Kustaafu jaji augustino ramadhani ni shinikizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kustaafu jaji augustino ramadhani ni shinikizo?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mesaka, Dec 28, 2010.

 1. M

  Mesaka Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Habari za Asubuhi wanajamii!

  Jaji Augustino Ramadhani amelitumikia taifa kwa nafasi hiyo kwa miaka mitatu tu! Mabo ambayo najiuliza ni je, Kikwete alipomteua mwaka 2007 hakujua kwamba amebakiza miaka mitatu tu ya kustaafu kwake kwa mujibu wa sheria? na je kama alijua hakuona kwamba analiingizia Taifa Hasara kwa uteuzi huo kwa kuongeza idadi ya majaji wakuu wastaafu?

  Lakini kutokana na kauli za Mwanasheria Mkuu wa serikali, mheshimiwa Jaji Werema, kwamba Tanzania haihitaji katiba mpya, ninapata wazo lingine kwamba huenda misimamo ya jaji Ramadhani ilikuwa tofauti na ya watawala wa serikali, kwani tayari Jaji Ramadhani keshasema katiba Mpya haikwepeki kwa sasa, huyu AG anasema 'haitakiwi' kwa sasa. Je anasoma alama za nyakati?

  AG anasema wanaohitaji marekebisho (Viraka), wampelekee mapendekezo. Je, hivi yuko nchi ama dunia gani ambako ameshindwa hata kunong'onezwa kwamba movement iliyopo sasa Tz ni suala la katiba mpya na si marekebisho? na wanao dai hivyo ni wa Tanzania ambao ndiyo wenye katiba? Au anadhani nchi hii ni ya watawala kama ambavyo katiba iliyopo ilivyo?

  Ndugu zangu watanzania, nadhani Tanzania sasa inahitaji uhuru wake halisi kutoka kwa serikali ya watawala, na hilo litawezekana kwa kuwa na katiba ya watanzania, Hivyo tunapaswa kuungana pamoja kudai katiba mpya na si marekebisho. Yanayotekea sasa na kauli za wapinga katiba mpya si mapya ni yale yale yaliyotumiwa na watawala wa kikoloni kwa waliokuwa wanadai uhuru enzi hizo.

  Naomba kauli y a Jaji Mkuu Mstaafu Jaji Ramadhani inayoungana na Majaji wengine wastaafu na baadhi ya Viongozi kwamba Katiba mpya inahitaji iwe ndiyo kauli ya Jaji Mkuu mpya, Jaji Chande, vinginevyo hakuteuliwa kwa ajili ya watanzania.
   
 2. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kila kitu ni siasa sasa kwani jaji mpya ana miaka mingapi?? lazima atakuwa kwenye hamsini na hukoo.... ila sijaona kama Augustini Ramadhani alikuwa mzee hivyo. Ila nasema ni siasa kwa sababu pengine alisema ukweli na alikuwa na misimamo kwenye mambo ya msingi sana japo bado nadhani hakutoa hukumu ya halali kwenye kesi ya mgombea binafsi..

  Sasa kama kungekuwa na katiba mpya huyu jaji mkuu lazima angechunguzwa kwanza na tume ya sheria pamoja na bunge kabla ya raisi kumpitisha.. lakini huku ni tofauti sana.

  Jamani tunahitaji katiba mpya/.//
   
 3. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jaji Ramadhani amewahi kutamka siku nyingi kwamba hana mpango wa kuongeza mda wa ujaji akifikia umri wa kustaafu. Sioni sababu yoyote ya kuhusisha kustaafu kwake na mtizamamo wake binafsi juu ya mabadiliko ya Katiba. Nijuavyo mimi wapo wengi katika serikali iliyopo wanaounga mkono katiba mpya na pia wapo wengi wanaopinga. Serikali, kwa maoni yangu, bado haijatoa msimamo rasmi wa kiserikali kwamba haitaki katiba mpya. Serikali imetoa nafasi kwa wananchi kujadili juu ya hili. Bila shaka ndio maana hivi juzi katibu mkuu wa wizara ya sheria alipokea rasmu ya katiba ya chama cha wananchi kwa niaba ya waziri. Kwamba katiba mpya inahitajika au la utashi wa wananchi wengi ndio wenye mamlaka ya kuamua. Wale wanaotaka katiba mpya wanapaswa kuuza hoja kwa wananchi ili kwa wingi wao waunge mkono msimamo wao hali kadhalika wale wanaopinga. Hiyo ndio maana sahihi ya mjadala wa mabadiliko ya katiba.

  GEORGE JINASA
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Labda watampatia yeye kuwa kiongozi wa hiyo Tume aliyoiunda Rais Kikwete kwa vile tayari ameonesha kusupport wazo la Katiba Mpya. So itajulikana kama Tume ya Jaji Ramadhani
   
Loading...