Kutokuwepo magari ya UDA barabarani Dar nini tatizo?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,924
8,174
Wadau Wa JF, mabasi ya UDA ya Nazi Mmoja - Kivukoni Leo hayaonekani, je tatizo no nini? Vipi sehemu nyingine yapo huko?

Leo karibu jiji zima la Dar hakuna magari ya Uda karibu njia zote ambazo zimekuwa zikitumiwa na magari hayo.

Tetesi zilizopo ni kwamba, mmiliki amepewa muda ajitokeze.

Kwa anaye jua taarifa juu ya hili atujuze. Magari haya yamekuwa msaada hususani kivukoni na mnazi mmoja ambako magari mengine hayaruhusiwi kutoa huduma isipokuwa UDA tu.
 
Kwani mmiliki wa Uda hujulikani,waache mazingaombwe,ni vigogo wa CCM ,Robert Kisena na Idi Simba,hata Magufuli anajua.
 
Kwa nini magari mengine hayaruhusiwi kutoa huduma kwenye njia hiyo, au ndio ukiritimba?
 
Kwani mmiliki wa Uda hujulikani,waache mazingaombwe,ni vigogo wa CCM ,Robert Kisena na Idi Simba,hata Magufuli anajua.

Hao wamekataa kuhusika na umiliki wa UDA, kunatetesi eti hata wao wanashangaa kuhusishwa nayo
 
Kusema mmiliki ameombwa ajitokeze, hizo ni tetesi tu. Ukweli mwenye nayo anajulika, maana mpaka wanapewa tenda ya kubeba abiria peke yao tu toka mnazi mmoja - kivukoni, dar wanaruhusiwa kwenda ruti zote za mjini. Pia, kwny kampeni zao za dar ktk uchaguzi mkuu ccm wametumia sana hizi basi za UDA. Labda kwavile mkubwa ameamua kuimba na mfanyabiashara yeyote anayekwepa kodi, bila kujali amechangia kwny kampeni au la.
 
Hao wamekataa kuhusika na umiliki wa UDA, kunatetesi eti hata wao wanashangaa kuhusishwa nayo
Kama Uda imekosa mmiliki Serikali iichukuwe mala moja,Mungu ni mkubwa mali ya wananchi imeludi.
 
Si tulisikia zimezuiliwa, ama zilishaachiwa tena?! Hata mimi sijajua bado, wengine tupo nje ya mkoa!

Ahsante!
 
Nikisikia Uda toka mgogoro ule wa wa wabunge wa dar walipolalamikia kuhusu uuzwaji wa shirika hili na kuambiwa wanafikiri kwa kutumia............
Sina hamu na shirika hili, yawezekana lisemwalo lipo kama halipo linakuja ngoja tusubiri mwisho wake.
 
Back
Top Bottom