Kutokana na sababu hii, CHADEMA inasambaratika na CCM inainuka

Mimi sio CDM.
Lakini msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Naona Kama unaingiza topic mpya hapa ya kumhusu Lowasa.
Hasa Unapohoji ajenda ya CDM tangu Mamvi aingie.

Mpaka sasa:-
Kile niNachojua,
Mkuu amepiga marufuku siasa za majukwaani, akidai mpaka 2020.
(Ajenda utaisikia wapi? Kama hakuna mikutano)

Ingawa yeye amekua akijipigia siasa Kama vile;- kuwapokea madiwani wapya wa CDM waliohamia CCM.(hapa napo IPO shida kwa mujibu WA kanuni za nchi na Takukuru)

Pia Mkuu apandapo jukwaani kwenyw majimbo ya wapinzani, haachi kuwalaumu wananchi wa majimbo kwa kuchagua wapinzani. Etc.(so sad!)


Amepiga marufuku maonbezi kwa Lisu,
amepiga marufuku Wabunge wa Upinzani iwe Bungeni au nje ya Bunge kukosoa serikali yake especially namna anavyotatua swala La Rasilimali za Taifa hususani madini yetu, bombadear yake.

Na Amemtaka Spika kutunga sheria mpya ili kuwadhibiti wapinzani WA Serikali yake ndani ya Bunge.

Yeye amekua hakimu na amekua bunge.

Mfano:-Ameonyesha waziwazi kumtetea Bashite aliyefoji Cheti. Kwa maana hii amezuia Takukuru(PCCB) wasifanye kazi yao.

Kupitia uongozi wake, CUF walinyimwa haki ya kushika dola kule Zanzibar.

Amepiga marufuku kujadili namna bashite alivgovamia chombo Fulani cha habari. Kudhihirisha hatanii akamfukuza kazi waziri wake wa habari kwa kuunda tume tu ya kumshauri. Which implies hashauriki! Kama asemavyo yeye mwenyewe kua anajiamini.


Mbali na wakina Roma kutekwa na kutokuruhusu uchunguzi. bado
Amepiga marufuku wasanii kuimba siasa.

Na wewe unashuhudia haya bado unahoji ajenda mpya ya CDM? Yaani hata wasanii wananyimwa ajenda!!?!.


Bado unafurahia kusikiliza mziki wa Uongo unaopigwa masikioni kwako militia gazeti LA Uhuru.
Ni kweli kua na macho sio kuona. IPO tofauti Kati ya kutazama na kuona.

Kama utaniuliza Mimi ajenda ya CDM. naona ni ile ya kupinga UDIKTETA.

Ndiyo ilioshika kasi Sana hapa nchini.

Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni. Utawala wa juu wa CCM umekua ukimuhofia Lowasa (unayemwita mamvi) kuliko kitu ingine. Na inaonyesha wangetamani wamtoa uhai ila ndo hivyo tena. Mungu hajaruhusu.
Pia napata picha kua lowasa sio WA nchi hii.

Kama aliweza kuwavuruga,na kuwagawa wana CCM kisha kwa mtazamo wako amemvuruga Dk Slaa with his ambition to become a President of Tanzania kupitia CDM 2015.

Huyu MTU sio WA kubeza hata kidogo. Maneno machache lakini his actions are louder. Chama chako pale Lumumba wanamjua zaidi.
Lowasa Hajawahi kumjibu MTU maneno ya kuudhi au kumtusi sijui mpumbavu, pigeni mbizi wivu wa kike nk.

Mpaka Leo kuna watu wanaendelea kufukuzwa ndani ya CCM kwasababu yake.
CCM ilibadili structure yake(Organogram) ili tu kudhohofisha mzimu wa Lowasa ndani ya chama Chao. Still bado mamvi amebaki kua Pasua kichwa na ajenda kuu mpaka 2020.
Kibaya kuliko vyote, hawawezi kumpata na kumuundia kashfa.
Kila wanalumumba wakisema wanatumbua jipu, wanaishia kutumbuana wao kwa wao.

And yet unaona haya ila huoni uzito wake.
Wakati nyerere alikua akipambana na maadui watatu kwa mpigo na wakamshinda wote.

Lowasa aliwahi kusema priority kubwa ya nchi ni Elimu, ya pili ni elimu ya tatu ni Elimu.
Kwakua igonarance imekua stumbling block ya kudumaza fikra huru.
 
Na ccm inafanya nini mbona hamdhibiti mabaya yote yanatotendeka nchini. Mnadhani watu wote ni wJinga?
 
Labda ccm ya malawi hii ya hpa ni mfu kabisa imebaki kutumia mabavu na uwongo mwingi kila kukicha
 
Labda sasa mtusambaratishe na mabomu kama rais wako kakutuma mwambie sasa tutaingia mitaani bora tufe au tuwe na democracy


Swissme
Wewe utaendelea kufraisha nafsi yako hapa JF lakini za kuingia mtaani itaendelea kubaki ni hadithi!!
 
1.Kama CCM inainuka kwanini mikutano halali ya siasa imezuiliwa?

2.Kama CCM inapeendwa kwanini haitaki tume huru ya uchaguzi?

NB : Sio lazima kunijibu you can choose to ignore me.
 
1.Kama CCM inainuka kwanini mikutano halali ya siasa imezuiliwa?

2.Kama CCM inapeendwa kwanini haitaki tume huru ya uchaguzi?

NB : Sio lazima kunijibu you can choose to ignore me.
Haijazuiliwa kabisa. Hata wale walioruhusiwa wanafanya hiyo mikutano? Mbona mnaomba vitu mkipewa mnazidiwa tena, au lengo lenu lilikuwa kuleta vurugu? Aliyekuambia tume haiko huru ni nani?
 
Ccm ishakufa kitambo bali sasa ipo kwenye oxygen tu siku mipira ikichomoka basi tunazika mzoga
 
Yaani umejiunga leo jf kuja kuharisha mtandaoni?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…