Kusokotwa na tumbo (Colic) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusokotwa na tumbo (Colic)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Tumbo Kuuma wanawake wanapoenda mwezini, virusi na mchanganyiko wa vyakula ambavyo hugeuka na kuwa sumu.Unaweza kuzuia kuumwa na tumbo na kuhara kwa kutotumia vyakula vinavyotoa harufu mbaya ya kuchacha.
  Ukiumwa na tumbo unaweza kujitibu:
  Damu ya hedhi

  • Ukiwa mwezini meza tembe kama Panadol au utakayoambiwa na daktari ili kupoteza maumivu.
  • Tumia sodo kwa utulivu wako.
  Virusi vya tumboni

  • Unapotapika, kuwa na homa, kichwa kuuma, misuli kuuma, na viungo vya mwili.Hizi dalili hudumu kwa muda wa masaa 24.
  • Ikiwa unaendesha usimeze dawa ya kujaribu kuzuia kwa muda wa masaa 2-3.
  • Pumzika zaidi.
  • Kula vyakula vyepesi, ndizi, wali, na vinywaji vya matunda.
  • Usile vyakula vilivyo na mafuta mengi, vinzari au bidhaa zozote kutokana na maziwa, pombe, kahawa n.k.
  Mchanganyiko wa vyakula vibaya.
  Unaweza kutapika, kuhara, kuwa na homa au kupungukiwa na maji mwilini.

  • Ukiwa unaendesha unapoumwa na tumbo, usimeze dawa masaa 2-3, inawekana kuwa uchafu uliokuwa tumboni unatoka.
  • Baada ya masaa kadhaa unaweza kumeza madawa ya kuzuia kuendesha Kama "Valoid", utaipata katika maduka ya kuuza madawa.
  • Kunywa maji mengi sana ama vitu vioewevu kama vile chai isiyo na majani mengi, sharubet ya matofaa ama vinywaji vyovyote visivyolewesha ili urudishe mwilini maji uliyoyapoteza wakati ulipokuwa ukiendesha.Pia tangawizi husaidia kutuliza tumbo.Iwapo una wasiwasi kuwa huenda mwili ukanyauka kwa kupoteza maji,basi tumia dawa ya "Redidrat" ya kurudisha maji mwilini.
  • Iwapo utapata hamu ya chakula, kula ule mkate mwembamba au mweupe , ndizi na wali ,vitakusaidia katika kufungisha kuendesha.Usile vyakula vizito vyenye mafuta mengi , vyakula vitokanavyo na maziwa au vile ambavyo ni vya nyuzinyuzi (matunda mabichi ,mboga vyakula vya afya bora vya ngano) wakati ambapo tumbo limevurugika au unaendesha.
  • Pumzika vya kutosha.
  Muite daktari wako iwapo:

  • Kwa ghafla tu unaanza kuendesha na tumbo kuvurugika ama uwe na joto la zaidi ya digirii 38oC .
  • Hali ya tumbo kuvurugika husikika upande wa chini wa kulia wa tumbo yako. (unaweza kuhitajika kuhudumiwa katika chumba cha huduma za dharura iwapo zipo katika sehemu hii.
  • Tumbo linaweza kuvurugika mara kwa mara na kuacha , kasha unaweza kupata mojawapo za ishara hizi au hata mbili au zaidi , kushtuka, mtu kuwa dhaifu, kipigo cha moyo kupiga kwa haraka haraka , kuhisi baridi kali, kuumwa na kifua ,midomo kukauka ,kutapika ,tumbo kufura, tumbo kujaa hewa nyingi na hata mtu kushindwa kutoa hiyo hewa ama kufunga choo, mtu kuwa mnyonge ama kuona kizunguzungu,kwenda haja kubwa nyeusi au iliyo na damu, ukiwa na joto kali, ya zaidi ya digirii 38oC ama hewa inayotoka mdomoni kunuka .
  • Hali ya tumbo kuvurugika huwa haishi iwapo utaitibu mwenyewe kwa siku 2 au 3.
   
Loading...