Kutoa container bandarini

svc

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
429
157
Kuna yeyote mwenye experience ya kutoa mzigo bandarini ndani ya siku 21 bila ya kuanza kulipa gharama za ziada za daily storage fees kwa makampuni binafsi kama Azam?

Experience yangu inaonyesha clearing & forwarding agents hawawezi kutoa mzigo chini ya siku 21, hata uwe umewakilisha documents zote mapema kabla meli haijatia nanga bandarini, na una fedha za kutosha kulipia kodi za TRA na gharama nyingine zote wakati process ya kutoa mzigo inaendelea.

Lazima itazidi siku 21 ili watu kama Bakhresa na wengineo wenye container yards binafsi wadai thousands of dollars in unnecessary storage fees na upuuzi mwingine.

Nadhani kuna ushirikiano kati ya clearing agents, customs na kampuni binafsi zinazomiliki container yards kuchelewesha mzigo ya wateja makusudi ili watozwe gharama kubwa za storage, ku-move container ndani ya yard na kuliweka chini ili lipakuliwe, na gharama lukuki wanazotoza.
 
Ndugu! Mimi nimeweza kulitoa pale AMI, lakini OMG! NI usumbufu, kuna gharama za ajabu, actually nipo ninaziweka sawa ili walau nijulishe wadau kuwa hizi gharama zinazolipwa kwa watu binafsi is a hell of money. Serikali inachukua fungu dogo, but the rest inakwenda mikononi mwa wenye maeneo, na pengine pasipo lazima sana. Sikuwahi kujua mtu kufungua na just kukagua container moja anakutoza about US$ 90! Hii inafanyika within 5minutes hasa kama ni mzigo mmoja kama gari
 
Ni balaa tupu mkuu!

Kwa kweli inasikitisha sana, tena sana!

Umewasilisha shipping docs zote well in advance kabla meli haijaingia, unapewa 21 days grace period, lakini mzigo hautoki hadi baada ya wiki moja au mbili baada ya grace period kumalizika.

Wanachofanya wanapeleka mzigo wako mara moja kwenye yard binafsi baada ya kupakua kutoka kwenye meli, kitu ambacho kilikuwa hakipo pale zamani.

Azam na AMI wanachaji hata kusogeza container kwenye yard yao wenyewe ili likaguliwe, achilia mbali storage fees za hadi $80 kwa siku kwa container la futi 40, na haijalishi kama ni Jumamosi au Jumapili.

Hivi tutapona kweli?
 
Back
Top Bottom