Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na uzao kutokuwa na mvuto.Mtu alitegemea azae mtoto mwenye muonekano fulani,lakini kutoka na sababu zilizopo nje ya uwezo wake akaja tofauti.Kuna makala moja nilisoma ilikuwa inawahusu raia wawili wa nchi fulani,inaelezea mwanamke aliyekuwa na sura mbaya akafanyiwa 'plastic surgery' ya sura na maungo yake.Baada ya muda alikuja kuolewa,na akajifungua watoto kadhaa na wote walichukua sura yake halisi...wakawa hawavutii,sasa mumewe akafungua kesi kwa nini mkewe amemzalia watoto wenye sura ambayo haieleweki?katika migogoro ya namna hii,nani huwa chanzo cha haya yote?