Kutafuta umaarufu kwenye internate kwawamaliza vijana wa wales. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutafuta umaarufu kwenye internate kwawamaliza vijana wa wales.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Oct 29, 2008.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  KUTAFUTA UMAARUFU KWENYE INTERNATE KWAWAMALIZA VIJANA WA WALES.


  Jambo Forum:

  Kizungumkuti cha vijana hawa kujimaliza kimchezo mchezo kiliamzishwa na Dale Crole kijana wa umri wa miaka 18 ambaye alijimaliza kwa kujinyonga katika jumba bovu hapo mnamo Januari 5, 2007.
  Majuma machache baadae katikati ya mwezi wa Februari rafikie ambaye ndiye aliyewapeleka Polisi katika eneo la tukio aitwae David Dilling aliyekuwa na umri wa miaka 19, nae alijiuwa kwa njia ile ile ya kujinyonga.
  Wiki iliyofuata rafiki yao mwingine aitwae Thomas Davies aliyekuwa na umri wa miaka 20 nae akajinyonga. Miezi miwili baadae kijana mwingine aitwae Alan Price aliyekuwa na umri wa miaka 21 na vile vile kama wenzie akajinyonga.
  Miezi kadhaa baadae mnamo Juni rafikie wa karibu aitwae Leigh Jenkins aliyekuwa na umri wa miaka 22 nae akajinyonga chumbani mwa rafikie.
  Kama mchezo vile, mwezi Desemba 2007 wakati wa sherehe za Krismas rafikie na Dale aitwae Liam Clarke aliyekuwa na umri wa miaka 20 nae akajinyonga kama wenzie ikiwa zimepita siku mbili baada ya Krismas.
  Mnamo Januari 5, 2008 wakati wa kumbukumbu za kuadhimisha mwaka mmoja tangu Dale Crole ajinyonge, zafikie mwingine aitwae Gareth Morgan aliyekuwa na umri wa miaka 27 nae akajinyonga nyumbani kwao.
  Mtiririko wa vijana kujinyonga ulioukumba mji wa Bridgend ulioko Wales nchini Uingereza ulianza kuwatisha watu hasa wakazi wa mji huo kwani tangu Dale Crole ajinyonge, na kufuatiwa na wenzie mpaka kufikia hivi karibuni imeshafikia idadi ya vijana 17 ambao wamejinyonga na kuacha simanzi kwa wapendwa wao.
  Baadhi ya wakazi wa mji huo wameelezea hisia zao kuwa mtiririko huo wa vijana kujinyonga sio jambo la kawaida, na limewasitua sana.
  Kwa mujibu wa Takwimu za hivi karibuni zimebainisha kwamba idadi ya watu kujinyonga katika eneo la Wales ni mara mbili ukilinganisha na Uingereza (Wales ni sehemu ya Uingereza ambayo iko chini ya Malkia).
  Hali ni mbaya zaidi katika mji huo wa Bridgend wenye idadi ya watu wapatao 130,000 na ambao umetamalaki kwa umasikini ukilinganisha na miji mingine ya Wales.
  Takwimu zaidi zimebainisha kwamba idadi ya vijana kujiuwa imeongezeka sana majuma ya hivi karibuni.
  Na kila inapotokea kijana mmoja kujinyonga inakuja kugundulika taarifa yake ya kumbukumbu aliyoisambaza kwa wenzake kupitia mtandao wa Inteneti maarufu kwa vijana kusambaza taarifa zao na unaowapa fursa ya kuwa na kurasa zao zinazo wawezesha kufunguwa mijadala na kubadilishana uzoefu.
  Hilo ndilo lengo kuu la waanzilishi wa mtandao huo, lakini siku za karibuni kumeibuka wimbi la vijana katika mji huo wa Bridgend kutumiana salaam za kuagana kabla ya ya kujinyonga. Kwa mfanoMnamo Januari 15, 2007 Binti mmoja aliyepoteza maisha kwa mtindo huo huo wa kujinyonga aitwae Natasha Randall aliyekuwa na umri wa miaka 17 alituma salaam za kumbu kumbu kwenye ukurasa wa mwenzie aliyefariki kwa kujinyonga katika mtandao maarufu wa Bebo akimweleza kuwa atamkumbuka sana, kwa maneno yake mwenyewe aliandika “kwako Clarky, nitakukumbuka sana rafiki yangu, kila wakati kumbuka wakati wetu wa furaha”
  Siku mbili baadae Natasha alijinyonga, na huo ukawa ni mwanzo wa utata mwingine kuhusiana na wimbi hili la vijana wa Ki Welsh kujinyonga.
  Kwani uliibuka mjadala mingoni mwa madaktari kuwa ni vigumu sana kwa wanawake kujiuwa kwa jinsi alivyojiuwa Natasha, wataalam hao wa tiba walibainisha kuwa mara nyingi wanawake hupendelea kujiuwa kwa kunywa sumu na sio kwa kujinyonga kama alivyofanya Natasha.
  Hata hivyo siku iliyofuata rafikie Natasha alijaribu kujinyonga nyumbani kwao lakini kwa bahati nzuri akaokolewa na baba yake akiwa tayari ananing’inia kwenye kamba.
  Wiki mbili baadae binti mwingine aitwae Angelina Fuller aliyekuwa na umri wa miaka 18 nae akajinyonga.
  Idadi hiyo haikuishia hapo kijana mwingine aitwae Nathaniel Pritchard aliyekuwa na umri wa miaka 15 nae akajinyonga hapo mnamo Februari 15, 2007, akifuatiwa kwa masaa machache na kijana mwingine aliyekuwa na umri wa miaka 20 aitwae Kelly Stephenson. Siku nne baadae alifuatia jirani yao aitwae Jenna Parry aliyekuwa na umri wa miaka 16 nae akakutwa akiwa amejinyonga juu ya mti nje ya nyumabani kwao.
  Ndugu jamaa na mararfiki walimiminika na kuweja mauwa na kadi kwenye mti huo aliojinyongea Parry, hata hivyo baadhi ya kadi zilizowekwa ujumbe wake uliwatisha wengi, miongoni mwa kadi hizo iko iliyoandikwa “Niwekee nafasi jirani na wewe” nyingine iliandikwa “uko katika mahali pa usalama zaidi” na nyingine tena ikaandikwa “Tutaonana muda si mrefu, nakupenda sana!” kadi zote hizo hazikuwa zimesainiwa hivyo kuwa vigumu kuwafahamu walioweka kadi hizo pale chini ya ule mti.
  Baadhi ya wananchi nchini humo walianza kuvilaumu vyombo vya habari na hasa magazeti ya udaku kuwa yanahusika na wimbi hilo la vijana kujinyonga kwani vyombo hivyo vimekuwa vikiandika habari za kujinyonga kwa vijana hao katika hali ya ushabiki kiasi cha kuwapa umaarufu wale waliojinyonga.
  Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa Polisi katika mji huo alivilaumu sana vyombo vya habari kwa jinsi walivyoandika habari za kujinyonga kwa Natasha Randall kwa namna ambayo ilichochea vijana wengine kujinyonga ili kujipatia umaarufu hata baada ya kufa.
  Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mji huo waliliangalia jambo hili kwa mkabala tofauti.
  Mkazi mmoja wa mji huo wa Bridgenda aitwae Tracy Roberts alisema si busara kuvilaumu vyombo vya habari.
  Aliendelea kuvitetea vyombo vya habari kuwa ndivyo vilivyoonyesha kuwa kuna tataizo la vijana kujinyonga katika mji huo kwa hiyo si vyema kuvitupia lawama.
  Mama huyo alimpoteza mwanae wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 19 ambye alikufa kwa kujinyonga mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka juzi 2006, hata hivyo mama huyo hakuhusisha kifo cha mwanae na mtiririko wa vijana kujinyonga katika mji huo wa Bridgend.
  Naye Profesa mmoja Saikolojia katika maswala ya kijamii aitwae Arthur Cassidy ambaye anaendesha mtandao wa kuzuia wimbi la vijana kujinyonga katika mji wa Belfast mtandao uitwao Youth-Suicide Intervention group,
  nae aliungana na Tracy kuyatetea magazeti ya udaku akisema kuwa vifo hivyo havikuchangiwa na na magazeti ya udaku.
  “Hatuna ushahidi kuwa magazeti ya udaku yameshiriki kwa njia moja au nyingine kuchochea vijana hawa kujinyonga, kwa kawaida vijana wa siku hizi hawasomi magazeti bali hupata habari kupitia mtandao wa inteneti” Alisema Profesa Cassidy.
  Hata hivyo baadhi ya wataalam wa mambo ya kiuchumi walitafsiri hatua hiyo ya vijana kujimaliza kwa kujinyonga kuwa inatokana na vijana wengi kupoteza matumaini ya maisha baada ya kumaliza masomo kwani mji huo wa Bridgend umezungukwa na umasikini kutokana na kukosekana kwa vyanzo vya ajira hasa kwa vijana wanapomaliza masomo.
  Historia inmaonyesha kuwa mji huo ulikuwa ni eneo la machimbo ya makaa yam awe miaka ya nyuma , hivyo baada ya machimbo hayo kufungwa kumekuwa hakuna chanzo kingine cha ajira mbadala na hivyo vijana wengi katika mji huo kujikuta wakiwa na wakati mgumu mara baada yas kumaliza masomo yao, hivyo kujikuta wakitumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya inteneti.
  Mtoto mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 14 ambaye wazazi wake waliomba jina lake lihifandhiwe alisema kuwa, Inteneti imekuwa ikiwaandaa vijana hawa kujinyonga katika mji huu wa Bridgend, na hata
  Ukingalia vijan wote hao waliojinyonga walikuwa ni wanachama wa mtandao wa Bebo na walikuwa wakitumiana salaam za kumbukumbu katika ukurasa maalum wa kutuma salaam za kumbu kumbu kwa wale waliopoteza wapendwa wao.
  “naamini vijana hawa walikuwa wanafahamiana, na nimetokea kuwafahamu vijana sita miongoni mwa waliofariki kwani nilishawahi kutembelea kurasa zao kwenye mtandao wa inteneti wa Bebo, na walichokuwa wakikizungumzia sidhani kama nitakuja kujihusisha nacho, na sikudhani kuwa watakuja kutekeleza yali waliyoyaandika” alisema kijana huyo aneishi jirani na familia moja iliyopoteza kijana wao kwa mtindo huo huo wa kujinyonga.
  Nae rafikie aitwae George alidai kuwavijana wengi wanachukulia kujinyonga kama fasheni fulani hivi.
  Nao Polisi kwa upande wao wantembelea famili za vijana ambao wametuma taarifa kwenye kurasa zao katika mtandao huo wa Bebo wakiashiria kutaka kujinyonga.
  Hata hivyo wamiliki wa mtandao huo wamekuwa wakitoa baadhi ya taarifa hizo kutoka kwenye mtandao wao.
  Msemaji wa mtandao huo alisema kuwa wamekuwa wakitoa waraka wowote wa kumbukumbu ya kifo au dalili ya mtumaji kuonyesha kuwa huendana yeye akajiuwa, ikiwa tu watakuwa wameombwa na familia ya kijana husika au wameagizwa na mamlaka ya kisheria.
  Mpaka sasa wamiliki wa mtandao huo wa Bebo wanashirikiana na Polisi katika kuchunguza vifo hivyo.
  Hali hiyo haijaukumba mtandao wa Bebo pekee kwani hata mitandao mingine nayo imechukuwa hatua kadhaa katika kuchunguza wimbi hilo la vijana kujinyonga kama linatoakana na inteneti.
  Kwa mfano Mtandao maalum wa intenetiwa kutuma salaam za kumbukumbu za vifo uitwao “GoneTooSoon.co.uk” uliondoa kumbukumbu zilizotumwa kwa vijana wote waliojinyonga katika mji huo wa Bridgend na kisha kuweka taarifa ya kuomba radhi na kufafanua sababu ya kuondoa kumbukumbu hizo.
  Mwanzilishi wa mtandao huo Terry George alisema kuwa antaka kuepuka dalili zozote za kuuhusisha mtandao wake na wimbi la vijana wa Ki Welsh kujinyonga.
  “ ikiwa unajinyonga kwa matumaini kuwa utakuwa mtu maarufu hata baada ya kufa basi hiyo haiwezi kutokea kwenye mtandao wetu, hatuwezi kuruhusu jambo hilo litokee, na lazima kufanyike juhudi za kuzuiya vijana wetu kujiuwa” alisema Terry George.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Habari hii inasikitisha sana....
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Oct 29, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  inasikitisha sana kivipi?
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Sound to be too childish...Huenda ni kutokuwa na responsibilities kwenye family zao...
   
 5. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 680
  Trophy Points: 280
  Umri wa vijana barubaru kutaka kujaribu au kufanya kila jambo. Ukisoma vizuri hiyo taarifa inaoyesha kuwa waliojinyoga walikuwa wanatafuta umaarufu. Umaarufu wa kijinga huo!
   
Loading...