KUUZWA KWA NYUMBA ZA SERIKALI KWA HASARA NI JIPU ?

wuhulo

Member
Feb 20, 2016
28
8
Katika utawala wa Awamu ya 3 zilizokuwa nyumba za serikali nchini ziliuzwa kwa mizengwe kwa bei ya chini sana ukilinganisha thamani halisi ya nyumba na viwanja vyake.

Kuna nyumba zilizokuwa katika viwanja vikubwa kiasi kwamba walionunua waliweza kujenga nyumba nyingine hadi tatu au kuweka majengo ya milango ya biashara yenye milango isiypungua 10 bila kuingilia nyumba iliyokuwepo.

Hakukuwa na sababu hasa ya msingi iliyosukuma nyumba zile kuuzwa zaidi ya ubinafsi wa viongozi hasa katika baraza la mawaziri kwa kutamani ulaji ule .

Kutokea wakati ule watumishi wa serikali wenye hadhi ya kupewa nyumba wamekuwa wakitumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kulala katika hotel za gharama kubwa badala ya fedha hizo kufanya shughuli za wananchi kama vile huduma za shule, maji au afya.

Zoezi hili la uuzwaji wa nyumba za serikali lilikuwa la kiharamia lililoacha maswali mengi ambayo hadi leo yanaulizwa. Mfano mmoja kuna nyumba ziliuzwa zikiwa zinamilikiwa na Jeshi la polisi zilikuwa mita tano kutoka vituo vya polisi na walionunua kwa sasa walishastaafu kazi hivyo unakuta zinakaliwa na raia wa kila aina wazuri na wabaya.

Nina mifano hai mingi ya madhara yanayoendelea kutokana na kadhia hii, namuomba mhe. na wah.wanaomsaidia waone hili jipu na KULITUMBUA ninafahamu gharama za kurejesha siyo kubwa kwani wanunuzi walizuiwa kuziendeleza kwa mda mrefu abao haujaisha. Ingawa ktk utawala wa JK wanunuzi wameendeleza sana majengo na viwanja vyake.

Sasa kama na mh. JPM anahuska sijui itakuwaje. mmmh. asante.
 
Ngoja nimpelekee Mbunge wangu swali alipeleke bungeni.
Kwamba in kiasi gani cha Pesa kilitumika kwa mwaka wa fedha 2014/15 kuwalipia watumishi wa umma mahotelini kwa kukosa nyumba za kuishi. Hii no kuanzia mawaziri, majaji,makamishna hadi maofisa wa chini wenye stahili ya kupewa nyumba.
Nahisi kuna watu watazimia kwa hiyo figure itakayo tajwa
 
Katika utawala wa Awamu ya 3 zilizokuwa nyumba za serikali nchini ziliuzwa kwa mizengwe kwa bei ya chini sana ukilinganisha thamani halisi ya nyumba na viwanja vyake.
wuhulo, naomba nikurudishe nyuma kidogo, miaka kumi nyuma hadi Mei 26, 2006 miezi michache tu baada ya chaguo la mungu, Jakaya Mrisho Kikwete kukamata madaraka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Kama kawaida ya Watanzania, Raisi mpya huyo aliingia kwa mbwembwe na msururu wa wapiga debe na mashabiki hadi humu JamiiForums (wakati huo ikiitwa JamboForums) kama tunavyoshuhudia hivi leo kwa chaguo lingine la mungu, hapa kazi tu na utumbuaji majipu.

Serikali mpya ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya iliwateka mioyo wengi na yupo mwana JF moja (Mzee Mwanakijiji) aliyeshindwa kujizuia mpaka kuanzisha mada iliyosema, Hatimaye Kikwete afanya kweli.

Naomba kuorodhesha kidogo tu michango kama ilivyotolewa na wachangiaji wa wakati huo...

2006

Mzee Mwanakijiji: Kwa mujibu wa habari, serikali ya Jakaya Kikwete imesitisha mara moja uuzaji wa nyumba za Serikali kwa viongozi na kuanzia sasa nyumba hizo hazitouzwa tena.


He got some nerves, Kuna watu imedaiwa wamekasirishwa na kitendo hicho.



Field Marshall, ES: I do not buy this nonesense!, alikuwa wapi siku zote? kuzuia sasa faida yake ni nini wakati tayari nyumba zote zilizotakiwa kuuzwa zimeuzwa? Hebu nitajieni ni kiongozi gani wa zamani ambaye alitaka kununua nyumba ameshindwa? Nia na madhumuni ya kuuzwa kwa nyumba ilikuwa kuwapatia viongozi wa zamani nyumba, na hilo limeshatimia tayari sasa huu mkwara ni wa nini kama sio uongo?

Look at this, BM amenunua ile nyumba ya Sea View, JM amenunua ile nyumba ya Sea View, JK mwenyewe amenunua, Sumaye amenunua, Kawawa alijengewa bure, Msekwa amenunua, Siwale amenunua, Jumbe amenunua, Mwinyi amenunua, Msuya amenunua…Warioba tu ndiye aliyekataa…


Wazee, hii serikali inadanganya kuhusu nyumba, ukweli ni kwamba tayari wazee wote wa CCM walishapata nyumba ndio maana sasa wanasimamisha, NONESENSE!


Mzee Mwanakijiji: Mzee ES, mimi nilikuwa shabiki wa Mkapa just kutokana na habari za magazetini, lakini jinsi JK anavyoanza kufanya haya mambo naanza kujiuliza hivi Mkapa alikuwa ni Rais wa nchi gani? Nafikiri kama kuna mtu ambaye Nyerere anajutia kutupa Watanzania ni Mkapa.


Angalau Mwinyi ilikuwa ni majaribio ya utawala bila Mwalimu!! Mimi nafikiri Rais afanye hatua moja zaidi. Kama kuna kiongozi yeyote aliyenunua nyumba za serikali zaidi ya moja, basi warudishe hizo nyingine serikalini!!! Wachague ni ipi wanataka kuendelea kuwa nayo, na hizo nyingine zirudishwe kwenye matumizi ya serikali au ziuzwe kwa wafanyakazi wa kati!!



Nurujamii: Du niliichangamkia hii thread kwa spidi ya ajabu. Nilidhani JK kaamua kumshughulikia Mkapa. Kumbe...


Field Marshal, ES: Kati ya viongozi ninaowaheshimu bongo na nitawatetea mpaka dakika ya mwisho, Mramba ni mmoja wao, kazi aliyoifanya hazina kipindi cha Mkapa, haina mfano,


sasa hivi amepewa wizara yenye mlo, na yeye si mtandao ndio maana kuna kampeni kubwa sana ya kumdhalilisha ili hatimaye atolewe, na hiyo ndio siasa mpya ya kimtandao tuliyonayo sasa, leo uongozi ni unamjua nani, sio tena unajua nini,

lakini Mramba is a good man, na technically a good leader, isipokuwa sio politician, kama Mkapa alivyokuwa, hakuwa mwanasiasa!


Halafu atuhakikishie kuwa hizo nyumba mpya walizopewa Mawaziri hazitauzwa kwao baada ya uchaguzi ujao. Hizo zibakie kuwa ni nyumba za serikali.


Kitila Mkumbo: Kuhusu, vyombo vya habari, naam, nimerudi jana Bongo na nitakuwa hapa kwa utafiti kwa miezi mitatu. Leo nimejaribu kudodoza magazeti; mpaka sasa niandikapo hii post sijaamua ninunue gazeti gani! Kila gazeti limesheeni, pamoja na Tanzania Daima ambayo imesifiwa kuwa na mlengo tofauti, habari za kumtukuza JK na serikali yake. Hamna hoja mpya. Kwa hiyo ukinunua gazeti moja huna haja ya lingine. Na kama unatafuta kitu gani kinaendelea ndani ya nchi zaidi ya sifa kwa serikali itakuwa vigumu kupata.


2015


Nguvu ya Hoja: Waziri mhusika wa kuuza nyumba sasa yupo Ikulu, vipi zoezi litaendelea au itakuwaje mzee?


KORBOTO: Kumbe ni kawaida Mzee Mwanakijiji kuyumba vipindi kama hivi


pepsin: Alichofanya Kikwete ni hicho hicho anachofanya Dr Magufuli…First impression!


2016


Mzee Mwanakijiji: Go Magufuli go. Mabadiliko yana gharama na maumivu! Mwanzoni kabisa baada ya kuchaguliwa kwa Magufuli na kazi ilipoanza nilisema kitu ambacho sidhani kama watu wengi walielewa au walidhani nasema tu kwa sababu ya ushabiki.


Nchi yetu ilipokuwa imefikia kiongozi yeyote ambaye alikuwa anakuja kuupokea uongozi uliopita jukumu lake la kwanza kabisa lilikuwa ni kusafisha; kuleta nidhamu na kubwa zaidi kupambana na ufisadi kama simba mbele swala. Sidhani kama watu walitegemea shock and awe ambayo inaendelea sasa nchini na labda inakwaza watu wengi.


Mag3: wuhulo, Wadanganyika ndivyo tulivyo. Tupo wachache tunaotambua kuwa adui wa nchi hii ni CCM na msimamo huo tumekuwa nao tangu tunadai mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa 1990s. Wapo wengine wanaoamini kwamba nguruwe ukimpaka lipstick hawi tena nguruwe, anakuwa binadamu mrembo.

Alikuja Mwinyi na mfagio wa chuma, akaingia Mkapa na uwajibikaji na utandawazi, akaja Kikwete na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya na sasa kaingia Magufuli na hapa kazi tu pamoja na utumbuaji majipu...ambacho kimebaki kile kile, oh ni kile kile, ni CCM.


Ili kuisoma thread nzima, bonyeza hapa chini;

 
Back
Top Bottom