muungano wetu ukabaki kama ulivyo. Ndivo ninavoelewa kusambaratika kwa USSR. Na kwa kweli lilikuwa li nchi kubwa lenye mfumo kandamizi ikawa Politburo ya watu 13 wanaokaa Moscow ndio walichagua viongozi wa USSR yote. Kwa hali hiyo wananchi hawkuwa na mapenzi na Muungano huo ndio maana ilisambaratika wananchi wanashangilia. Na ukawa mwisho wa ukuta wa Berlin na Warsaw Pact maana zilishikiliwa na dude hill la USSR. ndivyo ninayoikumbuka hiyo mianzo ya 1990's