Kuuzwa kwa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira

babad

Member
Feb 9, 2011
95
13
Kwa habari ya faster niliyosikia jana kwenye vyombo vya habari mgodi wa kiwira umeuzwa kwa wawekezaji,wana JF hii ina maanisha nini wakati serikali ndo iko kwenye mchakato wa kutumia makaa ya mawe kupata umemem endelevu?
 
Kama ni kweli, wauzaji na walionunua wapelekwe kwenye vyombo vya sheria. Tuone sasa wanaharakati wakiwafikisha hawa mahakamani vinginevyo waache uanaharakati wao!!
 
Nani wamenunua na nani wanahusika?

Akizungumzia suala la Rais Mstaafu Mkapa ambaye aliomba kumiliki hisa 200,000, kupitia kampuni yake ya ANBEN Limited, Ngeleja alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani alinyang'anywa hisa hizo Januari 10 mwaka 2005 baada ya kushindwa kuzilipia.

"Mheshimiwa Spika, tarehe 10 Januari, 2005, (Siku 13 tangu kuanzishwa kwa TPR), ANBEN Limited iliondolewa kuwa miongoni mwa wamiliki wa hisa kwa vile haikuweza kulipia hisa ilizokuwa imechukua wakati wa usajili wa TPR.

Hivyo wamiliki wa TPR waliobaki walikuwa ni DevConsult International Ltd, Universal Technologies Ltd, Choice Industries Ltd na Fosnik Enterprises Ltd zote zikiwa na hisa 200,000," alisema Ngeleja.
(News 2012)
 
Yeyote atakaye miliki mgodi huo anafaida ya kupata mkaa, Iron Ore na Uranium. Itakuwa ni uzembe wa kurudia kuuza mgodi wenye vyote hivi kwa bei ya kimoja. Sawa na kuuza migodi ya buliyankulu, buzwagi na mengineyo kwa kuchimba dhahabu kumbe wachimbaji wanapata faida ya Platinium na Uranium. Itakuwa ni uzembe wa maksudi.
 
:lol:

Mbona mnaogopa kumtaja, au uzushi tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom