kutokulipa ada yawarudisha wanafunzi udom nyumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kutokulipa ada yawarudisha wanafunzi udom nyumbani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by SOKON 1, Jul 4, 2011.

 1. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Haya ndio maamuzi ya kisiasa dhidi ya chama kinachotawala nchi kwani maamuzi ya kitahalumu yamewekwa kando na kulinda maslai yao kwa kufunika kombe mwanaharahu apite.
  Wanafunzi wa udom kwa wale ambao hawana uwezo wa kulipa ada jana wameambiwa warudi nyumbani waje kufanya mtihani mwenzi wa tisa pindi watakapo kamilisha kulipa ada.
  Pia wameamua kufanya ivi kwa dhumuni la kukomoa wanafunzi na pia kama njia ya kuwapa adhabu ili wasigome tena. Pia hakuna majibu ya field yaliyosababisha mgomo ila wanafunzi wanachotakiwa ni kufanya Mitihani na sio vinginevyo.
  My take;
  Wakati mwanafunzi huyu akiwa sekondari alishindwa kulipa elfu ishirini vipi leo awe na uwezo wa kulipa milioni?
  Tanzania ni nchi yetu sote, ujamaa na upendo tulioachiwa na baba wa taifa tufaidi wote ila leo hii tumeanza kutengana kwa matabaka nchi yetu inapoelekea Mungu mwenyewe ndio anajua.
  UDOM bomu lingine na limeshaanza kuleta madhara kilichobaki ni kusambaa kwani kujengewa chuo na kupewa mkopo wamekuwa watumwa kwa serikali ya ccm na kuamua kufanya watakavyo dhidi ya wanafunzi.
  Nawasilisha
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  wanachokipanda watakuja kuvuna kwa majozi ,kwa nini sasa waliwaiita si wangewambia wabaki huko nyumbani,wao hawajali kitu,wao watoto wao hata wa mahawara wako marekani austalia,afrika kusini au marekani,watoto wa KIkwete wale pacha aliozaa na Rahma wanasoma marekani unadhani atakuwa na uchungu na watoto wa maskini na wakulima hapo
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Hao wanafunzi wako wangapi mkuu?
   
 4. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  wapo wengi kwani ata kama unadaiwa elfu kumi wanakurudisha nyumbani kama unavyoelewa hali ya watoto wa wakulima.
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  dah!!kazi 2nayo..
   
 6. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Hizo ndizo faida za migomo mkuu, so tafuta wanafunzi waliosoma DIT na UDSM mwianzoni mwa 2000 watakuambia, hakuna mgomo ambao uliwafaidisha wanafunzi.
   
 7. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  lakini hili linatokea kwa vyuo vya serikali tena chukulia kama mzazi umeangaika na mwanao mpaka kafika chuo ila mtawala mbovu wa mwongozo wa masomo ndio unamfukuzisha mwanao chuo wakati akipigania kupata elimu bora na sio bora elimu ungefanya nini?
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi sishangai saaana,udsm ilikuwa hata kama unadaiwa mia,nini buku teni.......

  Wanafunz wa udom lazima mtambue kuwa wanasiasa wanawatumia sana......kuanzia na jk ambae alikuja huko na wakatumia kigezo cha kuchangiwa pesa na wanafunz ili akachukue fomu........lakini pia wapinzani nao wanataka wasomi
  rejea maon ya wakuu wa wilaya waliotembelea UDOM,walisema wanafunz wa ccm warudishwe ila wale wa chadema wasirejeshwe maana wana vurugu.....tazama maajabu haya......
   
 9. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Zaidi ya wanafunzi elfu 18 udom hawana imani na serikali yao kwani kwa kudai maslai yao ya elimu bora wanaambulia vitisho na kufukuzwa chuo walianza wanaosomea ualimu walifukuzwa mwaka 2009, wakaji wanaosomea komputa wamefukuzwa, wakafuata wanaosomea sayansi wamefukuzwa, wakafuata wanaosomea takwimu nao wapo nyumbani bila kuwasahau sayansi na jamii wote wapo nyumbani je serikali yetu ya ccm inajivunia chuo kikubwa ama chuo kikuu?
  Ila wakumbuke hawasomi bure kwani ule ni mkopo iweje iwaburuze na kuwapa elimu mbovu na kuwalazimishia kuihita degree wakati haijatimiza vigezo ukilinganisha na vyuo vingine.
   
 10. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Yanayojiri udom ni elimu mbovu na ndio yanayoleta mgomo na sio siasa ila kwa kutafuta mtaji wa kisiasa ndio yanaleta kuonekana udom yanayoleta mgomo inasababishwa na wanasiasa.
   
 11. S

  Sebali Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika kuwa Udom inaendeshwa kisiasa zaidi. Viongozi wa chuo wanakuwa hawana maamuzi sahihi kutokana na kuingiliwa na viongozi magamba wa nchi hii. Nimeamini Udom imekaa kisiasa zaidi kwa chama cha magamba kujifunzia kunyolea ndiyo maana migomo kila siku haiishi. Poleni wana Udom!
   
 12. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kuna wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao wanadai ela ya field baada ya kwenda field wakisubiria hela ila mpaka sasa hawajapewa ila kwa sababu ya kuogopa kufukuzwa chuo imebidi wanyamaze kwani wamefuatalia mpaka siku walipofukuzwa wanafunzi wote wa sayansi na jamii.
   
Loading...