GE2025 Kutoshiriki Uchaguzi: Faida ya Usalama kwa Wagombea na Wanachama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
3,112
Reaction score
5,364
Nimekuwa nikifuatilia taarifa kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Kwa kweli tusibeze uamuzi wa CHADEMA kususia uchaguzi kwani umewasaidia sana viongozi, wagombea na wanachama wao angalau kuwa na usalama kuliko kama wangeshiriki.

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu kuzinduliwa kampeni hatujasikia kiongozi au mgombea wa upinzani kuanzia udiwani akiwa ametekwa au mivugugano ya kuenguliwa holelaholea kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita tofauti na Mpina wa ACT.

Uzoefu unaonesha mwaka 2020 hali ilikuwa mbaya sana kwa wagombea wa upinzani hasa CHADEMA, mara huyu kaenguliwa, mara yule kakimbiwa ofisi wakati wa kurudisha fomu nk. Lakini mwaka huu kila mtu ni shahidi, hali imekuwa shwari kwa kiasi fulani hatusikii matukio. Purukushani ni chache kuanzia kipindi cha uchukuaji wa fomu mpaka sasa katika kampeni.

Wakati mwingine unahitaji kuwa mvumilivu, na kulitoa muhanga jambo hili ili upate lile lililo bora zaidi.

Kitendo cha CHADEMA kususia uchaguzi ni bora zaidi kwao kuanzia usalama wa wagombea na wanachama wao kwa ujumla.

Wamejitoa muhanga kupoteza miaka mitano ambayo si mingi sana kwani siku hazigandi.

Katika miaka hii, ni vyema wakabuni mbinu mpya za kuishinikiza serikali kuendeleza mchakato wa katiba mpya na kuwa na uchaguzi huru na haki. Kama watafanikiwa, basi come back ya CHADEMA mwaka 2030 itakuwa na faida sana kwao na wakishindwa basi itakuwa ni hasara pia.
 
Naunga mkono hoja na hapo ndipo utajua kiwa CCM ni tatizo na ni kansa nchini
 
Back
Top Bottom