Kuteleza sio kuanguka

Kuteleza sio kuanguka

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
355
Reaction score
701
Ilikuwa ni asubuhi tulivu wanafunzi wote tumekusanyika parade kwa ajili ya kupata maelekezo na taratibu za shule

shule yetu ilikuwa na utaratibu wa kufanya presentation ya masomo kwenye pared ya wanafunzi.

Mara baada ya taratibu za shule kukamilika , ikawa ni zamu ya darasa letu kufanya presentation.

Kwakuwa hatukuwa na zamu au ratiba nani afanye presentation lini na kitu gani? Ili kuwa inapofika zamu mmoja kati yenu anasimama na kufanya presentation.

Siku hiyo mara baada ya darasa ketu kutangazwa na mwalimu hakukuwa na mwanfunzi ambaye alitaka kusimama kufanya presentation

Moyoni mwangu ukaingiwa ujasiri ndani yangu wa kusimama na kufanya presentation

Nikasimama nikapanda kwenye eneo la kufanyia presentation, ambalo lilikuwa juu unaona wanafunzi wote wa shule nzima kama wanafunzi 1000.

Nilisimama nikajitambulisha nikaanza kufanya presentation, nilianza vizuri na kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya watu tena shule nzima kufanya presentation na sikuwa na uzoefu wowote wa kuongea mbele za watu

Ghafla maneno yakaanza kunipotea sikuwa na chakuongea , mwalimu akaniuliza umemaliza? nikamjibu ndio kwa kuwa sikuwa na chakuongea

Mwalimu alikasirika sana maana presentation ilikuwa ya dk 5 nimezungumza chini ya dk1 na hakuna kilichokuwa cha maana zaidi ya utambulisho

Siku hiyo darasa letu wote tulikula fimbo kila mmoja, kwangu mimi nilijiskia vibaya sana na tangia siku hiyo ilijenga hofu kuu ndani yangu

Ujasiri ambao nilikuwa nao ulipotea, nikakosa ujasiri wa kusimama mbele za watu kuzungumza

Nilichojifunza kuto kujaribu kufanya majaribu ya silaa wakati wa vita

Kitendo cha kufanya presentation mbele ya wanafunzi 1000 wakati sikuwai kufanya hata kwa wanafunzi 20 kiliweza kuua ujasiri mdogo niliokuwa nao

Nilijifunza ili uweze kuwa mwongeaje mbele za watu ziko kanuni za kuzingatia kufanya ili uweze kuwa mzungumzaji mbele za watu

Nilijifunza kufanya mazoezi ya kuongea mwenyewe, na kumwomba Mungu anisaidie kunipa ujasiri

Kuongea mbele za watu alikuwa jambo la kawaida kwangu, lilichukua miaka mingi sana kuweza kusimama mbele za watu

Sio kwamba ni kiti kigumu hapana , ila inategemea na mazingira uliyokulia

Shule uliyosomea na mazingira yanayokuzunguka yanachangia kwa kiasi kuwa mzungumzaji mzuri au laa

Jitihada nilizofanya nilijua huko mbeleni ninatakiwa kusimama kuongea mbele za watu

Nilijaribu kuondoa hofu ndani ya moyo wangu kwa tafuta kila haina ya hofu ndani yangu nakuipatia majawabu

Nilijifunza kufanya maandalizi mapema kabla ya kufanya presentation mbele za watu

Nilijifunza ukitaka kuongea vizuri mbele za watu kutokukalili kile ambacho unataka kukiongea bali ukielewe maana ukikielewa kitu hata kama maneni yatakosekana ila utapata maneno mbadala ya kuwasilisha mada yako

Kuondoa hofu ya watazamaji , nilijifunza ili niweze kuwa muongeaji mzuri naitaji kutokuwaangalia watu sana machoni yaani eye to eye contact bali kuwaangalia pasipo kuweka focus, ukiweka focus kwa watu utapoteza focus ya kuzungumza

Nilijifunza kuomba msaada wa Mungu kabla ya kuongea ili ninaposahau nipate msaada kutoka juu

Wazungu wanasema Practice make Parfect , kadri unavyojaribu kuongea ndivyo unavyozidi kuwa mwongeaji mzuri, nilijifunza kuongea mara kwa mara ili kuboresha uwezo wangu wa kuongea mbele za watu.

Nikijifunza kupitia wale ambao wanafundisha mbinu za kuongea mbele za watu , ghafla uwezo wangu ukaanza kubadirika kidogo kidogo.

Bado naendelea kujifunza, na siku zote nimekuwa mwanafunzi.

Uhauwezi kuwa mzugumzaji mzuri pasipo kufanya mazoezi ya kuzungumza, na hauwezi kuwa mchekeshaji mzuri kama ujifunzi namna ya kufanya watu wacheke

Siku mmoja nilipewa kazi ya kufanya presentation mbele ya viongozi wakubwa tu, siku hiyo nilikumbuka nilikotoka na kukumbuka kile kitendo cha kushindwa kuzungumza mbele ya wanafunzi wangu ilikuwa tu ishara yakwamba natakiwa kujifunza kuzungumza mbele ya watu kwa sababu itakuwa shehemu ya maisha yangu

Leo hii liletukio linanikumbusha kwamba kila kitu kinatokea kwa sababu, ila usijaribu kufanya kitu ambacho ujawai kufanya siku ya vita fanya maandalizi mapema usijekuhaibika.
 
Back
Top Bottom