Kuumwa na Kichwa Baada ya Mazoezi......?

peter willson

Member
Dec 4, 2015
19
3
Habari.

Mimi huwa nafanya jogging ambapo huwa natumia saa moja
au mawili. Huwa ninaumwa na kichwa baada ya mazoezi (siyo mara tu nimalizapo), nikiwa nimepumzika.
Tatizo ni nini, na je itaniletea madhara gani?

Naomba kuuliza.
 
Huwa inatokea lakini mara nyingi kuumwana kichwa kuna sababu nyingi,inaweza kuwa ni Malaria,matatizo ya macho,pressure,joto kali,kukukosa usingizi wa kutosha,kukosa muda wa kupumzika,mawazo mabaya,n.k.Kwa ushauri kabla ya kuendelea na mazoezi yako pima afya yako kwanza na pia uangalie kiwango cha mazoezi unachofanya kinalingana na umri au uzito wako?isijekuwa umeanza mazoezi magumu kwa kasi wakati inatakiwa dose iongezeke taratibu..
 
Habari.

Mimi huwa nafanya jogging ambapo huwa natumia saa moja
au mawili. Huwa ninaumwa na kichwa baada ya mazoezi (siyo mara tu nimalizapo), nikiwa nimepumzika.
Tatizo ni nini, na je itaniletea madhara gani?

Naomba kuuliza.

Jitahidi uwe unakunywa maji sana baada au wakati wa mazoezi
Kichwa kinauma kwa sababu ya kukosa maji mwilini yanayopotea kwa njia ya majasho
 
Chukua maji yatie Glucose uwe unakunywa ufanyapo mazoezi. Kichwa kuuma ni dalili ya upungufu wa chumvi na sukari.
 
Back
Top Bottom