Ndugu zangu wanaJF napenda kuwafaamisha ya kwamba najiondoa kwenye Kijiji chetu hiki kwenda kutafuta maisha mapya huko Mjini.Nimeamua kujiondoa kutokana na kile ambacho kwa upande wangu nimeona kama ni kunyimwa haki yangu ya msingi hapa kwenye hiki kijiji cha JF.nimekulia hapa mmenisomesha nyote kwa njia tofauti hivyo basi nimejionea kwakuwa tayari nina elimu mliyonipatia sina budi kwenda kujitafutia maisha sehemu nyingine.Natoa sana shukran zangu kwenu kwa kipindichote tulichokuwa pamoja nilipata ushirikiano mzuri toka kwenu.Mungu hawabariki sana na pia na kiombea Kijiji hiki Amani na Upendo daima!
Ni mimi ndugu yenu
Carthbert C Lyimo