Kusini: Korosho kuzinyima mapato Halmashauri mwaka huu 2018/2019

Kusini: Korosho kuzinyima mapato Halmashauri mwaka huu 2018/2019

Malova

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2011
Posts
784
Reaction score
228
Halmashauri nyingi za Mikoa ya Kusini zinategemea ushuru wa mazao mbali mbali kama chanzo yamapato ya ndani. Korosho ni zao moja ambalo lilikuwa linaziingizia Halmashauri fedha nyingi za ndani. Kwa mfumo wa ununuzi wa korosho wa msimu huu wa 2018/2019, Halmashauri zinaonekana zitakosa mapato yatokanayo ya ushuru katika zao hilo. Sababu kuu ni kwamba bei aliyotangaza bwana mkuwa ya 3,300/= italipwa kwa mkulim amoja kwa moja. Maana yake hatutakuwa na makato kwa ajili ya vyama vya msingi wala Halmashauri. Jambo hilo linaonesha Halmashauri nyingi zitayumba sana kwa huu. Hazitaweza kujiendesha.

Kuna Halmashauri moja ilitarajia kukusana takribani 2,700,000,000/= kwa mwaka 2018/2019 kati ya hizo takribani Tshs 1,800,000,000/= ilitegemewa ipatikane kutokana na uhuru wa korosho pekee. Pesa hiyo isipopatikana maana yake Halmashauri hiyo haitaweza kujiendesha. Mazao mengine ambayo yalitakiwa yachangie kwenye mapato ni pamoja na choroko na mbaazi ambayo hadi sasa hayana soko na wakulima ni kama wameacha kulima mazao hayo. Madiwani wa Halmashauri hiyo hawajalipwa posho zao za mwezi na zile za vikao vya kamati pamoja na baraza tangu Mwezi wa sita 2018. Sababu ni kwamba Halmashauri haina fedha za ndani za kulipa posho hizo.

Wanaomshauri Bwana mkubwa wangemuambia jambo hili ili ajue. vinginevyo Halmashauri nyingi za Kuisni hazitaweza kujiendesha kwa sababu hazitakuwa na fedha.
 
Kanuni ya msingi ya biashara huria inapovunjwa, kwa serikali kuingilia kupanga bei katika soko au kuwa kinara wa ununuzi, uagizaji na upelekaji bidhaa nje lazima sehemu fulani kiuchumi ziyumbe. Hayo ndio yaliyomshinda baba wa taifa mpaka ikamlazimu ang'atuke baadae ya uchumi wa nchi kwenda kombo.
 
Kanuni y msingi ya biashara huria inapovunjwa, kwa serikali kuingilia kupanga bei katika soko au kuwa kinara wa ununuzi, uagizaji na upelekaji bidhaa nje lazima sehemu fulani kiuchumi ziyumbe
Exactly
 
Kuna faida gani kodi kwenda kulipa posho madiwani.
Madiwani wanalipwa posho kutokana namakusanyo ya ndani ya Halmashauri husika. Sasa kama Halmashauri hiyo chanzo chake ni ushuru wa mazao ikiwemo korosho tatizo linakuwa wapi?
 
Hili ni jambo la kheri tupu. Nadhani sahihi zaidi ni kuwasema: halamashauri zitakosa fedha za kufisadi.
 
Madiwani wanalipwa posho kutokana namakusanyo ya ndani ya Halmashauri husika. Sasa kama Halmashauri hiyo chanzo chake ni ushuru wa mazao ikiwemo korosho tatizo linakuwa wapi?
Madiwani wanaolipwa kutokana na mauzo ya korosho wao wamefanya nini kwa walima korosho ili korosho iwanufaishe mkulima mmoja mmoja???
 
Kanuni ya msingi ya biashara huria inapovunjwa, kwa serikali kuingilia kupanga bei katika soko au kuwa kinara wa ununuzi, uagizaji na upelekaji bidhaa nje lazima sehemu fulani kiuchumi ziyumbe. Hayo ndio yaliyomshinda baba wa taifa mpaka ikamlazimu ang'atuke baadae ya uchumi wa nchi kwenda kombo.

Kama kung'atuka ndi utaratibu wetulabda mshikaji naye anataka kufanya hivyo!
 
Back
Top Bottom