Kutumia mafungu na visado kupima bidhaa ni hasara kwa wauzaji na wanunuzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Wananunuzi wa bidhaa sokoni wametakiwa kununua bidhaa zilizo pimwa katika mizani ili kuepuka kupunjwa.

Hayo yameelezwa Novemba 4, 2020 na Denis Misango, Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Kilimanjaro wakati akizungumza na Darmpyablog juu ya umuhimu wa kutumia mizani pamoja na hasara ya kutokutumia mizani.

Misango ameeleza kuwa wateja wengi wamekuwa wakipunjwa bidhaa wanazo nunua sokoni kutokana na bidhaa hizo kutokupimwa hivyo mteja kupata huduma pungufu kulinganisha na hela anayotozwa.

“Bidhaa za masokoni ni kama mbogamboga zote na matunda ambayo yanapimwa kwa sadolini au kwa mafungu, vipimo hivyo siyo sahihi kwani vina hasara kwa mnunuzi na muuzaji, ikiwa mteja atanunua bidhaa zilizo pimwa kwa namna hiyo kwa asilimia kubwa atakuwa amepunjwa” alisema Misango.

Ameongeza kuwa mbali na mteja kupata hasara ya kupunjwa pia muuzaji anapata hasara kubwa kwani kuuza nyanya, vitunguu,hoho, viazi, karoti pamoja na bidhaa nyingine kwa njia ya sadolini au kwa mafungu, muuzaji anapata hasara, kwani kila bidhaa zinatofautina uzito hivyo ni bora kutumia mizani ili kupima kwa kilo.

“Wanaotumia mizani lazima waone faida ya kazi wanazofanya sokoni, muuzaji hawezi kupata hasara ya mzigo wake bali faida kutokana na kupima bidhaa huku mnunuzi akipata faida kwa kununua bidhaa katika kiwango husika” Alisema Misango.

Katika upande mwingine Misango amewataka wauzaji wa nyama na bidhaa nyingine za nyumbani katika maduka mbalimbali Mkoni huko kuhakikisha wanakuwa na mawe yenye uzito wa vipimo vyote na yaliyo hakikiwa na wakala wa vipimo.

“Wapo baadhi ya wauzaji katika maduka wanasema kuwa hawana mawe ya kilo zote zinazohitajika kwa kisingizo kuwa hayapatika badala yake wanatumia bidhaa nyingine iliyo pimwa kama mbadala wa jiwe au wengine wanatumia kiberiti na pakiti ya majani ya chai kupata mizania ya kilo jambo ambalo ni kosa kisheria,kama huna mawe yote yenye ujazo fika ofisini kwaajili ya kupatiwa mawe hayo ukafanye biashara kwa haki na faida. Alisema Misango.
 
Back
Top Bottom