Kutoka kwa Askofu Bagonza (Phd)

Pili Romwad

Member
Nov 10, 2018
22
23
Falsafa za Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
__________
Tumemaliza hatua ya kutia nia. Sasa ni kuchukua fomu. Utafuata uteuzi. Mawili yamejitokeza katika utiaji nia na uchukuaji fomu.

Kuna utitiri wa watia nia katika chama tawala na ukame wa watia nia vyama vingine. Kuna sura zisizozoeleka katika siasa. Ni kama kuku wageni wenye kamba miguuni. Wengine wanachomekea mashati yasiyochomekewa.

Historia imewekwa, tuliodhani hawana vyama, tumegundua wana vyama: maaskofu, wana usalama, watumishi wa vyombo vya utoaji haki mpaka watumishi wa tume ya uchaguzi. Tusijidanganye tena kuwa viapo vinafuta itikadi, dini, kabila na urafiki! Madhara yake watajua wajukuu.

Kwa nini utitiri chama tawala? Sababu zaweza kuwa nyingi. Nimesikia mbili zikitajwa na wengi:

1. Chama kinafunika mengi. Mgombea unakuwa salama ktk biashara, kodi, uraia, ajira, uteuzi, kura hewa, ulinzi, na hata mahakamani. Unakuwa salama kabla, wakati na baada ya kugombea. Haya yote tumeyashika tangu utoto ila safari hii hata waliovaa shati la kijani juu ya gwanda wametia nia!! Tutaisoma namba na herufi.

2. Kugombea kupitia chama hiki si lazima ufanye lolote ukiishachaguliwa. Serikali itafanya. Useme usiseme, serikali ipo. Wewe tulia na ule nchi kwa miaka mitano. Kusemasema si vizuri wakati wa kula. Hiyo ni kazi ya wasio na chakula.

Kwa nini kuna ukame wa wagombea katika vyama vingine? Nimesikia mbili zikisemwa na wengi kati ya nyingi:

1. Hawatapitishwa na tume kugombea. Fomu zitachafuliwa. Wafuasi wao watazuiwa kupiga kura. Wakijitokeza vituoni watazuiwa. Wakilalamika watakamatwa. Wakipiga kura hazitahesabiwa.Zikihesabiwa hazitatangazwa. Ni utitiri wa visa.

2. Kugombea kupitia upinzani ni maisha ya roho mkononi kila wakati. Kufutiwa uraia, kubambikiwa kesi, kufilisiwa, kutekwa, kujeruhiwa, kuuawa, na kuteswa kisaikolojia. Ni utitiri wa visa na hofu. Unashika fomu ya kugombea mkono mmoja na mkono wa pili unaandika wosia.

Haishangazi wagombea wengi wa upinzani ni kina mama (mashujaa wa nchi waliosahauliwa na historia). Kina mama ni jasiri. Kila nyuma ya mwanamme aliyefanikiwa kuna mama lakini si kila nyuma ya mama aliyefanikiwa kuna mume! Hilo ni somo jingine kwa siku nyingine. Muda si mrefu, wanaume tutagombea viti maalumu.

Jamani eh!! Maisha ni siasa na siasa ni maisha. Usiposhiriki siasa utashirikishwa bila kutaka. Hata maiti inashiriki siasa ndo maana kuna Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi.

Nina tatizo moja tu. Mnaogombea litatueni mpate kura yangu. Madhara ya siasa mbaya hayabagui, daima mkumbuke kuna maisha baada ya siasa. Kuna watu tulikuwa haturuhusiwi kula mpaka wafike kwanza, leo hii tunawaambia waondoke kwanza ndio tule.!
 
Lumumba lazima wakushambulie Baba Askofu . Kwao ni kusifu na kuabudu . Hata ukiwasikia hao utitiri wa watia nia ni kusifu na kuabudu. Nothing else
 
Kuna muda natamani kurudi shule halafu kuna muda naona ni kupoteza muda tu

Watu kama Baba Askofu Bagonza, Prof Assad watanifanya nirudi shule

Mzee amebobea kwenye Falsafa,

Kusimamia ukweli iwe mchana iwe usiku

Heshima kwenu Wazee wangu
 
Back
Top Bottom