Kutoka vipele kwenye uume

mtengwa

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
1,600
847
Ilianza na kasehemu kadogo kuwasha then kuanza vipele vidogo, now vimekua kama kidonda ingawa ni kasehem kadogo ka uume, haviumi sana. Kuna dokta jiran nilimuonyesha nikamwambia last j'mosi nilikunywa mitakelfin n 4rm j3 ndo vipele vikaanza. Akaniambia nitakua nina alegy na dawa zenye sulphur akanipa vidonge vimeandkwa cosmos. Bt bado hali iko vile vile. Naomba Ushauri jf doctor
 
Ungeeleza kuhusu hali yako ya ndoa ingeweza kusaidia, kwa sasa ni vizuri ukaenda kupima damu kipimo cha vdrl, siwezi kusema kama ni dalili za ugonjwa wa zinaa ikiwa hujapima wala kusema kama umengonoka lini na nani.

Ikiwa umeoa ni suala moja na ikiwa hujaoa na huna mpenzi mmoja basi ni suala la pili
 
Sijaoa na last time 2 have sex ilikua ferbuary this year, ilishawahi kunitokea mara moja kikakaa wiki moja na nusu hadi ikakauka but it was 3 years ago
 
Yapo magonjwa ya zinaa yenye sifa hizo na kwa girl dalili huchukua muda mrefu kuonekana tofauti na kwa wanaume, syphilis kwa mfano, huweza kusababisha vipele mwilini na inapokomaa husambaa na kuathiri maeneo mengi ya mwili hadi ubongo.

ugonjwa huu (kisosnono!!!) huonekana kama si tatizo, kikubwa nenda hospital kapime na usijaribu kutumia dawa bila kukutana na daktari na wala usijaribu kusaka tiba mbadala kwa sasa, kapime itakusaidia na hata kama itakuwa ni mzio (allergy) basi itakuwa ni wasaa wa wewe kutambua nini unywe na kwa namna gani.

Atakuja dokta Riwa hapa na wengine wanaweza kusema kwa utaalam zaidi, mm ni mkunga
 
It is a sign of syphilis my friend. You have to see the doctor immediately.
 
Sijaoa na last time 2 have sex ilikua ferbuary this year, ilishawahi kunitokea mara moja kikakaa wiki moja na nusu hadi ikakauka but it was 3 years ago

woow.....jaribu kwenda kufaya vipimo hospitali.......magonjwa ya zinaa sio lazima uambukizwe kwa kufaya ngono.....
 
woow.....jaribu kwenda kufaya vipimo hospitali.......magonjwa ya zinaa sio lazima uambukizwe kwa kufaya ngono.....

Kutumia choo kischosafishwa (hygienic), mate- kudendana kulikopitiliza!!!!, kuchangia nguo za ndani na zile za bafuni(towel)
 
yanaweza kuwa magonjwa ya zinaa.lakini alergy ya sulphur ni mbaya sana kwa wanaume.inaweza kuku unguza kabisa eneo hilo
 
inaweza ikawa Neoplasia.

Ni kweli allergy ya sulphur ni mbaya na inaweza kuunguza na hasa inapojitokeza maeneo yenye ngozi laini na ambayo mara nyingi huwa tunayaficha kwa nguo zaidi ya moja.

inaweza pia kuwa ni neoplasia (unusuall swelling in or on the body), ni vizuri akaenda kupima na kuangalia kama kuna vijinya vinajitokeza na kuleta huwa uvimbe/vipele vigumu
 
Kama walivyokushauri wana jf hapo kuna dalili za magonjwa ya zinaa.Kubwa hapo vunja ukimya kamuone dokta kwavipimo then utakuwa ktk safe side.Mficha maradhi....,kwakuja jf utapona umepata michango na ushauri murua kwa hatua za kumaliza maradhi hayo.
 
Ilianza na kasehemu kadogo kuwasha then kuanza vipele vidogo, now vimekua kama kidonda ingawa ni kasehem kadogo ka uume, haviumi sana. Kuna dokta jiran nilimuonyesha nikamwambia last j'mosi nilikunywa mitakelfin n 4rm j3 ndo vipele vikaanza. Akaniambia nitakua nina alegy na dawa zenye sulphur akanipa vidonge vimeandkwa cosmos. Bt bado hali iko vile vile. Naomba Ushauri jf doctor

vinawasha? au havina maumivu yeyote?, vinajitokeza katika uume tu au hata mdomoni juu na chini?. nitajie urefu wako katika sentimita na uzito wako ktk kg. www.maajabuyamaji2.artisteer.net
 
Vilianza na kuwasha ila now haviwashi vimetengeneza kidonda kama ngozi iliyoungua na moto na nikijigonga kwenye mapaja au boxer ndo kuna maumivu
 
Back
Top Bottom