Kutoa nyongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoa nyongo

Discussion in 'JF Doctor' started by snochet, Aug 8, 2011.

 1. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  eti wadau,nina haka kaswali kangu kadogo,kuna watu wana katabia ka kuchokonoa koo hasa wakiwa wanapiga mswaki,ivi hii kitu ina madhara kiafya?
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  njia nzuri zaidi ya kutuliza nyongo ni kunywa glasi mbili za maji ya vuguvugu asubuhi nusu saa kabla ya kula kitu chochote au kunywa nusu kikombe cha aloe vera(shubiri) asubuhi ukiamka na usiku nusu saa kabla ya kula.
   
 3. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  nimekusoma,lakini je kutoa huko kwa nyongo kuna madhara yoyote kiafya?
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sijui mnamaanisha nini mkisema 'kutoa nyongo', lakini kama mnazungumzia nyongo ninayoijua mimi kisayansi...haitolewi kwa mswaki wa koo wala kunywa maji ya vugu vugu!

  Nyongo (bile) inahifadhiwa kwenye mfuko maalum tumboni (gall bladder) ambao umejishikiza karibu na ini tumboni huko. Una kimrija (bile duct) ambacho kinaconnect na utumbo mdogo sehemu inayoitwa duodenum, hivyo nyongo humwagwa kwenye utumbo mdogo ambapo husaidia kwenye umeng'enyuaji wa vyakula vyenye asili ya mafuta (emulsification of fat), ziada iantoka kwenye haja kubwa (ndiyo inayoipa haja kubwa rangi ya kimanjano au brownish).

  Sasa hicho mnachoongelea hapo hakina uhusiano wowote na nyongo. unapochokonoa koo na mswaki unapata 'gag reflex' (ile kama unataka kutapika) ambacho sio kitu kizuri...pia koo lina ngozi laini hivyo waweza lichubua, na kwa sababu mdomo ni mchafu (kuna bacteria hata ukipiga mswaki mara kumi kwa siku), wale bacteria wanaweza ingia kupitia kidonda na hivyo kupata infection ya tonsils (Tonsilitis), na mbaya zaidi infection inaweza fikia kwenye moyo (especially kwa watu wenye matatizo ya moyoy already) ukapata tatizo la hatari linaloitwa 'bacterial endocarditis'.

  Kuchokonoa koo hakuna faida yeyote.
   
 5. K

  Karry JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  thanx kwa ufafanuzi huu makini
   
 6. i

  igwe sr. Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  duh umetufahamisha,wengi tulikuwa tunajua unatoa nyongo kwa staili hyo ya kupiga mswaki kwenye koo
   
Loading...