Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,122
RIWAYA; KUTA ZA DARFUR.
NA; BAHATI K MWAMBA.
SIMU; 0656741439/0758573660.
1:
Alikuwa akikatiza katikati ya mitaa ya jiji la Dar Es laam akiwa amening'iniza mfuko kwenye mkono wake wa kulia, mkono wake wa kushoto aliutumbukiza kwenye mfuko wake wa suruali. Alitembea akiwa hana hili wala lile, mawazo yake hayakuwa kwenye mkinzano wowote zaidi ya kupangilia njia atakazopita ili kufika alikokuwa akienda. Alikuwa akipiga mluzi taratibu huku akipishana na watu wengi ambao na wao walikuwa kwenye mizunguko yao ya kila siku, hakuwa na wasiwasi wowote wala hakujali uwepo wake katikati ya jiji.
Hatua zake ndefu zilimfanya aonekane kama mtu aliyekuwa akitembea kwa kasi kubwa, lakini kwake ulikuwa ni mwendo wa kawaida. Alikuwa akikatisha barabara hii na kwenda kutokea kwenye barabara nyingine, alitembea kwa mwendo usioongezeka hadi alipofika mtaa wa msimbazi na mbele yake alikuwa akitazamana na kituo cha mabasi yaendayo kasi. Alitazama kushoto na kulia na aliporidhika na usalama, haraka alivuka barabara na kusimama kwenye kingo iliyokuwa ikitenganisha barabara ya magari yaendayo kasi na barabara ya kawaida ambao alitarajia kuivuka sekunde chache mbele yake, lakini kabla hajavuka, alitazama upande wake wa kushoto ambao ulikuwa na kituo cha bus, kisha alitazama upande wa kulia yalikokuwa yakiingilia magari. Alipohakikisha pande zote zipo shwari alishusha mguu wake kwa nia ya kutaka kuanza safari ya kuvuka barabara ya mwendokasi na kwenda upande wa pili, lakini alijikuta akisita baada ya kuona moshi mdogo ukifuka katikati ya miguu yake huku masikio yake yakinasa sauti ndogo ya mlipuko kutokea sehemu ambayo hakujua.
Alisita kuinua mguu wake kisha kwa utulivu mkubwa aliangalia mbele yake ambako aliamini ndiko risasi iliyotua miguuni mwake ilitokea. Hakuona mtu yeyote wa kumtilia shaka, taratibu aliinua macho yake na kutazama kwenye jengo la ghorofa moja lililokuwa mbele yake, aliishia kuona kamba na nguo zikiwa zimeanikwa huku zikiziba eneo kubwa la madirisha.
“Huyu aliyepiga hii risasi yuko huku chini” Aliwaza huku akianza kumzingatia kila aliyekuwa akikatiza mbele yake.
“Kwa nini hajapiga risasi nyingine kama alikuwa na nia ya kuniua?” Aliwaza huku bado akiwa makini kuzidaka harakati za watu wote waliokuwa wakikatiza mbele yake. Ndani ya dakika moja hakuweza kumuona wa kumtilia shaka, lakini muovu hajifichi hasa akiwa kwenye dhamira mbaya, alimuona.
Macho yake yakiwa yanarandaranda huku na huko ili kuweza kubahatisha yeyote, hatimae yaliweza kunasa sura ya jamaa mmoja aliyekuwa amevaa kofia pana kichwani mwake na koti la baridi.
Alimtilia shaka kwa namna yule bwana alivyokuwa amevaa kwa sababu, ni aghalabu sana kuona mtu kavaa koti la baridi majira ya jioni katikati ya jiji la Dar hasa majira ya kiangazi yenye joto kali, pia alikamilisha mashaka yake kwa namna yule bwana alivyokuwa akiinama kuchagua nguo huku kila mara akikunja shingo yake kumtazama.
“Anaweza kuwa ni mwizi ananipigia hesabu za kunipora huu mfuko…” Aliwaza kwa nia ya kujaribu kumpuuza ijapokuwa aliamua kumtega ili kujua uhusika wa yule bwana kwenye upigaji wa risasi karibu na miguu yake, risasi ambayo ilitua katikati ya miguu yake. Alijifanya kuvuka barabara huku akiwa anaangalia upande wake wa kushoto. Kwa mtu ambae angelimuona, angelihisi jamaa alikuwa akitazama gari lililokuwa likitokea kituo cha msimbazi kuelekea Kimara, lakini kama angelikuwa makini zaidi angeliweza kuona namna macho yake yalivyokuwa yamekaa kupingana na uelekeo wa uso na yalifuata uelekeo wa miguu yake.
Zuki Gadu p.a.k Miguu ya kuku alikuwa akimchungulia yule jamaa aliyekuwa amevaa koti kwa kutumia pembe ya macho yake, hila zake zilimpa matokeo aliyoyatarajia pale alipoweza kuziona vema nyendo za mtuhumiwa wake namna alivyokuwa akijaribu kuinua mkono wenye bastola, huku akiwa ameuzinga kwenye nguo aliyokuwa ameichagua kutoka kwenye rundo la nguo nyingi zilizokuwa zikiuzwa na machinga.
Kwa wepesi wa hali ya juu aliweza kupiga hatua moja upande wake wa kushoto, kisha akanesa na kuruka kingo ya barabara huku akiwa amemkazia macho mtuhumiwa wake ambae alikuwa amezubaa asielewe kilichokuwa kikiendelea.
Zuki Gadu aliendelea kupiga hatua ndefu huku akiwa hataki kumpoteza mtuhumiwa wake kwenye upeo wa macho yake, alipoona jamaa ameshitukia hila zake, aliamua kuanza kukimbia taratibu jambo lililofanya yule jamaa nae aanze kukimbia bila kujali alikuwa ameshika nguo ambayo hakuilipia. Jamaa mwenye koti alizidi kuongeza kasi huku akiitupa mbali nguo iliyokuwa mkononi mwake na dhahiri kila mmoja aliweza kuiona bastola yake. Kuonekana kwa bastola kwenye mitaa ya kariakoo kuliibua taharuki kwa kila aliyemtizama yule bwana ambae alikuwa akikimbia huku akigeuka nyuma kila mara, alikatiza mtaa mmoja na kwenda kutokea mtaa mwingine, lakini kila alipogeuka aliishia kumuona adui yake akiwa nyuma yake hatua chache zaidi. Hofu ikaanza kuutafuna uimara wa mwili wake na viungo vikaanza kumlegea huku mapigo ya moyo yakiongeza kasi maradufu na akaanza kuhisi asingeliweza kukimbia mita nyingi zaidi. Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa, Zuki Gadu alimwacha akimbie awezavyo huku yeye akiwa nyuma yake, hakutaka kuwahi kumshika japo uwezo huo alikuwa nao. Aliamua kufuata kanuni za riadha ambazo huwapa ushindi wa bure wanariadha wengi wa mbio ndefu. Aliamini mara nyingi mshindani wako akikutangulia na akiwa anageuka nyuma mara kwa mara, hofu itachukua uimara wake na wewe utamfikia kirahisi. Kwanini? Kwa sababu ubongo utashindwa kukubaliana na hali inayotokea na matokeo yake moyo utaongeza kasi ya mapigo na mkimbiaji atachoka au kujitoa kwenye riadha.
Naam! Kanuni hiyo ilifanya kazi vema kwa yule bwana ambae alikuwa amevaa koti la baridi licha ya kuwa na jua na joto kali, kila mara alipogeuka aliishia kuona hatua zake zikipunguzwa na adui yake na dhahiri angeliishia mikononi mwake wakati wowote. Hilo hakutaka litokee, haraka alijichanganya kwenye maduka ya santuri huku akitweta kujaribu kuweka sawa pumzi zake, kila alipogeuka nyuma yake hakuweza kumuona mshindani wake jambo ambalo lilianza kumpa ahueni kichwani mwake, akaificha silaha yake kiunoni mwake kisha akaendelea kuzihesabu korido za maduka ya santuri bila kujali idadi ya watu waliokuwa wakifuatilia nyendo zake baada ya kumuona akiwa na bastola. Alizihesabu korido huku akiwa na nia ya kuzimaliza na kutokea kwenye uchochoro fulani ambao ungelimkutanisha na njia ya kuingilia kwenye kanisa lililokuwa nyuma ya maduka yale.
Hesabu zake zilikuwa sawia kama alivyokuwa amedhamiria, alitokea nyuma ya ukuzio wa kanisa. Alisimama kwa sekunde kadhaa kabla ya kuona geti dogo la dharura kwa waumini na wahudumu wa lile kanisa. Taratibu huku akitazama pande zote, alilifuata lile geti na kulisukuma. Bahati njema ikawa kwake kwani halikufungwa hivyo kwa urahisi akawa ameingia ndani ya uzio wa kanisa na bila wasiwasi alichukua uelekeo wa upande uliokuwa na vyoo, lakini kabla ya kufika huko alibadili uelekeo na kuchukua njia ya kuelekea geti kuu ambalo lilitumika kuingiza na kutoa waumini waliotembea kwa miguu.
Alitembea bila kujali macho ya baadhi ya watu waliokuwa kwenye viwanja vya kanisa ambao walikuwa wakijiuliza maswali mengi bila kupata majibu kuhusu uwepo wake maeneo yale, aliendelea na safari yake hadi alipofanikiwa kufika nje ya uzio wa kanisa. Alishusha pumzi kwa nguvu huku akijishika kiuno chake na kutazama upande wake wa kulia, kisha akapiga hatua zake kulifuata gari jeupe lililokuwa limeegeshwa upande huo. Alipolifikia lile gari hakutaka kungojea, haraka alichomoa ufunguo wake na kufungua mlango na kujitosa ndani, kisha taratibu aliliondoa gari lake huku akijifuta jasho lililokuwa limeanza kukaukia kwenye ngozi yake.
Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa kila kitu alichokuwa anakifanya, kilionwa vema na Zuki Gadu ambae alikuwa nyuma yake hatua zaidi ya ishirini. Wakati jamaa anaingia kwenye viambaza vya uuzaji wa santuri, haraka sana alizunguka upande wa pili ambako kulikuwa na kanisa, akaingia kanisani na kuelekea sehemu ya kuegesha magari huko alijibanza nyuma ya gari aliloona linatosha kumsitiri, kisha akaanza kutizama upande wa lango la kuingilia huku akiwa makini uwepo wake pale usitiliwe shaka. Alifanya vile kwa kuwa alijua yule jamaa baada ya kuingia kwenye maduka ya kuuza santuri ilikuwa ni danganya toto lakini lengo lake lilikuwa ni kutokea upande wa pili ambako angeliingia kanisani kwa kupitia geti dogo ambalo halikuwa likipitika mara kwa mara. Aliotea hivyo kwa kuwa alikuwa anafahamu vichochoro vingi ndani ya kariakoo na posta hadi gerezani. Alifahamu njia zote kwa sababu aliamini ipo siku njia hizo zitamsaidia kwa jambo lolote.
Akiwa palepale amejibanza, macho yaliona kile alichokitarajia. Alimuona yule jamaa akiwa anakimbia na nusu kutembea kuelekea kwenye geti na alipolifikia alitoka nje huku kila mara akigeuka na kutazama alikokuwa akitokea. Alimuona namna alivyoingia kwenye gari na kuondoka.
“Huyu mtu ni nani? Kwa nini anataka kuniua? Kwa nini anaonekana kuniogopa? Nani kamtuma?” Yalikuwa ni maswali mfululizo ambayo yalipita kichwani mwake bila majibu.
“Hakuna wa kunipa majibu zaidi yake.” Alijisemea huku akiangaza huku na huko kuona kama atafanikiwa kupata usafiri wowote ambao ungelimrahisishia kazi yake.
Macho yake hayakumdanganya, aliona pikipiki kubwa ikiwa imeegeshwa umbali wa mita tatu kutoka pale alipokuwa amesimama. Haraka aligeuka huku na huko mithili ya mwizi wa kuku kwenye banda. Licha ya kutumia sekunde kadhaa kuangaza huku na huko lakini hakuona mtu aliyekuwa akimfuatilia nyendo zake. Kwa kasi kubwa aliifuata pikipiki iliyokuwa mbele yake na kuiinamia kwa sekunde chache na alipoinuka alidandia juu na kuiwasha bila kungoja kuletewa ufunguo na mwenye mali, tayari alikuwa ameshanyofoa waya na kuipigisha shoti na pikipiki ikawaka tayari kwa matumizi. Zuki Gadu hakutaka kupoteza wakati, alizungusha pikipiki kama anaewahi mashindano ya kuruka viunzi kisha akaiondoa kwa kasi kubwa bila kujali kelele alizoacha nyuma yake na kero kwa waumini waliokuwa kwenye maombi wakati ule.
Alitokeza barabarani na kuchukua uelekeo ambao yule jamaa alikuwa ameelekea, njiani alikuwa makini kuhakikisha anaiona gari iliyotumiwa na yule mvaa koti wakati wa joto lakini hadi anaikamata Ilala boma, hakuwa amefanikiwa kuiona ile gari jambo ambalo lilimfanya aanze kuhisi atakuwa amekosea kufuatilia nyendo za yule jamaa.
Kwa kuwa alikuwa ameiba pikipiki hakuona kama itakuwa vema kuendelea kuzubaa maeneo ya karibu na eneo alilpora, akachochea moto na kuchukua uelekeo wa barabara ya kuelekea Kinondoni akiwa ameungana na magari yaliyotokea Mbagala na kuelekea makumbusho kupitia mwananyamala. Wakati alipokuwa akizipita ofisi za mkuu wa mkoa mbele yake aliona kile ambacho hakuwa ametarajia kukiona, lile gari lililomfanya aibe pikipiki ya kanisa aliliona likiwa mbele yake mita kadhaa na likiwa kwenye kasi ya kawaida.
Alitabasamu huku akienda kusimamisha pikipiki pembezoni mwa barabara bila kujali uvunjaji wa sheria za barabara kwa kusimama sehemu isiyotakiwa. Baada ya kusimamisha pikipiki akaukumbuka mfuko wake aliokuwa ameuweka karibu na tanki la mafuta huku akiuzuia kwa kuibana miguu yake, aliuchukua na kutoa barakoa nyeusi kisha akaurejesha mahali pake na kabla hajaondoa pikipiki, akainama kuchukua bastola ndogo ambayo alikuwa ameibana na soksi za mguu wake wa kulia, akafyatua kilinda usalama kisha akaishika kwa mkono wake wa kushoto na mkono wa kulia ukavuta mafuta na ule wa kushoto ukatenga vidole vyake kwa kusaidia kuibana bastola na vidole vingine vikiruhusu pikipiki kuingia barabarani. Alipoingia barabarani alivuta mafuta na kuiruhusu pikipiki yake ikimbie juu ya lami huku akiyapita baadhi ya magari yaliyokuwa mbele yake bila kupunguza mwendo, macho yake yalikuwa makini kuhakikisha gari ya adui yake haipotei kwenye upeo wake.
Dakika mbili baadae alikuwa ameikaribia ile gari kwa ukaribu zaidi japokuwa na yenyewe ilikuwa kwenye kasi kubwa huku dereva wake akizipita baadhi ya gari kwa kasi ile ile bila kuchukua tahadhari zaidi, kwake ilikuwa bora uhai kuliko kifo na hakujua kama mwendo wake pia ungeliweza kumsababishia kifo kibaya zaidi ya kile alichokuwa akikimbia.
Zuki Gadu aliinua bastola yake na uilenga ile gari, alifanya vile akiwa nyuma hatua kadhaa na aliamini kwa kufanya vile dereva angelisimamisha gari pembeni, lakini ikawa tofauti na alivyofikiria, dereva hakusimamisha gari licha ya kuona mdomo wa bastola kupitia kioo kilichokuwa mkono wake wa kulia. Kitendo cha dereva kushindwa kujisalimisha kulimlazimisha Zuki kuchukua maamuzi mengine ambayo hakuwa akitaka kuyachukua kwa sababu ya kuogopa kumuua yule jamaa ambae aliamini angelikuwa msaada mkubwa wa kujibu baadhi ya maswali aliyokuwa akijiuliza. Lakini kwa sababu ya ukaidi aliokuwa nao yule bwana, hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kufanya alivyoona inafaa.
Aliamua kufyatua risasi iliyoenda kutua kwenye moja ya gurudumu la gari kitendo kilichosababisha gari ikose mwelekeo na kwenda kujigonga kwenye kingo za barabara na kupaa juu kisha ikajibwaga chini na kusambaratika. Kuanguka kwa lile gari kulimfanya Zuki Gadu apunguze mwendo na hatimae alisimama kabisa na kisha kuigesha pikipiki kando mwa barabara. Alikimbia kwa kasi kuelekea kule ilikokuwa gari aliyoisabishia ajali, aliwahi kufika kabla ya watu wengine waliokuwa wameanza kushuka kwenye magari yao na wengine waliokuwa wakitembea kwa miguu kusogea eneo lile.
Baada ya kufika moja kwa moja alikimbilia upande wa dereva ambapo ambapo alimkuta dereva akiwa amebanwa na usukukani huku akiwa anahema kwa taabu.
Hakujali maumivu yake, alimuuliza…
“Unaitwa nani nani kakutuma?”
Licha ya kuumuuliza kwa sauti kubwa kidogo lakini yule jamaa hakujibu. Alimuuliza tena..
“Kwa nini ulitaka kuniua?”
Jamaa hakuhangaika kujibu badala yake alizungusha kichwa chake taratibu na kumtazama, kisha akazungusha shingo yake na kutazama upande wa kushoto kwake huku akijaribu kusema kitu na asiweze, badala yake akaishia kukoa mabonge ya damu.
Zuki Gadu alitamani kumvuta kwenye gari na kumtoa nje ili amlaze chini lakini alishindwa kufanya hivyo baada ya kuona harakati zozote za kumsaidia, zingeishia kuchukua uhai wake haraka zaidi. Aliona alihitaji kumuuliza akiwa pale pale lakini changamoto nyingine ikaingilia..
Watu! Watu tayari walikuwa wameanza kujaa huku wakimshinikiza aanze kutoa msaada kwa yule mtu badala ya kumwinamia na kumuuliza. Zuki Gadu hakuhitaji watu waendelee kumzonga pia alijua kitakachofuata ni baadhi ya watu kuanza kupiga picha na hakutaka picha yake isambazwe mtandaoni. Alihitaji kufanya maamuzi ya haraka ili kuweka mambo sawa.
Bila kujiuliza alichomoa bastola yake aliyokuwa ameificha kwa kuifunika na shati lake, ilipojaa kwenye mkono wake aliondoa kilinda usalama na kupiga risasi mbili juu.
“Paah! Paah!” Mlio wa risasi ulisabisha patashika barabarani, watu walikimbia hovyo huku kila mmoja akiomba kwa imani yake, wengine walishindwa kuhimili walijikuta wakipiga ukunga wa wiga na wengine wakianguka bila kutarajia.
Hekaheka za wasamalia wema hazikumzuia Zuki kuendelea kumuuliza yule jamaa ambae bado alishindwa kuongea japo alionekana dhahiri kutaka kuzungumza.
“Hey!” Zuki alimshitua baada ya kuona jamaa ameanza kuzungusha tena kichwa chake kama awali, alimshitua kwa sababu alihitaji asikie sauti na si kichwa kikizunguka. Licha ya kukemewa na kuendelea kuulizwa, lakini yule bwana aliendelea kuzungusha kichwa chake kuanzia kulia na kumalizia kushoto. Licha ya kushindwa kuelewa sababu ya yule bwana kuzungusha kichwa chake, lakini alianza kuhisi yule jamaa alikuwa akijaribu kumpa ujumbe fulani kwa ishara. Alitulia huku akiendelea kufuatilia mjongeo wa kichwa na macho ya yule jamaa.
Macho!.
Alifuatilia zaidi mjongeo wa macho na alifanikiwa kuona macho ya yule jamaa yakiangukia upande wake wa kushoto ambapo kulikuwa na mfuko wa shati lake lililokuwa limeloa damu. Kwenye ule mfuko kulikuwa na kalamu iliyokuwa imebana vema kwenye mfuko. Zuki Gadu alioona ile kalamu na bila kusita aliichukua ile kalamu na kuitia mfukoni mwake kisha akaanza kukimbia kuelekea ilipokuwa pikipiki aliyoiba kanisani. Alidandia juu yake na kuliacha lile eneo likiwa bado liko kwenye taharuki kubwa kwa wenyeji na wapitaji wa barabara, huku yeye alishindwa kujua kama alichochukua kitakuwa na msaada wowote au kulikuwa na kitu kingine kilichokuwa kikioneshwa na yule jamaa.
Bado mbele yake kulikuwa na giza.
Endelea kuwa nami.