Kutokana na kuwa na Wizara YA Kilimo

Kutokana na kuwa na Wizara YA Kilimo

StevMsuya

Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
30
Reaction score
11
Siku chache baada ya Mhe. Dkt. JPM kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri na kutenganisha Wizara iliyokuwa imechanganywa na kilimo na ufugaji, achana na Ile ya Nishati na madinj. Nimeona haja kwa Mawaziri walioteuliwa katika Wizara ya Mifugo kuainisha FURSA zilizopo katika sekta hii kusudi kusaidia kuboresha hali ya ufugaji ambapo Kutokana na ufinyu wa extension services kwa wafugaji imekuwa chanzo cha migogoro ya wafugaji na wakulima(ardhi).
Binafsi FURSA ninayoiona kwasasa ni kwa serikali kuhamasisha uanzishaji na uboreshaji wa miradi mikubwa ya ranches zilizopo au zitakazojengwa ili kuokoa jamii ya kifugaji na Wao kuchangia kwenye uchumi wa viwanda na kuzalisha ajira hasa vijijini.
RAI YANGU zaidi ni kwa Wizara ya Mifugo iunde tume itakayoibua FURSA zilizopo ndani na nje YA nchi na kuweka mazingira wezeshi kwa watanzania kushiriki katika FURSA hizo.

Nawasilisha
 
Ushauri mzuri mkuu, fursa hizo zitasaidia vijana kujikwamua na suala la ajira linalowakabili
 
Likifanyiwa kazi hilo, litatusaidia vijana wengi sana
 
Back
Top Bottom