Kutoka kwa legend Edo Kumwembe

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
"Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF ! Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama wangefika nusu fainali wangeweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

-Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchini mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani. Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

-Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA! Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Ila kuna muda ukiwa maskini kila kitu utahisi unaonewa tu pamoja na bashasha la kwenda kutwaa ubingwa wa NBC Premium wale wenzangu na Mimi lakini linapokuja swala la TotalEnergies CAF Champions League & Confederation Cup basi wanajikuta wanyonge sana yani pamoja na kuwa mabingwa mara 27 lakini kule CAF ni kama watoto changa
Kuna namna tu hii Post inatia hasira, kuna namna tu wakisoma watekereka sana wengine utasikia wanasema "Edo tunamjua yule ni wa mchongo tu, ni simba pure"

By the way ukweli utasimama tu Simba SC Tanzania sio wajukuu wa CAF Bali ni ubora walioonyesha kule na nyie mkienda next season tunawaomba fanyeni kweli msituangushe

Yanga haina muda wa kusikiliza porojo kutoka kwa hao wachambuzi uchwara. Nguvu kubwa kwa sasa imewekezwa kwenye kuchukua mataji yote msimu huu. Tulianza na Ngao ya Jamii, na sasa tunakaribia kuchukua Kombe la Ligi kuu Bara, na pia lile la Shirikisho la Azam.

Baada ya hapo ndiyo tutahamishia nguvu zetu kwenye mashindano ya Kimataifa.
 
Mapinduzi hamchukui?
 
Kwa msimu wa 2022/2023 simba ni ya 14
IMG_20220524_161011.jpg
 
hivi bado tu kuna huu mjadala wa ipi timu kubwa kati ya Simba na Yanga? Yanga ni underdog full stop, tusipoteze sana muda kwa suala lililowazi hata alieko Misri, Morocco, Congo, South Africa, Niger, Nigeria na kwingineko wanajua Simba ni habari nyingine!!!
Tunashindwa kuzifikisha timu zetu mbali medani za kimataifa kwa ushabiki usio na tija kama huu. Ilipaswa timu zetu zitakazoshiriki kimataifa msimu ujao kwenye suala la kusonga mbele kimataifa, zijifunze kwa kaka yao Simba anafaulu vipi ili nao waweze kufika mbali kwani kwa kufika kwao mbali kunaleta heshima kwa nchi na vilabu vyao binafsi. badala ya kuendeleza mijadala isiyo na afya na kujichosha bure kwa vitu vilivyowazi tuwekeze zaidi kwenye maandalizi ya safari za kimataifa
 
"Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF ! Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama wangefika nusu fainali wangeweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

-Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchini mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani. Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

-Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA! Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Ila kuna muda ukiwa maskini kila kitu utahisi unaonewa tu pamoja na bashasha la kwenda kutwaa ubingwa wa NBC Premium wale wenzangu na Mimi lakini linapokuja swala la TotalEnergies CAF Champions League & Confederation Cup basi wanajikuta wanyonge sana yani pamoja na kuwa mabingwa mara 27 lakini kule CAF ni kama watoto changa
Kuna namna tu hii Post inatia hasira, kuna namna tu wakisoma watekereka sana wengine utasikia wanasema "Edo tunamjua yule ni wa mchongo tu, ni simba pure"

By the way ukweli utasimama tu Simba SC Tanzania sio wajukuu wa CAF Bali ni ubora walioonyesha kule na nyie mkienda next season tunawaomba fanyeni kweli msituangushe

😁😁😁😄😄😄😄
 
Kwani ngao ya jamii ni kombe? Maana umelihesabu kwenye makombe yenu.

Bora mapinduzi ni kombe kabisa tofauti na ngao unapewa ubao tu ulioandikwa ngao ya jamii.
Umeona kwenye maelezo yangu nimeitaja hiyo Ngao ya Jamii kama Kombe?
 
Back
Top Bottom