Kuteta kwa lugha ngeni, maana yake nini?

mrumi

Member
Jan 12, 2016
31
24
Kuna baadhi ya watu wana kasumba ya kuteta kwa lugha isiyofahamika vizuri na wote katikati ya mazungumzo ya kundi lenye mchanganyiko wa watu.

Nataka kusema kwamba, wakati fulani mnaweza mkawa kwenye kundi la watu watatu au zaidi mnafanya mazungumzo ya kawaida kabisa, na lugha inayowaunganisha na kufahamika na wote ni kiswahili . Lakini inaweza kutokea, kwa mfano, watu wawili au watatu kwenye lile kundi, kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanachomekea lugha ngeni, labda tuseme wanaanza kuongea lugha ya kabila lao huku wakijua wazi kwamba kwenye lile kundi kuna ambao hawaelewi lugha wanayoongea, baadaye wanaendelea tena na kiswahili. Hali ni hiyo hiyo pia kwa wale waliobahatika kufahamu kidogo lugha fulani ya kigeni hasa Kingereza.

Binafsi nachukizwa mno na kasumba hii. Naitazama kama kiashiria cha majivuno na dharau, na inalenga kuumiza hisia za mtu mwingine.

Una maoni gani kuhusiana na jambo hili! Je, nakosea kufikiri namna hiyo? Lengo la kufanya hivyo ni nini hasa? 2
 
kwa kweli huwa inakera sana, nakumbuka siku moja nimepewa lift na rafiki angu mmoja yeye ni kondakta wa costa za ruti flan, tukawa tumepakia watoto flan wa shule ya girls ilikuwa msimu wa likizo. Wale watoto wakaanza kashfa kwa mshkaji wakati wa kudai nauli walikuwa wanaongea kingereza. Yaani bila kujua jamaa anaelimu gan, kumbe jamaa anamastaz so aliwaelewa vizuri sana na busara zikamwongoza. ustaarabu ni kitu cha bure kwakweli.
 
Back
Top Bottom