Kusikia kwa kenge........

Kusikia kwa kenge........

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
326
Reaction score
67
Zipo simulizi nyingi zinazohusiana na tabia ya kukosa usikivu na ufahamu wa kutenda jambo sahihi kwa wakati unaofaa. Kutokana na madhara ya yatokanayo na tabia hiyo upo usemi usemao kwamba, 'kusikia kwa kenge mpaka atokwe damu sikioni'. Usemi huu unaleta ladha na maana nzuri zaidi nikiutamka kwa lugha ya kisukuma...' gwiigwa go mbulu miininga mmatu'. Kwa kifupi unaashiria tabia ya mtu asiyesikia la mtu! Yeye ni yeye anajua yote siku zote. Ukijaribu kumwonya na hata kumwambia madhara yanayoweza kumpata kwa tabia au misimamo yake atakwambia mimi ninaelewa. Tabia hii huendelea hadi atakapopata madhara makubwa yanayowakilishwa matumizi ya lugha ya picha ya 'kenge, damu' na sikio/masikio'.Itokeapo damu ndipo kenge hukurupuka mbio akijua ameumia huku tayari akiwa amechelewa kuchukua hatua hiyo.

Tabia hii ya kenge ipo kwa ccm ambayo siku zote huchukua hatua baada ya tatizo kuwa kubwa ambalo pengine si rahisi kulirekebisha tena.Tazama matokeo ya f4! Cha kushangaza waziri anasema shule za serikali hazina 'facilities' wala walimu wa kutosha wakati za binafsi zina 'facilities' na walimu wa kutosha. Mimi ni mwl na kawambwa ni bosi wangu, najiuliza kuwa hizi shule za binafsi ambazo kawambwa huwa hazipi mgawo wa walimu zinatoa wapi walimu wa kutosha? Je, anajua hao ni wahitimu wa vyuo gani? kama ni vyuo vya kitanzania ambako walimu wa shule za serikali wanatoka wanapangiwa huko na nani? Je, ni walimu wangapi hupangiwa shule za serikali lakini wakaishia shule za private na kwa sababu gani ? Ok, anapotutangazia sisi kuwa shule hazijitoshelezi kwa miundo mbinu na walimu,hilo ni tatizo la nani? Anataka kutuaminisha nini juu ya hili tukiwa tumeshuhudia mbwembwe na matumizi ya mamilioni kwa kutimiza miaka 50 ya uhuru karibu sawa na nchi kama china, cuba, korea na nyiginezo?

Mimi binafsi ninaamini kuwa kawaida ya kenge huwa hasikii chochote! Piga uwezavyo kama hajatoka damu na akaona hawezi kuchukua hatua! Inasemekana anaweza hata kuuawa lakini akiona damu basi hujitutumua kukimbia. Tanzania imeshamegwa vipande viwili hatari sana:yaani walio na wasio nacho. Naamini watoto wa wakubwa hawa wanasoma kule kwenye walimu wa kutosha na facilities lufufu. Kwa wasio nacho St Kayumba/kata ambako tusitarajie muujiza kwa ccm eti zitaboreshwa.

Kwa upande mwingine, raia wa tanzania nao ni kama kenge anayengoja damu imtoke sikioni ndipo achukue hatua. Tusipochukua hatua watawala wa nchi watasomesha watoto wao na kuwa na elimu bora na ndio watakaoshika dola na maeneo mengine muhimu. Watagawana rasilimali zetu zote maana tunangoja damu sikioni. Nawaomba watanzania 2015 tutumie vizuri nafasi ya kupiga kura. Kwa hili la kura, PEOPLEEEEEEES POWER NDILO CHAGUO BORA!
 
Back
Top Bottom