Kusimikwa kwa wale kumi na mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusimikwa kwa wale kumi na mbili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, May 18, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kabla ya ordination kuanza rasmi Yesu aliongea na wale kumi na mbili,walipokaa kumzunguka.Akasema,
  ''Ndugu zangu,hii saa ya ufalme imefika. Nimewaleta hapa pembeni ili niwatambulishe kwa Baba kama mabalozi wa ufalme. Wengine wenu mmenisikia nikizungumza kuhusu huu ufalme katika sinagogi[synagogue]mlipoitwa kwanza. Kila mmoja wenu amejifunza zaidi kuhusu ufalme wa Baba mlivyofanya kazi na mimi katika miji inayozunguka bahari ya Galilaya.
  ''Ufalme mpya ambao Baba yangu amekaribia kuuanzisha katika mioyo ya watoto wake wa duniani utakuwa utawala wa milele. Hakutakuwa na mwisho wa huu utawala katika mioyo ya wale wenye hamu ya kufanya utashi wake mtakatifu.Nawaambia kwamba Baba yangu siyo Mungu wa Myahudi au ambaye siyo Myahudi. Wengi watakuja kutoka mashariki na kutoka magharibi kukaa na sisi katika ufalme wa Baba,wakati wengi wa watoto wa Abrahamu watakataa kuingia katika huu undugu mpya wa utawala wa roho ya Baba katika mioyo ya watoto wa binadamu.
  ''Uweza wa huu ufalme utakuwa siyo katika nguvu za majeshi au katika nguvu za utajiri,bali katika utukufu wa roho ya kitakatifu itakayokuja kufundisha akili na kutawala mioyo ya raia waliozaliwa upya katika huu ufalme wa kimungu,watoto wa Mungu[sons of God]. Huu ndio undugu wa upendo,ambapo haki inatawala,na ambao kilio chao cha vita kitakuwa ''Amani duniani na nia njema kwa watu wote.[Peace on earth and good will to all men]Ufalme huu ambao hivi punde mtakwenda kuutangaza,ndio matamanio ya watu wema[good men]wa zama zote,matumaini ya dunia yote,na kutimiza[fulfilment]kwa ahadi za hekima za manabii wote.
  ''Lakini kwenu nyinyi,watoto wangu na kwa wale wote watakaowafuata katika huu ufalme,watawekewa mtihani mkubwa. Imani peke yake itakuwezesha kupita katika milango yake,lakini lazima ulete matunda ya roho ya Baba yangu kama unataka kupanda juu katika maisha ya kuendelea kujumuika na watakatifu wengine. Kweili kabisa nawaambia siyo kila mtu anayesema,'Bwana,Bwana' ataingia mbinguni,ila yule tu anayefanya utashi wa Baba yangu aliye mbinguni.
  ''Ujumbe wenu kwa dunia utakuwa;Tafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake,na katika kupata hivi,mambo yote mengine muhimu kwa uhai wa milele utayapata. Na sasa nataka kuwaeleza wazi kwamba ufalme huu wa Baba yangu hautakuja kwa onyesho lolote la nguvu au kwa maandamano yoyote yasiyofaa. Unapokwenda kutangaza ufalme usiseme 'uko hapa au uko pale'kwa vile huu ufalme unaohubiri ni Mungu ndani yako.
  ''Yoyote atakayekuwa mkubwa katika katika ufalme wa Baba yangu atakuwa waziri kwa wote;na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu,awe mtumishi wa ndugu wote.Lakini mtakapopokelewa katika ufalme wa kimungu,hamtakuwa watumishi,mtakuwa watoto,watoto wa Mumgu aliye hai[sons of the living God]. Na hivi ndivyo huu ufalme utakavyoendelea katika dunia mpaka utakaposhinda kila kikwazo na kuwaleta watu wote[all men]kumfahamu Baba yangu na kuuamini ukweli unaookoa ambao mmekuja kuutangaza.
  ''Na hili ambalo mnaliona sasa,huu mwanzo mdogo wa watu wa kawaida kumi na mbili,utaongezeka na kukua mpaka hatimaye dunia yote itajaa utukufu wa Baba yangu. Na itakuwa siyo zaidi kwa maneno mtakayoongea isipokuwa kwa maisha mnayoishi ndio watu watajua mlikuwa na mimi na mmejifunza kweli[realities]za ufalme;na ingawa sitaki kuweka mzigo mkubwa katika akili zenu,lakini nimekaribia kuwapa jukumu la kuniwakilisha katika dunia,baada ya mimi kuondoka kama ambavyo mimi namwakilisha Baba yangu katika maisha haya ninayoishi katika mwili''
  Alipomaliza kuzungumza akasimama.
   
Loading...