Kumekucha baada ya hekaheka za jana huku macho na masikio yakiendelea kutosadiki yanayotarajiwa kujiri hasa baada ya kigugumizi kuwatawala wanaokusudiwa kufunguwa midomo yao kupaza sauti itakayokata mzizi wa fitna na kufungua ukurasa mpya wa historia ya uwajibikaji katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Kwa ujumla wabunge wanaoonekana kuranda hapa katika viwanja vya bunge ni wachache saana, sijui wengine wako wapi na ORDER PAPER haionyeshi kama PM kapangiwa kusema jambo licha ya kuwa yeye a kama mtendaji mkuu wa serikali hawajibiki kufanya hivyo kwani wakati wowote anaohitaji kutoa taarifa kwa maelekezo na mwasiliano na Spika anaweza kufanya hivyo.
Tafakuri ni zito, na muda punde Bunge litaanza
Upande anaopitia PM ulinzi upo kuashiria anakuja na muda wowote atafika hapa mjengoni
Yapi yatajiri, Endelea kubaki JF
UPDATES: HOFU YANGU YA KUTOWAONA WABUNGE ILIKUWA SAHIHI
PM ana mjadala Mkali tena, Sitashangaa Maamuzi haya yakachakachuliwa Vibaya na zikazuka Hadithi mpya kabisa ambazo zitasononesha Vibaya mioyo ya Watanzania waliokwishajawa na dukuduku la kujua hatima ya Mawaziri wanaotuhumiwa kwa kutafuna mali ya UMMA na kukosa uwajibikaji.
Tunasaka DETAILS ZAIDI
UPDATES:
Muongozo Ulioombwa ni kutaka Ufafanuzi wa Serikali kwa nini haijatoa Tamko lolote wakati Nchi ipo katika sintofahamu zito na wananchi hawajui hatima ya Mawaziri wanaodaiwa kukaa Kujiuzuru. Naomba Muongozo wako Mh. Spika
KAUMINYA PENGINE ANATAKA USHAURI NINI ASEME ILA ATASEMA TU MAANA NDO KINACHOFUATA YEYE KUULIZWA BAADA YA MAJUMUISHO YA HOJA ZA KAMATI
RECENTLY: PM AMEINGIA MJENGONI NA LOTS OFKABRASHA....Ngoja Tuone
UPDATE: MEDIA zimetega anapotokea PM kwa shauku ya aina yake, ataingia mitini kamajana au atatoa neno?????
Hon Mbowe: Anasisitiza kutojikita katika kujadili matatizo ya Taarifa za kamati na kuwa mchango wake leo utalenga katika kutoa mawazo yake ili kuondoka katika dilema hiyo
Mfumo mbovu wa kurundika madaraka makubwa kwa mawaziri ndio chanzo hata kama tutabadilisha mawaziri leo bila kuwapunguzia madaraka waliyonayo tatizo litarejea tena.
Lawama kati ya watendaji hazitakwisha kama mfumo uliopo wa kurundika mayai yote katika kapu moja hautabadilika
Tuunde mfumo wa kugawa haya madaraka
Waziri hawezi kusimamia madini na rasilimali zote nchi nzima au kilimo
Katiba mpya iangalie jinsi gani tunadecentralize madaraka
kila mmoja anangojea serikali kuu itende, uzembe wa waziri mmoja unaweza kulisababishia serikali mgogoro mkubwa
Naendelea kuamini kuwa wabunge sasa wanafanya kazi waloagizwa na wananchi wao. Mungu na awape nguvu zaidi na kuyaondoa makandokando yote yanayowazunguka
Mbowe anawahamsisha watanzania wote viongozi wa Dini, vyama vya siasa na wadau wote katika mchakato wa katiba kuifikiria kwa kina Hoja ya Serikali za Majimbo na DECENTRALIZATION ndio utakuwa ufumbuzi wa matatizo haya ya watanzania, hata kama mabadiliko ya mawaziri yatafanyika bila kubadili mfumo huu ambao CDM imeshatoa mwelekeo katika sera yake ya MAJIMBO hakuna mabadiliko yatakayotokea