Anashangaa mpaka sasa Ngeleja ni waziri!
jamani hakuna mtu mwenye link online?? Msaada pse
anabwabwaja wapi?
Kuropoka kwa Makinda ndio chanzo.Kigola anaomba umeme na kumpongeza Ngeleja sijui kwa lipi huku analalamikia Giza na
anakiri kuwa suala la TRANSFOMA ni CRITICAL Problem
Spika Makinda to Mbowe "una bahati Jambazi lako limekuwahi kuomba mwongozo sivyo ungekosa nafasi" Mnyika aliomba mwongozo kabla ya Mbowe kuongea
Sio Kange ni Kigola naomba urekebishe.
Kuropoka kwa Makinda ndio chanzo.
Leo anafyatuka tu kashamwita Myika Jambazi, ila tumemuweka kiporo kwa hilo maana halina tija sana leo
Saalaaaaam
Kumekucha baada ya hekaheka za jana huku macho na masikio yakiendelea kutosadiki yanayotarajiwa kujiri hasa baada ya kigugumizi kuwatawala wanaokusudiwa kufunguwa midomo yao kupaza sauti itakayokata mzizi wa fitna na kufungua ukurasa mpya wa historia ya uwajibikaji katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Kwa ujumla wabunge wanaoonekana kuranda hapa katika viwanja vya bunge ni wachache saana, sijui wengine wako wapi na ORDER PAPER haionyeshi kama PM kapangiwa kusema jambo licha ya kuwa yeye a kama mtendaji mkuu wa serikali hawajibiki kufanya hivyo kwani wakati wowote anaohitaji kutoa taarifa kwa maelekezo na mwasiliano na Spika anaweza kufanya hivyo.
Tafakuri ni zito, na muda punde Bunge litaanza
Upande anaopitia PM ulinzi upo kuashiria anakuja na muda wowote atafika hapa mjengoni
Yapi yatajiri, Endelea kubaki JF
ADIOS