Nani wamenunua na nani wanahusika?
Akizungumzia suala la Rais Mstaafu Mkapa ambaye aliomba kumiliki hisa 200,000, kupitia kampuni yake ya ANBEN Limited, Ngeleja alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani alinyang'anywa hisa hizo Januari 10 mwaka 2005 baada ya kushindwa kuzilipia.
"Mheshimiwa Spika, tarehe 10 Januari, 2005, (Siku 13 tangu kuanzishwa kwa TPR), ANBEN Limited iliondolewa kuwa miongoni mwa wamiliki wa hisa kwa vile haikuweza kulipia hisa ilizokuwa imechukua wakati wa usajili wa TPR.
Hivyo wamiliki wa TPR waliobaki walikuwa ni DevConsult International Ltd, Universal Technologies Ltd, Choice Industries Ltd na Fosnik Enterprises Ltd zote zikiwa na hisa 200,000," alisema Ngeleja. (News 2012)