Kutoa Kadi ya Mualiko

Kutoa Kadi ya Mualiko

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
969
Reaction score
3,065
Kuna Rafiki yangu ana owa kesho.

Ametoa Kadi za Mualiko. Sasa Kuna Baadhi ya Rafiki Zetu wanasema angetoa hata kadi za mchango.
Naomba ufafanuzi wenu kwani kutoa Kadi za Mualiko au Kuto kuomba watu michango ya kuendeshea shunghuli yako unaweza athiri Jamii au Rafiki zako.

Kwa mtazamo wangu nimeona ni Jambo la kawaida tu, maana ni maamuzi ya mtu.

Ila Kuna mtu mmoja yeye analalama kua Bora tungechangishwa, kuliko kwenda kula na kunywa Bure.
Mi nimeletewa Kadi ila kwa kesho Ratiba yangu ni ngumu kwenda kwenye hiyo Harusi.

Sasa Hawa waendaji povu linawatoka.
 
Nibora kafanya hivyo kuepuka vijimaneno maneno na manung'uniko ya waja
Amejiepusha na mengi
 
Hapo ni kwenda na zawadi tu...ila wabongo sasa anakula anakunywa anacheza kidancee alafu anakuzawadia Thermos ya afu kumi na mbili 😂😂😂
 
Watu ni wanafiq tu ukiwapa hizo card hawachangi ikiwa kweli mtu alikuwa na moyo wa kumpongeza mwanae kwa kuoa apokee kadi ahudhurie sherehe kile alidhani angemchangia ampelekee ukumbini kama zawadi.

Lakini utakuta yanaenda yanakula na hayatoi hata cent.
 
Hataki mchango ambao kikawaida una limitation ya kiasi utakachotoa,anataka muende kwa hiari yenu kisha wakati mnatoa zawadi awakazie.
Kama huna laki mfukoni usikimbilie nyama.
 
Back
Top Bottom