Kutimiza Masharti ya Microfinance Act 2018

Kutimiza Masharti ya Microfinance Act 2018

Joined
Dec 12, 2019
Posts
9
Reaction score
7
Sheria ya kuendesha, kusimamia na kudhibiti microfinance institutions zile ambazo haziruhusiwi kupokea wala kutunza akiba/amana za umma tayari inafanya kazi.

Serikali kupitia wizara ya fedha tayari imeshatunga kanuni za uendeshaji, ambapo ilitoa kipindi cha mwaka mmoja kutoka 1st November 2019 hadi 30th October 2020, taasisi zote kuzingatia matakwa ya sheria mpya.

Ni mambo mengi sana yanahitajika kurekebishwa na asasi nyingi ambazo zaidi ya 95% zilianzishwa kiholela bila weledi kwa lengo tu la ''kupiga hela''. Sasa sheria imekuja kwa ajili ya kumlinda mlaji pia kuzilinda hizo taasisi.

Mchakato huu wa kubadilika kutoka kuwa asasi ya isiyosimamiwa na mamlaka yoyote hadi kufika ngazi ya kukubalika na wasimamizi (Benki Kuu) sio jambo la kitoto. Inahitaji weledi, uzoefu na uzeefu katika tasnia hii kuandaa hayo yote na hatimaye kupewa leseni (kibali) na Benki Kuu.
 
Back
Top Bottom