Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,764
- 2,347
Tumeona kasi ya Mh Magufuli katika kuhakikisha heshima ya serikali kiutendaji inarudi kwenye viwango vyake.Tumeona ubadhilifu wa kutisha unaofanyika, hususan Bandarini, TRA na vitengo vingine ambavyo ni vyanzo vya mapato ya serikali.
Wahusika wametumbuliwa huku kukiwepo na ushahidi usiotia shaka, uhusika wa watumbuliwaji majipu.Hata wegine wamejikuta wakiingia kujibu maswala ya jinai kwa uhusika wao.
Lakini inabidi tuwe na staha katika zoezi zima.Mwizi lazima achukuliwe hatua kisheria kama inavyotakiwa, si kukomolewa.Ikiingia suala la kukomoana, zoezi zima linaanza kupata ukakasi.
Majuzi Waziri wa Utumishi a Utawala Bora, Mh Angela Kairuki amsimamisha kazi Mkuu wa Chu Cha Utumishi nchini wakiwa wamekaa meza moja!
Watu wa kawaida wanapata hisia tofauti juu ya hili.
Hakuna waziri aliyefundishwa au kupata maelekezi juu ya utumbuaji majipu, lakini hata kama mtu huyu ana makosa, ni staha tu kumwita pembeni, hata wakiwepo wapelelezi na kumwambia tuhuma zake na baadaye hata kumfungulia mashtaka.
Hii la la huyu jamaa, Mkuu wa Chuo cha Utumishi halipendezi sana kulisikia maana linachukua sura ya kukomoana.Tukumbuke kuwa cheo ni dhamana, tusipende kutenda kile tusichopenda kutendewa hata kama kuna kosa.