Umri ni miaka 30 wake 24.
UMRI WAKE UNAFAA KUOLEWA, MNAENDANA
1. Nilimpenda kwa hisia kabisaaa but sasa imekuwa tuko kwa mazoea tu ule msukumo wa mapenzi kutoka ndani umekata kabisa.
SABABU ZA KUISHIWA HISIA NI NYINGI, KWANZA UMESHAMJUA SANA, MNA MTOTO PIA ANAYEGAWA MAPENZI YENU. KWA HIYO HII SI SABABU YA KUMWACHA . NDOA NYINGI TUNAISHI VIZURI TUU KWA AKILI, NA SIO HISIA . . KWA KUWA BAADA YA KUONA, MKAZAA NA KUONGEZA MAJUKUMU, LAZIMA MABADILIKO YA KIHISIA YATOKEE . . BADO ANAFAA KUWA MKE . .
2.Naweza sema vimepungua cse mahitaji na nyakati haviko sambamba. Matarajio yangu kwake ni kama hayapo maana ujuavyo mke au mume anatakiwa kuwa multipurpose maana ndoa ni zaidi ya kuwa watoto na kulala pamoja.
WEWE INAELEKEA HUJUI MAJUKUMU YA MUME, NDIO MAANA UNATAKA MKE MULTIPURPOSE . . KWANZA UNAISHI NAE KIMAKOSA KABISA, HUJAFUNDISHWA MAANA YA NDOA NA MAJUKUMU YAKO, WEWE UNAISHI KWA HISIA TUU . . INAELEKEA UNATAKA KUTUNZWA NA MKE, KUMBE WEWE NDIE UNATAKIWA KUMTUNZA MKE WAKO NA WATOTO WAKO. UNATAKIWA KUMFUNDISHA YOTE JINSI UNAVYOTAKA AWE, SIO KUMKIMBIA . . OMBA USHAURI ZAIDI KWA WATU WAZIMA WENYE NDOA ZAO IMARA KABLA HUJAMWACHA, MIMI SIONI KOSA LAKE . .
3.Nadhani natakiwakiwa kuwa selective zaidi kupata yule ambaye ataweza kuwa multipurpose kwa angalau hata 75% ili nami niweze kufurahia mahusiano kuliko ilivyo sasa maana najikuta kama nipo mwenyewe kuanzia ushauri, financially na mengineyo na imefikia wakati naona ni bora kuwa single kuliko kuonekana upo na mtu kwenye macho ya watu wakati nafsi ipo single.
TATIZO UNALO WEWE, HUYO BINTI KAMA AMEWEZA KUKUPIKIA, KUKUFULIA, KUKUTUNZIA MTOTO, KUBEBA MADHAIFU YAKO, KUISHI NA WEWE AKIPENDA NDUGU ZAKO, BASI ANAFAA KUWA MKE.
JICHUNGUZE WEWE ZAIDI KAMA UNAFAA KUWA MUME NA BABA BORA . .
4. Mtoto ni wangu. Naamini naweza pata kitu kizuri zaidi na mtoto tayari ninaye. Usalama naona utakuwepo maana hata kama sitapata kizuri zaidi lkn nitakuwa single na furaha kuliko kuendelea na hii unhappy relationship.
MLIFANYA MAKOSA KUISHI PAMOJA KABLA YA KUONA, NYIE NI MKE NA MUME SIO WACHUMBA TENA . . UNGEOA RASMI, USINGEKUJA HAPA NA HADITHI ZA HISIA . . KUOA NI KAZI YA WANAUME, SIO WAVULANA . .
WEWE NI SELFISH MAN . . HUYO MWANAMKE ANAFAA KUWA MKE, SIJAONA SABABU YOYOTE YA MAANA ULIYOTAJA INAYO M DISQUALIFY KUWA MKE WAKO
5. Sihisi kushindwa kummudu ila ninaona kuendelea naye ni kuja kukosa ile support ya mke ambayo mimi naitarajia kutoka kwake kwani naanza kuyaona hayo mapema.
6.Bado sijazunguza naye kuhusu kuachana na bado napata wakati mgumu kulieleza hilo kutokana na sababu nilizozieleza kwenye mada. But yeye pia ameanza kuona tofauti kwangu maana ki ukweli nimepoteza furaha kabisa kwenye hii relationship.
Ushauri wako tafadhali.
ANGALIE USIJE KUJUTA KIJANA, HAKUNA MKE MALAIKA HUKO UNAKOTAKA KWENDA KUCHAGUA MKE MWINGINE. PIMA RISK YA UNALOTAKA KUFANYA, JICHUNGUZE WEWE ZAIDI KAMA UNAFAA KUWA MUME NA BABA BORA, HALAFU PATA USHAURI TOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU.
ACHA KUISHI KWA HISIA, ANZA KUISHI SASA . . , LIFE IS REAL !
Sent using
Jamii Forums mobile app